Hii ndiyo sababu ya pengo la maendeleo kati ya Wakristo na Waislamu kwetu Watanzania wa asili

Hii ndiyo sababu ya pengo la maendeleo kati ya Wakristo na Waislamu kwetu Watanzania wa asili

Kwa muktadha wa post hii wahusika ni Watanzania wa asili pekee, bila kuhusisha Watanzania wenye asili ya kuhamia kutoka nchi nyingine (waarabu, wahindi, wachina, wasomali, n.k)

Unapo observe demographics za watanzania wa asili ni rahisi sana kugundua kuna gap kubwa la kiuchumi kati ya waislam na wakristo,

Haimaanishi kwamba hakuna waislam watanzania wa asili wenye maendeleo, walioelimika, n.k. wapo lakini ni kwa uwakilishi mdogo sana

Sababu ni hizi zifuatazo.

1. Waislamu wanapenda kusaidia (Charity), wakristo hupenda kuwezesha (Empowernment)

Waislamu wengi hupenda kusaidia kwa mfumo wa kutoa misaada, mfano muislam akiona mtu ana shida atampa hela au chakula au malazi, kwake ndio jambo kubwa zaidi, lakini misaada hii hufanya wengi kuwa tegemezi. Wakristo kwa upande mwingine, mara nyingi wanahamasisha maendeleo ya muda mrefu kwa kugawa ujuzi wa kazi, mikopo ya kuanzisha biashara na fursa za elimu. Hii ina maana kwamba wakristo huwekeza katika uwezo wa watu kujiwezesha kimaisha, hali inayoweza kuunda tofauti kubwa za kiuchumi kwa muda.

2. Wakristo wengi huamini kutafuta ni bidii na ulinzi wa Mungu huku waislam wengi huamini kama sio ridhiki basi kiache

Wakristo wengi huamini katika mchanganyiko wa jitihada binafsi sambamba na kusali, Waislam wengi hupendelea mtazamo wa kuona kitu kitachokushinda sio ridhki, wakiamini kwamba matokeo makuu yatatokea kwa mujibu wa fungu ulilopangiwa. Tofauti hii katika mtazamo inaweza kuathiri jinsi watu wanavyochukua hatua za kiuchumi na uwekezaji wa muda mrefu.

3. Wakristo wameshikilia biashara nyingi

Ukichanganya na maelezo ya point ya juu, matokeo yake tunayaona biashara nyingi za watanania wa asili zinaendeshwa na wakristo. Nenda kwenye masoko ukianzia na Kariakoo, fuailia kampuni za mabasi ya mikoani, nenda kwenye migodi ya madini, kampuni za utalii, wamiliki wa shule private, n.k. ukifuatilia ratio utaona wakristo wametawala zaidi kwenye hizi biashara.

Ukija kwa upande wa waislam sekta za utafutaji wanako tawala zaidi ni kwenye michezo na burudani, huku bila shaka wakristo wamepitwa sana kuanzia Muziki, filamu, mpira, n.k. shida ya sekta hii umaarufu upo ila pesa yake ni ya taabu, kuna wajaja wengi sana hufaidika kuzidi wenye vipaji.

4. Wakristo wengi wamewekeza na kuipa kipaumbele elimu

Fuatilia utaona kwamba karibia nusu ya shule zinazoongoza kitaifa huwa ni za taasisi za kikristo, Kuna vyuo vingi vya kikristo vinavyotoa watu wenye ujuzi na taaluma za kuwapa sifa za kujiajijiri au kuajiriwa kwenye taasisi za serikali. ukija katika level za familia, wakristo wana umakini mkubwa wa kufuatilia maendeleo ya watoto kielimu na kuwakumbusha mara nyingi watie juhudi kwenye masomo.

Ukija kwa upande wa waislam hata vyuo vimekuwa changamoto kuvijenga, na hata kilichopo pale Morogoro baadhi hukikimbia kwa skendo zilizopo ikiwemo video iliyowahi kusambaa ikionyesha wanafunzi wakichapwa viboko

5. Watoto wenye wazazi wakristo wana uhakika wa malezi kuzidi waislam

Tunda la ndoa ni watoto, ndio wanaotakiwa kupewa attention zaidi. Utofauti mkubwa wa wakristo na waislam kwenye ndoa, Ndoa za kikristo zimewapendelea sana watoto kwa kuwabana wazazi wawap attention kubwa, hata wazazi wanapotaka kuachana makanisa huwa yanaangalia zaidi watoto kuzidi wazazi, na hata ikitokea wameachana wakristo wengi tamaduni zao huwalazimu kuendelea kuhudumia watoto hata kama wazazi wametofautiana. Lakini sasa kwa upande wa waislam sheria za ndoa zimewaangalia zaidi wazazi kuzidi watoto, Mzazi anaweza kuacha na kuoa kadri anavyotaka, wazazi wakikosana talaka ni kitendo cha kuchukua kalamu tu, madhara huathiri watoto zaidi kwenye malezi na matunzo yao.

Kitu kingine wakristo wengi huoa wakiwa wamejiandaa kwajili ya ndoa mfano kuwa na kipato, makazi, n.k. lakini waislam ni kawaida kuoa kwasababu tu kimefika kipindi cha Ramadhani bila kujali uwezo wa kuhudumia familia au kuwa bado anaishi kwao au kwa ndugu yake
Akili za masikini bhana!!!?
 
Universtiy of Arusha

Leta chuo au hospitali ilijengwa na nyinyi wakristo wabantu weusi ambao mpaka leo mnaoomba kujengewa vyoo na wazungu pamoja na kuwa na utawala wenye zaidi ya miaka 40 kati yenu ya uongozi wa nchi wa wakristo kuanzia nyerere miaka 25, mkapa miaka kumi na magu miaka 5.
Mmeongoza hii kwa zaidi ya nusu ya tokea tupate uhuru, lakini nchi bado maskini
Halafu nyinyi vilaza mnakuja kujitamba humu mna maendeleo


Unajua na hiki pia ilijengwa nani?
1780849872451.png
 
Leta chuo au hospitali ilijengwa na nyinyi wakristo wabantu weusi ambao mpaka leo mnaoomba kujengewa vyoo na wazungu pamoja na kuwa na utawala wenye zaidi ya miaka 40 kati yenu ya uongozi wa nchi wa wakristo kuanzia nyerere miaka 25, mkapa miaka kumi na magu miaka 5.
Mmeongoza hii kwa zaidi ya nusu ya tokea tupate uhuru, lakini nchi bado maskini
Halafu nyinyi vilaza mnakuja kujitamba humu mna maendeleo


Unajua na hiki pia ilijengwa nani?
View attachment 3603106
Kwako tatizo lipo wapi taasisi ya kikristo ya nje ikijenga chuo au hospitali Tanzania ? Ni sawa na nchi za kiarabu zikitoa misaada wala hakunaga shida, huwa kuna misaada wanatoa mfano makontena ya tende, watu wanafuturu wanashiba, maisha yanaendelea.

Angalia mradi una faida gani usiangalie ulijengwa na nani, mfano vyuo vya afya vinatoa madaktari ambao huzalisha hata wanawake wa kiislamu, hata wewe mwenyewe kuna uwezekano mkubwa tu mama yako alihudumiwa na mkunga mkristo, sasa kwa akili yako ilivyo unaweza kuchukia ukigundua hayo badala ya kushukuru ulizaliwa salama.

Ni vyuo hivyo vinavyotoa madaktari, wahasibu, wanasheria, ma engineer, walimu, maafisa ugavi, n.k. waliojaa kwenye taasisi za serikali, jeshi, makampuni, n.k. wengine wametumia maarifa hayo kufungua biashara zao
 
Kwako tatizo lipo wapi taasisi ya kikristo ya nje ikijenga chuo au hospitali Tanzania ?
Hapa inatosha kuhitimisha mada kuwa unapotaja waislamu wa Tanzania hawana maendeleo, basi sema waislamu wote na ulete ushahidi sio unarukaruka
Zikiwa zinaendeshwa au zimejengwa na wazungu wakristo unajimilikisha ni za wakristo lakini zikijengwa na waislamu wahindi au waarabu hizo sio za waislamu.

Maana na sisi tusema tuna Agha Khan Univesity ni waislamu, na kweli hata mahafali mnavalisha majoho ya kiislamu.
Pia tuna shule zinazoongoza kama Almuntazir mimi mbantu nimesoma hapo, na dada zangu pia wamesoma hapo na nyingi tu siku hizi.
Na pia hospitali zote kubwa na mpya sasa nchini ni kwa njia moja au nyingine zinaendeshwa na waislamu.
Siafee Hospital
Shifaa Hospital
Aga Khan
Ebrahim Haji Hospital

​

 
Hapa inatosha kuhitimisha mada kuwa unapotaja waislamu wa Tanzania hawana maendeleo, basi sema waislamu wote na ulete ushahidi sio unarukaruka
Zikiwa zinaendeshwa au zimejengwa na wazungu wakristo unajimilikisha ni za wakristo lakini zikijengwa na waislamu wahindi au waarabu hizo sio za waislamu.

Maana na sisi tusema tuna Agha Khan Univesity ni waislamu, na kweli hata mahafali mnavalisha majoho ya kiislamu.
Pia tuna shule zinazoongoza kama Almuntazir mimi mbantu nimesoma hapo, na dada zangu pia wamesoma hapo na nyingi tu siku hizi.
Na pia hospitali zote kubwa na mpya sasa nchini ni kwa njia moja au nyingine zinaendeshwa na waislamu.
Siafee Hospital
Shifaa Hospital
Aga Khan
Ebrahim Haji Hospital

​

Zinaweza kujengwa kwa misaada ya nje lakini zikishajengwa wanaoziendesha na kunufaika ni watanzania wa asili.

Taasisi kama Agha Khan hao ni chuo hospitali private, hao kina Agha Khan ni biashara ya familia, ni mabilionea

Pia fuatilia vyuo kama CuoM kimejengwa na taasisi za kikristo za hapa hapa

Watoto wako wanakaribishwa kusoma, hakuna ubaguzi, kuna wanafunzi wa dini zote na ada ni nafuu.

N:B: Hakuna viboko

1780852893594.png
 
Back
Top Bottom