Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

Hii ndiyo orodha ya maamuzi ya ovyo kuwahi kufanyika Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

2. Kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano. Hili jambo ukichanganya na matokeo ya jambo la kwanza limeturudisha nyuma sana. Leo hii Watanzania wengi wanaogopa kupambania fursa zinazopatikana duniani kwa kutokujua lugha tu. Lugha imepelekea pia kukosa fursa nyingi sana kwa Watanzania za ndani na nje.

3. Kuruhusu watu kujenga maeneo ambayo hayajapangwa wala kupimwa. Hili hadi leo limesababisha sehemu kubwa ya nchi yetu kujengwa hovyo bila mpangilio.

4. Utaifishaji wa Mali hasa Makampuni na Taasisi zilizokuwa zinajiendesha vizuri. Hili lilitokana na sera za ujamaa. Mali nyingi zilizotaifishwa hatukuweza kuziendeleza na ilikuja kusababisha uchumi wetu kuwa duni sana. Hadi leo hatujutii hili jambo

5. Kuvunja mikataba ya uwekezaji kwa Kiki za kisiasa. Hili jambo limetugharimu na litakuja kutugharimu sana huko mbeleni. Nchi hii imewapa wanasiasa nguvu kubwa sana ya kuamua mambo na imefika kipindi hawajali hata sheria na taratibu. Maamuzi yao hayahojiwi hivyo kupelekea kila siku tumekuwa tukiumizwa na maamuzi hayo.

6. Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji

NYONGEZA
7. Kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi. Kusema kweli ule mji haupendezi na utaligharimu taifa fedha nyingi sana kuupendezesha. Una kaukame kamoja kabaya sana na maji magumu sana. Kuna mda hadi pipes za kuingia majumbani zinaziba kwa sababu ya chumvi.

Sababu zilizotumika kuufanya kuwa Makao Makuu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu
Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 moja. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji
no:5 ukosahihi sana mkuu
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi wakitegemea Serikali kuwafanyia kila kitu

a Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Dah

Unaweza ujinga sana
 
Kuunda Muungano wa Serikali 2. Kiukweli muungano kama Muungano ulitakiwa kuwa wa Serikali 1 tu. Huu uwingi wa Serikali ni uchu wetu sisi waafrika kutaka nafasi ili kujipatia ulaji
Ikiwa hili lilikuwa kosa, dawa yake ni kuuvunja. Uvunjeni basi kuondoa maamuzi ya ovyo, ila hamfanyi kwani mna mawazo ya kikoloni kutaka kuitawala Zanzibar.
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazu ya nchi sikubaliani nazo na ingekuwa uamuzi wangu ningechagua sehemu yenye kijani na maji safi kama Mkoa wa Pwani, Morogoro au Arusha kuufanya Makao Makuu.
Namba tano kwa kweli inasikitisha.

Nakumbuka kipindi cha corona kuna mama majamzito alifia hospitalini kwetu kwa sababu ya corona.

Sasa mimi ni kaandika kuwa sababu ya kifo ni korona. Weeeh. Wanasiasa waliniwashia moto eti mkuu wa nchi ameshasema hamna corona. Sasa wewe unachafua mkoa wetu na sisi tutakuchafua. Issue ile iliniudhi sana maana hata ndugu walijua kuwa mgonjwa wao amekufa kwa korona sasa mwanasiasa anakataa. Wanasiasa ni shida.
 
1. Kuanzisha Azimio la Arusha mwaka 1967. Uamuzi huu ulipelekea jamii nyingi sana kuingia kwenye umaskini na nyingi hazijaondoka kwenye umaskini hadi leo. Pia imefanya jamii nyingi kuwa na akili mfu na kutopenda kufanya kazi
8. Wakristo na waislamu kuongoza nchi Kwa zamu ya Miaka Kumi kumi. Tunahitaji Ráisi mmoja tu mchapa kazi hata kwa Miaka 30
 
Naona wajinga leo mmeamka na Nyerere baada ya lile la udini kufeli, na hapa mtafeli pia, najua mmetumwa kuzima moto wa bandari zetu unaoendelea kuwawakia nyie wasaliti na vibaraka wa shetani.

Iko hivi; unapomlaumu Nyerere leo, miaka zaidi ya 20 baada ya kifo chake, na miaka zaidi ya 30, baada ya Nyerere kutoka madarakani, unaonesha ulivyo na akili mfu, na hilo sio kosa la Nyerere kama ulivyoandika, ni kosa la wazazi wako kukupeleka shule za hovyo.

Kwasababu ukitazama vizuri hiyo miaka, utakuta kuna miaka karibia 40 tangu Nyerere aondoke madarakani, sasa kitu gani kinawashinda kubadili hali hiyo hata baada ya miaka yote hiyo kupita?

Hebu tuambie, ni kipi kati ya hayo yote uliyoorodhesha hapo juu kinachohitaji kubadilishwa baada ya miaka zaidi ya 50 ili tumlaumu Nyerere? na kama sio unakurupuka tu, ni nini kingine?

Tena wewe Lord denning ndie chawa mzembe unayepigia debe ule mkataba wa hovyo wa bandari zetu watanganyika, wenye terms za kinyonyaji kwetu, halafu kwa ujinga wako unamlaumu Nyerere! kwamba Nyerere ndie alikutuma uwe mjinga kupigia debe ule mkataba wa hovyo?

Hauna akili.
 
Back
Top Bottom