Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Ajali ya kisiasa ni tukio ambalo linamtokea mtu kwa yeye mwenyewe kulitengeneza au kutengenezewa, na ambalo linamuondoa moja kwa moja kwenye ulingo na ramani ya kisiasa.
Zitto Kabwe ni mfano hai wa mwanasiasa Tanzania aliyepigwa na ajali ya kisiasa ambayo imempoteza kabisa kwenye ramani ya kisiasa angali bado yupo kwenye prime age ya kufanya siasa za ushindani kwa kiwango cha juu kabisa.
Baada ya kutamatika uchaguzi Chadema, kuna watu ajali za kisiasa zitakuwa zimewafikia. Kwangu ni Boni Yai, Yericko na Ntobi na wapuuzi wengine
Hawa watu walijiona ni miungu watu kwenye kipindi cha kampeni na hata wengine kufikia kujiita 'Machinery ya Chama' na maneno makali sana na dhihaka.
Natumai Lissu sio mtu wa visasi, ila kwa uchaguzi huu, atakuwa ameweza kusoma vyema uwezo wa kufikiri na kujenga hoja kwa aina ya wanachama dizaini ya Yericko na Ntobi, wamejipotezea heshima na kuaminika mbele ya wanachama wa kawaida na viongozi wengine wa chama.
Ajali ya kisiasa imewapiga rasmi kwa kushindwa kuwa na akiba ya maneno