Hii ndiyo mipango na maneno ya mwisho ya January na Maharage. Jee yataendelea kuwa na mashiko?

Hii ndiyo mipango na maneno ya mwisho ya January na Maharage. Jee yataendelea kuwa na mashiko?

Baada ya kupatikana Mwenyekiti mpya wa Bodi na Mkurugenzi mtendaji Tuna hitaji kuona Wajumbe wapya wa Bodi ili tujue muelekeo wa hili shirika.
 
Lakini kwanini juzi Hapa wamesema wamepata Faisal ya billion 100baada ya kuobgeza mishahara ya wafanyakazi..Iweje ghafla Bini vuu Hali ikawa mbaya hivi
 
Nashangaa wanapata wapi nguvu ya kuuza umeme nje ta nchi ilihali ndani umeme uko juu? Kwanini wasiendane na wazo la Magufuli tuzalishe umeme wa kutosha ili tushushe bei ya umeme ili viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa bei ndogo ttuze bidhaa za viwandan mpaka nje ya nchi kwa bei ndogo! Na pia itasadia kuvutia wawekezaji wa viwanda cos tutakuwa na reli ya SGR tayari, maziwa yetu yalikuwa tayari na meli pamoja na shirika la mdege kusimama!
 
1. Mahitaji ya umeme yameongezeka mara 8 zaidi ya awali.

2. Tunahitaji Tri+ kufanya maboresho ya miundombinu ya njia za umeme

3. Hata bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere likikamilika umeme utaendelea kuwa wa mgao kwakuwa shirika litauza nje ili kulipa deni la ujenzi wa bwawa.

TANESCO NI LIDUDE FLAN IVI LIKUBWA, SIO RAHISI KAMA TUNAVYODHANIA, HASA UKIPEWA KULIONGOZA. KUNA MIZIZI NI UNTOUCHABLE.
Sawa lakini tujiulize kwa nini tanesco imekuwa dudu gumu sana kuliongoza tangia kipindi cha Lowassa na Kikwete? Ni kirusi gani kiliingia ndani ya hilo shirika ambacho hakina dawa wala kinga? Mbona awamu ya tano chini ya Magufuli iliweza kupata formula ya kudhibiti hicho kirusi?

Mbona nchi zingine mashirika yao ya umeme haya matatizo na yanaendeshwa tu kiurahisi. Sisi kama nchi ya uchumi wa kati, tunashindwaje na nchi kama ya Burundi kuongoza shirika letu hili mhimu kwa uchumi wa nchi? Tunathubutuje kuweka ma comedian wa aina ya Maharage, Makamba na yule wa EWURA kuongoza shirika hili muhimu wakiwa chini ya mjanja Eng. Mramba? Halafu tunatafuta eti mchawi wakati kila kitu kiko wazi, wachawi wanajulikana hadharani.

Ngoja tusubiri huyu mnyamwezi aliyebebeshwa hilo zigo. Labda anaifahamu ile formula aliyotumia Jiwe kulibeba salama hilo zigo.
 
Back
Top Bottom