Hii ndiyo siri GSM kujiondoa katika udhamini ligi kuu, Simba inahusika

Hii ndiyo siri GSM kujiondoa katika udhamini ligi kuu, Simba inahusika

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kampuni ya GSM imetangaza kujiondoa katika udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hiyo siyo habari mpya kwa sasa, lakini kilichopo nyuma ya pazia na sababu kubwa ni wapinzani wao wa jadi Simba kugoma kuunga mkono juu ya udhamini huo.

Mara baada ya TFF kutangaza udhamini huo, kisha ikaelezwa kuwa klabu zote shiriki katika ligi hiyo kutakiwa kuvaa jezi zenye nembo ya GSM, Simba wao waliibuka na hoja kadhaa kisha wakagoma kutii maelekezo hayo ya TFF na Bodi ya Ligi.

Moja kati ya hoja za Simba ilikuwa ni kutoshirikishwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, GSM kuwa ni mdhamini wa Yanga wakati huohuo kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu na nyingine kadhaa.

Barbara ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba ndiye ambaye alilishikilia bango suala hilo kwa niaba ya klabu na kuiandikia barua TFF, pia klabu yake haikushiriki katika kuvaa jezi zenye nembo ya GSM.

Licha ya kuwa GSM hawajasema wazi kuhusu masharti ya mkataba ambayo wanaona yamekiukwa katika makubalano yao lakini ni wazi kuwa Simba ndiyo sababu hasa ya wao kuamua kujiondoa.

Chanzo kutoka GSM kimeeleza kuwa kitendo cha Simba kugomea kuvaa jezi zenye ‘brand’ ya GSM kisha TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kuwachukulia hatua, huku kesi ya udhamini wao ikipelekwa FCC ndiyo sababu ya kuamua kujiondoa.

Kesi hiyo ilifikishwa FCC kwa kuwa serikali iliamua kuingilia kuona kama mchakato wa fair competition ulikuwa katika njia sahihi.
 
Kesi hiyo ilifikishwa FCC kwa kuwa serikali iliamua kuingilia kuona kama mchakato wa fair competition ulikuwa katika njia sahihi.
Sasa kama mchakato ulikubaliwa na FCC, kwa nini ajitoe sasa? Aache longolongo, awape mpunga wao madogo watamtangazia brand yake humuhumu nchini
 
.
20220206_173630.jpg
 
Back
Top Bottom