Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Umechagua njia sahihi kwa wanaojisalimisha mbele ya Mungu na Mungu pekee ndiye wanaemuomba msaada.
Kuliko ungeendelea kuomba viumbe msaada kwa kutaja majina yao au kuomba mizimu kwenye miti mikubwa, au kuwa kerubi wa zumaridi au kuamini na kumuita yule mnyakyusa kuwa ni nabii
Ama kweli watu wengi wamepotea
 
pole Yako... jitafakari upya bado mlango upo wazi unaweza kutubu na kumrudia Kristo ambae ni yote ktk yote...

Ni suala la mda tu utajutia uamuzi wako..uyo Mohamed Hana pa kukupeleka sabb na yy anasubiri kuhukumiwa..Yesu ndio mamb yote...
 
Faida gani napata hadi nitunge uongo nakwambia uhalisia wa Mambo jinsi yalivyo,
Huo ni uongo...hakuna sehemu ambapo watu wanalipuka mapepo kama makanisa ya walokole.

Kama huamini Anza kuhudhuria ibaada zao, Kila J2 lazima Kuna lundo la watu wataanguka mapepo.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una waislam tupu. nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu.
Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.

PS: yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
Jitahidi kuishi kadri ya mausia ya dini
Sio kuswali pekee
 
Karibu katika quran na sunnah.
Uislamu maana yake Kusalimika.

Achana na propaganda za dini hii kuhusishwa na Ugaidi

Hivi unajua kuwa kuoa mke zaid ya mmoja kuna hekma kubwa sana kwa Alie tuumba.

Wacha hiyo, hivi unajua uislamu ndio dini iliyokuna kufundisha watu kujilinda vizuri na najisi( kinyesi na mikojo).

Ntaendelea wacha kwanza nimalizie kazi.
Najisi ni mavi na mkojo, vibavyotoka mwilini kwako? Basi mwili ni najisi!
 
Unafanya dhambi kubwa na kumkosea Muumba wako unapompa Yesu binadamu kama Wewe hadhi ya Mungu.

Yani unamuabudu binadamu mwenzio
Yesu alikuwa Nabii kama manabii wengine, na hakuwahi kusema yeye ni Mungu

Kina Paulo na Waroma ndio waliochakachua na kuanza kumuabudu Kama Mungu.
Shirki mbaya sana.
We hutaenda KWA ustadhi akufanyie dawa ya kishirikina?
 
Dini duniani ni moja tu, uislam
Sawa bado unajaribu

Cc: FaizaFoxy
 



Mcqueenen
 
Back
Top Bottom