Hii ndiyo pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle)

Hii ndiyo pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle)

Nimesoma machapisho mengi kuhusu hii dhana lakini nimetoka kapa, ingawa wikipedia inasema suala hilo limeongezwa chumvi sana. Je The Bermuda Triangle,ni kitu gani na kuna ushahidi gani kwamba ina exist? na Je ni kweli ni lango la kuzimu kama baadhi wanavyodai?



Angalia hiyo ina majibu yote unayohitaji so far about that section: NATGeo Documentary,
 
Pembe tatu ya Bemuda ni eneo lililoko bahari ya Atlantiki ikiwa inapakana na Miami ,Bemuda na Puertorico sehemu ambapo meli na ndege nyingi zimepata kupotea katika mazingira tatanishi sana kiasi kwamba watu wameshindwa kuelezea na kujikuta akisema pana maajabu yasiyoelezeka.

katika mazingira hayo yasiyoelezeka na ya kutatanisha kuna moja ya U.S Navy bomber alipoteza uelekeo wa ndege na wakati anaruka kwenye neneo hilo na ndege haijawahi kupatiakana. baadhi ya boti na ndege na meli zimekua zikipotea kwenye eneo hili kwenye mazingira mazuri tu ya hali ya hewa hata bila kuripoti kwamba kuna tatizo la hali ya hewa hutokea tu ghafla. Pamoja na kuwa na nadharia kwamba eneo hilo ni la kuogopwa kutokana na kupotea huko kwa kutatanisha kwa baadhi ya vyomba vaya anga na majini bila kupatikana bado hakuna udhibitisho kwamba ni eneo hatari sana maana kila uchwao bado kuna vyomba vinakatiza eneo hilo salama salimini wa salamat bila kupatwa na maswahibu hayo ya kupotea.

WADAU WA BEMUDA WANASEMAJE

Sehemu hii inayoitwa pembe tatu ya bemuda au pembe tatu ya shetani (Devil’s Triangle) ina ukubwa wa laki tano squire miles ya eneo la bahari upande wa kusini mashariki wa jimbo la Florida marekani. kwa wanahistorial wanamklumbuka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Christopher Columbus yeye anasema kwamba wakati amefika maeneo haya kwa mara ya kwanza ambapo inasemekana yeye ndio aliyegundua eneo la marekani aliripoti kwamba aliona moto mkubwa ukidondoka eneo hilo na inasadikika kwamba ni kimondo. Anaendelea kwamba baada ya wiki kadhaa palitokea mwanga flani ambao yeye hakuelewa ni wa kitu gani ila wajuzi wa jiografia wanadai ni kimondo hicho. Pamoja na hayo amezungumzia masuala ya kusoma kompasi , ila wadau pia wakasema ni kwa kuwa eneo hilo ndipo kwa kipindi hicho ndipo sehemu chache Duniani ambapo True North na Magnetic North zinapita kwa pamoaja. Hapa kwa wanajiografia wanaelewa zaidi.

Kuna mdau mmoja anaitwa Joshua Slocum yeye alijipatia sifa ya kusafiri baharini mwenyewe ingawaje alipotea mwaka 1909 na inasadikiwa alipotelea kwenye pembe tatu ya bemuda wakti akiwa anaelekea marekani ya kusini kutokea Martha Vineyard.Ingawaje bado kulikua na utata kwamba alipotelea sehemu gani hasa lakini inasadikiwa alipotelea maeneo ya pembe hii yenye maajabu mengi kwenye ulimwengui huu.

William Shakespeare mwanamashairi na plays nguli na mahiri kwenye ulimwengu huu aliwahi kuongelea kwenye play yake “The Tempest,” ambapo wanazuoni wa masuala ya play wanasema alikua akizunguimzia eneo hilo la bemuda na kupotea kwa meli katika eneo hilo. Ingawaje haya yote hayakuteka jamii ya watu mpaka kwenye karne ya 20 ndipo jamii ilianza kuwa na wasiwasi na eneo hili. Hii inapata uzito zaidi pale ndege meli ya marekani ya Navy ilipopotea ikiwa na USS Cyclop ikiwa na ukubwa wa 542 mita urefu na ilikua ya mizigo ikiwa na wanajeshi wa maji 300 na tani elfu kumi za manganese ilipozama maeneo ya karibu na Barbados and the Chesapeake Bay. Meli hiyo haikutuma mawasiliano yoyote pamaja pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya hivyo hamna mtu a najuaye ni nini kilichotokea kwenye meli na meli hiyo mpaka leo ni Mungu na bahari tu ndio wanaelewa kilichotokea. Baadae aliyekuwa Rais wa Marekani Woodrow Wilson wakati huo alikuja kudhibitisha kwamba meli mbili ndogo zilizoambatana na meli hiyo kubwa na zenyewe zilikuja kupotea maeneo hayo hayo mwaka 1941.

mfululizo wa kupotea baadhi ya vyombo na vingine kukutwa vimetelekezwa ndio hasa unaowatisha watu kuhusu eneo hilo . Mwaka 1945 five ne navy bombers zilizokua zimebeba watu 14 zikitokea Fort Lauderdale. Hizi zilikuwa zimepelekwa huko kwa ajili ya mazoezi na wanajeshi ila cha kushangaza zilikutwa zimetelekezwa. Inasadikiwa kwamba Compas ya kiongozi wa msafara huo ilishindwa kufanya kazi na wenyewe kujikuta wamepotea baada ya kuzunguka na kuishiwa mafuta na hata hivyo ndege iliyotumwa kwa ajili ya uokozi na yenyewe ilipotea ikiwa na watu 13 ndani. waliwatafuta bila mafaniio na mwishoni wakahitimisha kwamba ilipotea kana kwamba immeelekea sayari ya Mars.
 
Hii bermuda triangle nakumbuka aliishaiongelea Mshana jr kwenye moja ya nyuzi
 
kwann wasitume drone camera's tujee kuna nn vipi hawataki watu wa kujitolea kwenda kufanya utafiti maana mie kila nikickiaga kuhusu ili eneo napata shauku kufika

G.O.M.D
 
Hii bermuda triangle nakumbuka aliishaiongelea Mshana jr kwenye moja ya nyuzi
Yap kuna sehemu aliizungumzia kidogo sana kwa kutumia picha ila hapa tumeipa nyama zaidi .Kama itakua umeielewa kuna tofauti ndio maana hawajaiunga na ya mshana jr .

"Never stop learning because life never stop teaching"
 
  • Thanks
Reactions: bbc
Back
Top Bottom