Habari ya muda huu wanajanvi.
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu .
Hadithi ya Bermuda Triangle ni kilinge cha kuundwa kilicho anzishwa na kuenezwa na waandishi kwa makusudi au kwa kutojua , walitumia kauli zisizo sahihi pamoja na hoja zisizo kamilika kuuaminisha ulimwengu kuwepo kwa mambo ya ajabu ( miujiza ) katika eneo la Bermuda Triangle.
[emoji117]Hoja ya kwanza; tukio la kupotea Donald Crowhurst mwaka 1969.
Mfanya biashara raia wa Ungereza Donald Crowhurst ambae pia aliekuwa mwanamichezo wa mbio za majini .Mwaka 1968 - 1969 katika shindano la kuuzunguka ulimwengu lililoandaliwa na " The Sunday Times Golden Global Race " lililo husisha washiliki kuuzunguka ulimwengu kupitia bahari. Donald Crowhurst akiwa mmoja wa washiliki hao alipata ajari na kupotea baharini mwaka 1968 .
Aidha Charles Berlitz mwandishi wa kitabu cha " The Bermuda Triangle, 1974 aliliwasilisha tukio hilo kama kilinge licha ya ushahidi wa wazi uliokuwa kinyume na maelezo ya bwana Berlitz.
[emoji117]Hoja ya pili; Bermuda Triangle kuhusishwa na kupotea kwa Flight 19.
Kupotea kwa ndege ya kuangusha mabomu ya Grumman TBM Avenger Torpedo katika eneo la pembe tatu ya Bermuda munamo December 5, 1945 lilikuwa ni tukio la kustaajabisha na lililopelekea kuandikwa kwa habari nyingi zilizo tiwa chunvi huku zikihusishwa na Bermuda Triangle.
Aidha inadaiwa chanzo cha kupotea kwa ndege hiyo ni kupotea kwa mawasiliano wakati ndege hiyo ilipokuwa katika mafunzo . Wachunguzi wa jeshi la majini hawakuweza kutambua sababu halisi ya kupotea kwa Flight 19.
Aidha mwandishi wa makala ya " The Deadly Bermuda Triangle " alisema kuwa, kutoweka kwa Flight 19 kulikuwa sehemu ya mtindo wa matukio ya ajabu katika eneo la Bermuda Triangle. Jambo ambalo lilikuja kukanushwa na Lawrence David Kusche , mtafiti wa makitaba kutoka chuo kikuu cha Arizona State. Alisema kuwa madai mengi juu ya kupotea vitu katika eneo la Bermuda Triangle yalikuwa ya kutiwa chunvi , ya uwongo au yasiyoweza kuthibitishwa.
Hitimisho;
Waandishi wa Bermuda Triangle wametumia idadi kadhaa ya zana za miujiza kuelezea matukio ikiwemo teknolojia iliyo baki kutoka hadithi za bara la Atlantis.
[emoji762] By Alseneta Sir [emoji762]