Supu na nyama: Hii inaonyesha maisha yako yapo kwenye kipindi cha kujitafutia riziki kwa juhudi (kama ulivyozoea kunywa supu kazini), lakini sasa unapitia changamoto au vikwazo unavyovikataa (nyama huuitaki lakini inaambatana na supu yako). Inaashiria pia kuwa kuna mambo unayoyataka kwenye maisha yako ila yanakuja na mzigo au vikwazo usivyotamani.Inaanzia nikiwa eneo ninalifahamu nikaenda kunywa supu anaye pika supu namfahamu ni kweli anauzaga supu na huwa nakunywa mara kadhaa asubuhi nikiwa kazini.
Sasa nilipofika kwenye sufuria ya supu tulikuwa watu kama 3 hivi wenzangu wakachota na kuanza kunywa ila mm kila nikichota ile supu ilikuwa inakuja na nyama na mm nilikuwa nataka supu tu.
Basi kila nikirudisha nyama nakuta supu imerudi na nyama inabaki kama kijiko cha kulia
Basi nikajaribu mara kadhaa mwisho ikaja supu na nyama choma nikarudisha tena baadae akaja muuzaji akanichotea nikasogea na bakuli peembeni ili nikanywe supu baada ya kukaa nikaona bakuli imejaa mkaa basi nikawa nautoa ule mkaa mpaka mpaka supu ikaisha kwenye bakuli.
Wakati naendelea kushangaa kuangalia upende wa nga`gambo ya barabara nikaona watu ninaowajua ni madereva toyo wanaua nyoka ambaye alikuwa juu ya ukuta akiingia kwenye fremu ya biashara ambayo hiyo fremu naifahamu vizuri tu ni wanauzaga mchele.
Ikanibidi niende nikasaidie nilipofika nikakuta yule nyoka ndo anaishilia kuingia ndani kwa usawa wa lenta ya nyumba.
Basi mm nikawahi kwa ndani nikiwa na mawe mawili mkononi nilipofika mlangoni nikashangaa nyoka mwingine mdogo ananipita miguuni kwa kasi akaingia kwenye shimo lililo kwenye kona.
Kwenye kona pia kulikuwa na kuku kalalia mayai ila kuku alionyesha tu ile ishara ya kunyanyua mbawa na kulia.
Basi nikarusha jiwe la kwanza nikampiga yule nyoka mkubwa kwenye shingo akawa amepoteza mwelekeo.
Nikarusha na la pili nikampiga kichwani akaanguka chini maana alikuwa anakaribia kuingia shimoni nikaona anajikunja kunja ndiyo nkashtuka kutoka usingizini.
Wakati huo hapo ndani kwa hoyo fremu nilikuwa napaona ni kwangu maana niliona vitu vyangu kuanzia kitanda na vingine na hilo tukio lilikuwa ni kama la pili kwenye ndoto kumaanisha huyo nyoka ni kama alishawahi nitoroka mara ya kwanza.
Je? Huyu nyoka mdogo nitamuua lini? Kwa maana akikua si atanidhuru tu.
Nawasilisha kwenu wataalamu
Ila kwa sasa hii nyumba nimepanga ninahama muda wowote maana nimeshalipa kodi kwingine hivo bado nadaiwa hapa kama laki 2 hivi nikilipa tu nahamia zangu kwingine.
Asante kwa jinsi umeweza kunifunulia hujakosea changamoto ninazo na ndo maana hapo mwisho nimeeleza nadaiwa zaidi ya laki 2 na mwenye nyumba nimlipe ndo niondokeSupu na nyama: Hii inaonyesha maisha yako yapo kwenye kipindi cha kujitafutia riziki kwa juhudi (kama ulivyozoea kunywa supu kazini), lakini sasa unapitia changamoto au vikwazo unavyovikataa (nyama huuitaki lakini inaambatana na supu yako). Inaashiria pia kuwa kuna mambo unayoyataka kwenye maisha yako ila yanakuja na mzigo au vikwazo usivyotamani.
Bakuli kujaa mkaa: Mkaa unaashiria majaribu au matatizo yanayoharibu kile unachotarajia kuwa kizuri. Supu inamaanisha rehema au baraka, lakini unapofika unakuta imejaa mkaa – maisha yako kwa sasa yanaonekana yana uzito wa madeni, majukumu au matatizo unayohisi yanakunyima amani.
Nyoka mkubwa: Nyoka mara nyingi kwenye ndoto ni ishara ya watu wabaya, majaribu au roho za usumbufu. Nyoka mkubwa anayeingia nyumbani kwako na kujaribu kuingia shimoni, anawakilisha mtu au hali fulani iliyokuwa inakusumbua kwa muda mrefu, au shida iliyokuwa imejificha nyumbani au maisha yako lakini sasa umepambana nayo na umeishinda (kumpiga kwa mawe).
Nyoka mdogo anayekimbilia shimoni: Hii ni ishara ya changamoto ndogo, watu wanaojifanya marafiki lakini wana madhara baadaye, au shida ndogo ambayo huja kimyakimya na kujificha kwa muda, lakini ikikua inaweza kuwa kubwa zaidi. Kwa sasa hujamalizana nayo – lakini umeiona mapema kabla haijakua hatari. Hii ni tahadhari kwako ya kutoruhusu mambo madogo yaendelee bila suluhisho.
Kuku na mayai: Kuku analinda kizazi au malengo yako, lakini bado kuna hatari inayowazunguka (mayai ni malengo au ndoto zako). Kuku kuonyesha ishara ya tahadhari ni ujumbe kuwa kuna majaribu karibu na matarajio yako ya baadaye.
Kuona nyoka huyo ni kama amerudi mara ya pili: Hii inaonyesha kuwa kuna suala au mtu uliwahi kushughulika naye lakini bado kuna mabaki au athari zake zinajaribu kurudi tena maishani mwako.
Kiuhalisia Ndoto Inamaanisha Nini:Asante kwa jinsi umeweza kunifunulia hujakosea changamoto ninazo na ndo maana hapo mwisho nimeeleza nadaiwa zaidi ya laki 2 na mwenye nyumba nimlipe ndo niondoke
Umefafanua vzr mkuu naunga mkono hoja💪Supu na nyama: Hii inaonyesha maisha yako yapo kwenye kipindi cha kujitafutia riziki kwa juhudi (kama ulivyozoea kunywa supu kazini), lakini sasa unapitia changamoto au vikwazo unavyovikataa (nyama huuitaki lakini inaambatana na supu yako). Inaashiria pia kuwa kuna mambo unayoyataka kwenye maisha yako ila yanakuja na mzigo au vikwazo usivyotamani.
Bakuli kujaa mkaa: Mkaa unaashiria majaribu au matatizo yanayoharibu kile unachotarajia kuwa kizuri. Supu inamaanisha rehema au baraka, lakini unapofika unakuta imejaa mkaa – maisha yako kwa sasa yanaonekana yana uzito wa madeni, majukumu au matatizo unayohisi yanakunyima amani.
Nyoka mkubwa: Nyoka mara nyingi kwenye ndoto ni ishara ya watu wabaya, majaribu au roho za usumbufu. Nyoka mkubwa anayeingia nyumbani kwako na kujaribu kuingia shimoni, anawakilisha mtu au hali fulani iliyokuwa inakusumbua kwa muda mrefu, au shida iliyokuwa imejificha nyumbani au maisha yako lakini sasa umepambana nayo na umeishinda (kumpiga kwa mawe).
Nyoka mdogo anayekimbilia shimoni: Hii ni ishara ya changamoto ndogo, watu wanaojifanya marafiki lakini wana madhara baadaye, au shida ndogo ambayo huja kimyakimya na kujificha kwa muda, lakini ikikua inaweza kuwa kubwa zaidi. Kwa sasa hujamalizana nayo – lakini umeiona mapema kabla haijakua hatari. Hii ni tahadhari kwako ya kutoruhusu mambo madogo yaendelee bila suluhisho.
Kuku na mayai: Kuku analinda kizazi au malengo yako, lakini bado kuna hatari inayowazunguka (mayai ni malengo au ndoto zako). Kuku kuonyesha ishara ya tahadhari ni ujumbe kuwa kuna majaribu karibu na matarajio yako ya baadaye.
Kuona nyoka huyo ni kama amerudi mara ya pili: Hii inaonyesha kuwa kuna suala au mtu uliwahi kushughulika naye lakini bado kuna mabaki au athari zake zinajaribu kurudi tena maishani mwako.
🤣🤣🤣Nyoka yuko pale kukulinda. Huyo hapo ni Lord Shiva.
Mkuu nisaidie hii ya kwangu huwa naota mara kwa mara nipo nakula chakula hii ina maana gani?Ushauri:
Malizia deni lako kwa busara usihame huku umeacha mzigo unaokutesa akili.
Ukihamia huko kwingine, uwe makini na marafiki wapya au watu wa karibu – siyo kila mtu anayetabasamu ni mwema.
Pambana kutatua matatizo madogo kabla hayajageuka matatizo makubwa.
Usikubali hali ya “nyoka mdogo” ikuachie woga – umepewa uwezo wa kuishinda.
Endelea kumuomba Mungu akupe mwongozo kwani ndoto inaonyesha unaona “ishara” mapema kuliko wengine.
mkuu me hii kwangu imekaaje huwa naota mara kwa mara nipo nakula chakula hii itakuwa na maana gani?Nenda kwenu katambikwe acha Ujinga
Huo ni uadui unao sababishwa na mizimu ya kwenu ancestors wako Wana hasira wanaona umekaa muda mrefu bila kuwakumbuka so ndio Wana amua kukuwekea mtima nyongo katika mihangaiko yako ya utafutaji wa rizki ndio maana umeona kwamba hiyo supu uliyoitoa Kila ulipo kuwa Unataka kuinywa inashindikana inajitokeza changamoto Fulani soup tafsiri yake ni rizk au kipato
Na baada ya kuwa Kila unapo jaribu Kunywa hiyo supu inashindikana mizimu ya kwenu imeamua kuonyesha kwamba Kuna uadui upo ktk maisha yako ndio unao changia ushindwe Kunywa hiyo soup( ambayo Kwa tafsiri fasaha ni rizki) Yaani Ina maana kwamba Kuna uadui wa vifungo ktk nyota yako Nyoka uliye muota ni uadui unaopelekea kusababisha rizki yako kuwa ngumu na maisha yako kuwa yenye misuko- suko
Hiyo ndoto imekuja tena kuku dhihirishia mambo makubwa ya mikosi unayo yapitia Yana sababishwa na kwako wewe mwenyewe originality yako Chimbuko lako
kuota nyoka kaingia ndani kwako tafsiri yake ni kwamba huo uadui unatokea ktk chimbuko lako la kiasili hapa na maanisha nyumbani kwenu Kwa mababu na mabibi zako wanapo tokea ,
Hivyo basi ili huo uadui uweze kuisha inatakiwa urudi kwenu ukatambike ancestors wenu
Tatizo Miafrica /Mitanzania ni mijinga imekumbatia Mila na Tamaduni za ukristo na uislam na kuacha Asili /Tamaduni zenu Mwisho wa siku matokeo yake ndio kama hayo
Unakuta Kuna vijana wengi wamsoma na Wana potential + exposure but Kila wanachofanya hawafanikiwi Unakuta mtu ana jitambua lakini hata kazi Hana Kila afanyacho kina kwenda mrama na Bado mtu huyo ana Sali kanisani au misikitini ana muomba mungu wa kutungwa wa wa-Arabu na waisrael amsaidie lakini wapi hatoboi mpaka anadata !! So unadhani shida hapo itakuwa ni nini !?
Jibu ni Moja tu huyo mtu anapaswa kurudi kwao na kuwazuru /kuwatembelea ancestors wake atambikiwe then atakaa Sawa, Eti Unakuta waarabu na wazungu kupitia dini zao Wana wakataza kwenda kuwazuru mababu na mabibi zenu makaburi lakini wao huko makka Madina na Israel Huwa wanakwenda kuyazuru makaburi ya kina Paulo /Muhammad So hapo tofauti ni ipi hao kina Muhammad sindio ancestors wao why iwe haramu kwenu kwenda kuzuru makaburi ya mababu na bibi zenu halafu iwe haramu Kwa wao kuzuru makaburi ya mababu zao na mabibi zao kina Paulo kina Muhammad kina Bi-Aisha sijui na Bi- Khadija ,
Yaani mmekuwa brain wash mpaka mmekuwa mazuzu 🤣🤣🤣🤣😁
Waafrica acheni Ujinga nature the way ilivyo tu- create inamtaka Kila mtu afuate kanuni zake za Asili haiwezekani wewe uwe mbongo halafu kanuni zako za Asili zifanane na wachina / waarabu/ wazungu huko ni kujiongopea na kutojitambua ,
Kama namna ambavyo mazingira yetu haya fanani kitamaduni kijographia na kimila ndivyo ambayo pia hatufanani ktk mitetemo yetu ya ndani ya asili ,
Elimikeni