Hii Ndoa Tarajiwa Inaniumiza kichwa

Hii Ndoa Tarajiwa Inaniumiza kichwa

Oa mtoto wa watu acha hizo. Huyo ni wa kishua kama kwao hana shida...hawezi kuwa na mawazo mengi productive...akikuja kukaa kwako ww sio sio wa kishua so itabidi aanze kujifunza maisha then atakuwa productive na haswa ww ukimcoach vizur. Unless na ww huna wazo productive unamsema tu mwenzio...Unataka very perfect??? Je ww ni very perfect??? Tena huyo kukubali kuishi na ww usiye wa kishua hilo pekee ni wazo productive la huyo binti...usawa huu anakubali kuacha uhondo kwa baba yake aje kukaa kwako ahalaf uone yy hana wazo productive?? Anajua anakuja kuanza kutatafuta na ww..Dah kama unamdrop niunganishie mm nibebe leo leo....
Haahhahaaa Kuna Jamaa alisikia Nina Mpango wa Kumuacha Akamwambia mshikaji kwamba bwana Flan akitaka kumwacha flani Aniambie..Nlicheka sana
 
Kuna mambo umetuficha hapo, kuwa muwazi upate ushauri wenye manufaa
 
Huyu ni aina ya wale wanaopiga mapicha na kuyaweka mtandaoni....?
 
Miaka ya Nyuma kidogo kulikuwa na binti mmoja mrembo pale mtaani kwetu, binti kutoka familia yenye uwezo (ya kishua).

Binti huyu wanaume waliogopa Kutoka Naye na pia hata kumtongoza kutokana na nyodo zake pia hata ukali wa baba yake kwa kuwa binti bado alikuwa anasoma.

Nilikuwa namfaham kwa kitambo kiref ila sikuwaza kuja kudate naye mpaka pale nlipokosana na mpenzi wangu ndipo nikamtongoza na yule binti hakusita kuwa nami kwani nilitumia uBornTown mwingi kiasi kwamba binti akaona she deserves a Man like me!

Binti yule nilimkuta Hajatumika maanake mm ndio mwanaume wake wa kwanza na nilimpa ahadi nyingi pamoja na kumhakikishia kumuoa!

Sasa Miaka imeenda imerud ni zaidi ya miaka sita sasa tangu niwe nae na ule wakati wa yeye kuhitaji kuolewa umefika ila kisaikolojia mimi sipo tayari kabisa.

Kwanini sipo tayari? Hizi Hapa sababu!
1.Binti Huyu ni Mzuri wa sura na umbo sasa nafikiri ukioa mwanamke wa aina hii ni sawa na kulima shamba la miwa karibu na shule ya msingi!
2.Binti Huyu Hajui Hustles, kwanza physicaly anaeza kutembea kilomita moja akawa hoi taabani.
3.Binti Huyu sijawahi Kuona Fikra yake Productive Hata Moja na ujuavyo mwanamke wa Ndoa anatakiwa angalau awe na Fikra Productive!

Mimi Nafikiria kuamua kumpiga chini kwa utashi wa Fikra zangu ila kama una la kunishauri Nishauri tu Huenda ikanisaidia Pakubwa.

Muwe na Usiku Mwema!
Duuh
 
Back
Top Bottom