hii kesi imefikia tamati?
Kwa Tanzania Rushwa ina nguvu kuliko Haki. Mtuhumiwa yuko Huru na anaendelea na Kuuza zake Mihogo Soko la Kawe japo kwa sasa Ameokoka Kinafiki ( anasali Kanisa jirani la kwa Mchungaji Ndegi ) Kawe.
Ni kwamba wakati Kesi inaendelea na Mtuhumiwa yuko Lupango Mke wa Mtuhumiwa ( ambaye aliachwa kwa Kukashifiwa na Kipigo juu na Mumewe Cherehani ) ambaye anasali ( ni Mmoja wa Waumini ) kwa Kanisa la Living Water ( la Mchungaji Ndegi na Mkewe Lilian ) aliamua Kumpambania Mumewe huyo Mpumbavu Cherehani na Kesi yake hiyo kwa kuomba Msaada wa Waumini wa Kanisa hilo la The Living Water Kawe pamoja na wenye Kanisa hilo ili wamsaidie Polisi na kwa Wakubwa ili tu huyu Cherehani asifungwe mazima.
Hivyo kilichotokea ni Wakubwa wa Kanisa hilo la The Living Water na Waumini wake kuamua Kulibeba kama Wao ( kwakuwa tu Mke wa Mpumbavu Cherehani ) anasali Kwao ( Kanisani hapo ) na kutoa Hongo sehemu Kuu / Nyeti Mbili na Cherehani kupona Hukumu Kali iliyokuwa inaenda Kumkabili huku akipewa Masharti ya Yeye sasa kuwa Mkristo ( japo ni Muislamu kindakindaki ) na awe anaimba na Kwaya yao hapo kama anavyoimba huyo Mkewe na pia amrudie huyo Mkewe aliyemuacha kwa Kipigo, Dharau na Kashfa za kila aina huku Cherehani akiendekeza zake Uhuni kwa Wanawake na Kuwaambukiza vile vilivyoshindwa Kutibiwa na WHO tokea Viibuke rasmi mwaka 1981 baada ya Kugundulika huko nchini Uganda.
Baada ya Mpumbavu Cherehani kuvuka Kigingi hicho cha kukwepa Jela baada ya Rushwa kutembea sana ( kwa Nguvu na Ushawishi wa Kanisa la The Living Water Kawe ) akabakiwa na Kigingi kingine cha upande wa Kijana aliyemuumiza vibaya na Kikatili ( kwa kumkata Sikio na Kidole kwa Kisu na Panga huku akimpaka Spirit ) ambapo Ndugu Watata wa Mjeruhiwa ( wakiongozwa na Omary Muuza Mitumba Soko la Kawe na George Muuza Chips Soko la Kawe ) walimtaka Mpumbavu Cherehani awarudishie Viungo Ndugu yao ( yaani Sikio na Kidole ) kama vilivyokuwa huku wakimtaka akawaonyeshe alipovitupa.
Hivyo basi baada ya Mpumbavu Cherehani kuona Hali inakuwa siyo Hali na Ndugu wa Aliyemjeruhi wanakuja Juu akaamua Kuuza Moja ya Nyumba yake iliyoko Mtaa wa Ukwamani kwa kiasi cha Shilingi Milioni 20 ambapo Yeye Mpumbavu Cherehani alichukua Shilingi Milioni 10 na yule Kijana aliyefekwa Sikio na Kidole akalipwa Shilingi Milioni 10 huku na Ndugu hawa Wawili Watata tajwa nao wakapewa Hela yao Kidogo na Kulimaliza rasmi kwa Style hii na kuamini kuwa Tanzania Rushwa, Uonevu na Upendeleo vina Nguvu kuliko hata Haki na Sheria.
Kwa sasa Mpumbavu Cherehani karejea Kukaa na Mkewe aliyempigania ( japo alimuacha kwa Kipigo, Dharau na Kashfa ) huko Mji Mpya Kawe huku akiendelea na Biashara yake ya Kuuza Mihogo Soko la Kawe, akisimamia Pikipiki zake ( Bodaboda ) na akimiliki isivyo halali Vizimba ( Fremu ) zilizoko Soko la Kawe na akiwapangisha Watu ( Wafanyabiashara ) kwa Kodi ya Shilingi Elfu Sitini kwa Mwezi badala ya Kodi halali ya Shilingi Elfu Thelathini iliyowekwa.
Na kwanini haguswi ni kutokana na kwamba nae pia ni Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Soko la Kawe ambalo lina Madudu mengi ila linalindwa kwakuwa aliyewahi kuwa Meya wa Kinondoni Mzee Salum Londa nae ana Vizimba vyake kadhaa hapo na ana Maslahi makubwa na Soko hilo ( hasa Kiuchumi ) kwakuwa lilianzishwa alipokuwa Meya wa Kinondoni hivyo Mipango yote ya ilipokuwa, ilipo na iendako Mzee Londa anaijua na kuhusika nayo kwa 10% zitokanazo na zitakazotokana na Soko hilo la Kawe.
Nadhani huu ufafanuzi utauelewa na nakuomba Uamini kwa 100% kwani ni Tukio lililotokea huku Binafsi nikiwa karibu na Wahusika wote ( wa pande zote ) hivyo napata Taarifa sahihi na za uhakika kutoka Kwao Wenyewe ambapo kupenda Kuropoka hovyo kwa Ushamba, Sifa na Upuuzi wao ni Jambo la Kawaida mno ambalo ni Faida kwa wengine ( kama Mimi Cognizant ) mpenda kujua kila Kitu au Jambo.
Kila la Kheri Kiongozi.