Hii ndiyo Simba itakayo muua Casablanca Jumamosi

Hii ndiyo Simba itakayo muua Casablanca Jumamosi

Kweni wachezaji waloifunga Al ahly ndo Hawa waliopo sasa?


Muulize na muda wa mechi pia

AL AHLY ulikuwa anacheza nae kwenye jua la saa 10 .

Dar jua la saa 10 ni kali sana kwa mtu mgeni ambaye hajazoea kucheza juani.

Hata wewe ukiambiwa ukimbie mazoezi saa 10 jioni.. hutaweza kukimbia umbali mrefu sababu ya jua

Raja casablanca mechi ni saa moja usiku.

Aache kufananisha na wale aliowafunga kwenye jua kali
 
Amani ya bwana iwe nanyi wana wa MUNGU.

Kuelekea mechi dume jumamosi, mechi ambayo kila mtanzania anaisubiri kwa hamu, mechi ambayo kila mwafrika mpenda soka anaamini raja casablanca anenda kupata mateso makali kwa mkapa jumamosi, mechi ambayo hata watani wanaamini mwarabu ameyakanyaga

Basi napenda jumamosi akutane na ile simba ilomfanya kocha wa kaizer chief aone muda unaenda kwa speed ya kinyonga, simba ambayo inakushambulia muda wote, simba ambayo mo husein akikamata bali anakuja kwa nguvu, ile ambayo kapombe akipewa kabumbu anakufata mpaka ukome, simba ambayo chama akipewa gozi, wanasimba wote wanapata raha duniani na utukufu mbinguni, simba ile miquisone{sakho} akipewa kandanda unatoa jicho kuona wangapi watafungashwa tela, ambayo ilimpiga vita club manne pamoja na kamati pendwa ile ya mapokezi

Naitamani morali ile ya wachezaji kushambulia muda wote kama ile vita club anakufa 2-1 kwa mkapa, hakika itapendeza na hawa waarabu watatuambia kama ni waafrika ama waamerika, mwanakulitaka...?
Ambulance ziwepo kwa wingi.
 
Nakwambia mkuu kwa yale mambo yetu ya kiswahili yanayopelekea uwanja kulindwa na makomandoo, mwarabu j mosi atapata kilichompata al ahly mwaka juzi.
Hakuna cha uswahili kama boli halipo halipo tu, huwezi fananisha Simba ya Al ahly na Simba hii, tujiandae tu kisaikolojia.
 
Kana walifungwa na vibonde Galaxy iweje Raja wawaache??
 
Simba kwa Casablanca itakua ni janga[emoji1][emoji1][emoji1] simba ile iliyompiga Alahly sio hiii aiseh [emoji119]
 
Mkuu unaelewa Morocco ni namba 11 katika FIFA Men's Football Rankings sasa hivi?

Na Egypt ni 39.

Na Tanzania ni 130.

Haya mambo huwa yanabadilika sana hao waarabu wenu wakifungwa, ghafla mnaanza kuwaita ni wakawaida na kwamba hawana viwango vikubwa kwakua Simba sc imewashinda

Leo hii team zote za kimataifa ambazo zimefungwa na Simba Sc hapo kwa mkapa umazioma dhaifu, leo hii Ahly unawaona dhaifu hao raja mara ya mwisho kuchukua kombe mbele ya Al Ahly ni lini??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweni wachezaji waloifunga Al ahly ndo Hawa waliopo sasa?
Wakati Ahly inafungwa, kabla ya mechi mlitarajia itafungwa?

Kauli zenu zilikuwa ni kama hizihizi mwisho wa siku mkawaita vibonde (kisa wamefungwa na Simba sc) kisha wakawaaibisha kwa kubeba kombe lenyewe, hao Raja wakifungwa na Simba Sc mtakuja hapa kuwaita vibonde.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mlikuwa mnawachezesha juani.

Jua la saa 10 dar ni kali sana kwa mtu mgeni

Raja casablanca mechi usiku kwenye hali ya hewa nzuri..

Hata wewe ukiambiwa ukimbie kutroti saa 10 utachoka haraka kwa jua.. ila ukiambiwa ukimbie mazoezi saa 1 usiku hautachoka haraka hata kama sio mtu wa mazoezi
Msije kuwaita vibonde baada ya mechi, tunawatunzia risiti zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo huwa yanabadilika sana hao waarabu wenu wakifungwa, ghafla mnaanza kuwaita ni wakawaida na kwamba hawana viwango vikubwa kwakua Simba sc imewashinda

Leo hii team zote za kimataifa ambazo zimefungwa na Simba Sc hapo kwa mkapa umazioma dhaifu, leo hii Ahly unawaona dhaifu hao raja mara ya mwisho kuchukua kombe mbele ya Al Ahly ni lini??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa vidimbwi wao kazi ni zomea zomea tu, mwaka juzi tulipopangiwa kundi moja na al ahly, as vita na el mereck walisema simba ni under dog, na kwamba ingemaliza wa mwisho! Maajabu ya simba ikamalizo on the top, jamaa wakabadili maneno eti al ahly imechoka na vita club imeondokewa na wachezaji wengi, chakushangaza al ahly aliechoka akachukua ubingwa kwa kumpiga kaize chief ambae nae alinusurika pale kwa mkapa,
ila leo vyura wamesahau wanasema simba hii imechoka, ila kesho wataumbuka tena.
 
Nataka tuu niwakumbushe wale wenye roho za kichawi...hata tukipigwa ila hii rekodi haitakaa ifikiwe na yoyote
REKODI YA MNYAMA KWA MKAPA
Screenshot_20230217-144600_Chrome.jpg
Screenshot_20230217-144617_Chrome.jpg
Screenshot_20230217-144608_Chrome.jpg
 
Wale mlikuwa mnawachezesha juani.

Jua la saa 10 dar ni kali sana kwa mtu mgeni

Raja casablanca mechi usiku kwenye hali ya hewa nzuri..

Hata wewe ukiambiwa ukimbie kutroti saa 10 utachoka haraka kwa jua.. ila ukiambiwa ukimbie mazoezi saa 1 usiku hautachoka haraka hata kama sio mtu wa mazoezi
simba alicheza mechi saa 10, alicheza mechi saa 1, alicheza mechi saa 4 na zote alishinda sasa unapata wapi nguvu ya kuzungumzia muda kama kikwazo cha ushindi?
 
Back
Top Bottom