Hii ndiyo pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle)

Hii ndiyo pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle)

Yote hayo yanaweza yakawa yanasababishwa na nguvu za kishetani
Haya mambo yana siri kubwa ndo maana kila mtu ana majibu yake wakija wataalum ndo wanakujibu kuna force ya maji yanayozunguka akija mtu wa dini anakwambia ni nyumba ya shetani
 
Hakuna muujiza wowote hapo ni kwamba center of gravity of the earth iko hapo, kwa hiyo kuna kuwa na nguvu nyingi za mvutano (attraction forces) zinazopelekea vitu vingi kuvutwa once crosses that particular area
 
Nadhani NASA wameshakupa sababu kuna nguvu ya usumaku ndio sababu ya kisayansi.

Labda kama unataka sababu kwa mjibu wa conspiracy theories tupo tayari pia ila tegemea majibu mengi na yatakayokuchanganya.
Nitamuuliza babu
 
Black hole [emoji23][emoji23][emoji23] u can't be serious brother/sister/mother/father may u plz go find more education on black holes.
How do you relate black holes na kuzama kwa meli kwenye zone ya Bermuda triangle




Guys msijibu things u have no understanding of

A black hole is a region of spacetime exhibiting such strong gravitational effects that nothing—not even particles and electromagnetic radiation such as light—can escape from inside it. Wikipedia
Chagua kuandika lugha moja kama ni Kiswahili au Kiingereza,hii tabia ya kuchanganya changanya waachie wale mabinti wa Bongo Movie.
 
Ukikomaa na stori za masheikh wa Bakwata unaweza acha kutumia kila kitu duniani.

Wanajitia wanajua ufreemason wakati info wanazichimba kuoitia device ambazo wenyewe wanazipinga.

Tawi la ccm / Bakwata ni hatari sana.
 
Pembetatu ya Bermuda (kwa Kiingereza: Bermuda Triangle) ni eneo la Bahari ya Atlantiki pande zote mbili za ikweta mbele ya pwani ya Amerika Kaskazini, baina ya Florida, Puerto Rico na visiwa vya Bermuda. Tangu mwaka 1964 jina la "pembetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili

Kitabu cha Charles Berlitz cha mwaka 1974 "The Bermuda Triangle "kiliuzwa mara milioni na kusambaza habari za eneo lililoaminiwa kuwa na
hatari za pekee. Inadaiwa kutoweka kwa ndege na meli katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama makosa ya binadamu, uharamia, hitilafu ya vifaa, au maafa ya asilia.

Tamaduni maarufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo
haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi,
kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida .

Nyaraka nyingi hufunua, hata hivyo, kwamba sehemu
kubwa ya madai ya matukio haya ya kidude
hayajaripotiwa kwa makini au baadaye yali rembeshwa na waandishi, na mashirika rasmi
mbalimbali yamesema kwamba idadi na aina za kutoweka katika eneo hili ni sawa na eneo lolote la bahari.

Mipaka ya pembetatu imetanda hadi kwenye Straits ya Florida, Bahamas na eneo zima la kisiwa cha Karibiani na mashariki ya Atlantika hadi Azori; wengine huiongeza hadi kwenye Ghuba ya Meksiko . Mipaka inayojulikana sana ya pembe tatu katika kazi
za uandishi ina ncha zake mahali fulani kwenye
pwani ya Atlantiki Miami, San Juan, Puerto Rico, na Atlantiki ya katikati ya kisiwa cha Bermuda, huku ajali nyingi zikitokea kando ya mpaka wa kusini karibu na
Bahamas Straits ya Florida. Eneo hili ni mojawapo ya njia zinazotumiwa sana na
meli ulimwenguni, huku meli zikivuka eneo hili kila
siku ili kwenda bandari katika Amerika, Ulaya, na Visiwa vya Karibiani.

Meli za vinjari pia ni nyingi,na dau za raha mara kwa mara hupitia hapa kwenda kati ya Florida na visiwa. Pia ni njia inayopitiwa sana na ngege za kibiashara na kibinafsi zikielekea Florida, Karibiani, na Amerika ya Kusini kutoka kwa pointi zilizoko kaskazini.

Historia Chimbuko Madai ya awali kabisa kuhusu kutoweka kusio kwa kawaida katika eneo la Bermuda yatokea katika makala ya 16 Septemba 1950 Associated Press yaliyoandikwa na EVW Jones. Miaka miwili baadaye, jalida la fate lilichapisha "Sea Mystery At Our Back Door ", makala fupi yaliyoandikwa na George X.Sand yaliyohusu kutoweka kwa ndege na meli kadhaa, zikiwemo kupotewa kwa Flight 19, ya kundi la tano la la mabaharia wa US TBM Avenge wakurusha mabomu waliokuwa katika misheni ya mafunzo Makala ya Sand yalikuwa ya kwanza kuweka vilivyo eneo linalojulikana sasa la pembe tatu ambapo kutoweka huku kulitokea. Flight 19 peke yake ilishughulukiwa katika toleo la Aprili 1962 la jalida la American Legion.

Ilidaiwa kuwa kiongozi wa ndege alisikia akisema "Tunaingia njia ya maji meupe, hakuna kitu kinachonekana kuwa sahihi. Hatujui tuko wapi sisi, maji ni ya kijani kibichi, si meupe." Pia alidai kuwa maafisa katika bodi ya uchunguzi wa mabaharia walisema kuwa ndege "ilienda kwa Mirihi." Makala ya Sand yalikuwa ya kwanza kupendekeza jambo la kimiujiza kwa tukio la Flight 19. Februari 1964 katika toleo la Argosy, makala ya Vincent Gaddis "The Deadly Bermuda Triangle" alisema kuwa Flight 19 na kutoweka kwingine kulikuwa sehemu ya mtindo wa matukio ya ajabu katika eneo hili. Mwaka ujao, Gaddis aliezea na kupanua makala haya katika kitabu, Invisible Horizons.

Wengine wangefuata na kazi zao, wakitilia nguvu wazo la Gaddis: John Wallace Spencer (Limbo wa Lost, 1969, repr. 1973); Charles Berlitz (The Bermuda Triangle, 1974); Richard Winer (The Devil's Triangle, 1974), na wengine wengi, wote wakitilia maanani baadhi ya vipengele vya kimiujiza sawa na ilivyoainishwa na Eckert.
 
Triangle ni umbo kama ilivyo Trapeze
Dah, nimekumbuka shule ya msingi, Mambo ya Trapeza yalinipiga sana chenga. By the way nilipenda sana Sayansi, Jiografia na Lugha.
Ila ndiyo hivyo tena!
 
Habari ya muda huu wanajanvi.

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu .


Hadithi ya Bermuda Triangle ni kilinge cha kuundwa kilicho anzishwa na kuenezwa na waandishi kwa makusudi au kwa kutojua , walitumia kauli zisizo sahihi pamoja na hoja zisizo kamilika kuuaminisha ulimwengu kuwepo kwa mambo ya ajabu ( miujiza ) katika eneo la Bermuda Triangle.



Screenshot_20190621-182828.png



[emoji117]Hoja ya kwanza; tukio la kupotea Donald Crowhurst mwaka 1969.

Mfanya biashara raia wa Ungereza Donald Crowhurst ambae pia aliekuwa mwanamichezo wa mbio za majini .Mwaka 1968 - 1969 katika shindano la kuuzunguka ulimwengu lililoandaliwa na " The Sunday Times Golden Global Race " lililo husisha washiliki kuuzunguka ulimwengu kupitia bahari. Donald Crowhurst akiwa mmoja wa washiliki hao alipata ajari na kupotea baharini mwaka 1968 .
Aidha Charles Berlitz mwandishi wa kitabu cha " The Bermuda Triangle, 1974 aliliwasilisha tukio hilo kama kilinge licha ya ushahidi wa wazi uliokuwa kinyume na maelezo ya bwana Berlitz.


[emoji117]Hoja ya pili; Bermuda Triangle kuhusishwa na kupotea kwa Flight 19.

Kupotea kwa ndege ya kuangusha mabomu ya Grumman TBM Avenger Torpedo katika eneo la pembe tatu ya Bermuda munamo December 5, 1945 lilikuwa ni tukio la kustaajabisha na lililopelekea kuandikwa kwa habari nyingi zilizo tiwa chunvi huku zikihusishwa na Bermuda Triangle.
Aidha inadaiwa chanzo cha kupotea kwa ndege hiyo ni kupotea kwa mawasiliano wakati ndege hiyo ilipokuwa katika mafunzo . Wachunguzi wa jeshi la majini hawakuweza kutambua sababu halisi ya kupotea kwa Flight 19.

Aidha mwandishi wa makala ya " The Deadly Bermuda Triangle " alisema kuwa, kutoweka kwa Flight 19 kulikuwa sehemu ya mtindo wa matukio ya ajabu katika eneo la Bermuda Triangle. Jambo ambalo lilikuja kukanushwa na Lawrence David Kusche , mtafiti wa makitaba kutoka chuo kikuu cha Arizona State. Alisema kuwa madai mengi juu ya kupotea vitu katika eneo la Bermuda Triangle yalikuwa ya kutiwa chunvi , ya uwongo au yasiyoweza kuthibitishwa.



Hitimisho;
Waandishi wa Bermuda Triangle wametumia idadi kadhaa ya zana za miujiza kuelezea matukio ikiwemo teknolojia iliyo baki kutoka hadithi za bara la Atlantis.


[emoji762] By Alseneta Sir [emoji762]
 
Ni ngumu kumtenganisha binadamu na ushirikina awe mweupe au mweusi.Hata huku kwetu Afrika Kuna maeneo tunaamini watu na vitu hupotea kimaajabu.

Ndio yaleyale ya vitu huku tukiita vibwengo kule wanaita aliens.Kumbe tofauti technology tu ila ushirikina ni uleule.
Alliens sio vibwengo mkuu
 
Back
Top Bottom