Hii ndoto ni ya ajabu mno naombeni maana yake

Hii ndoto ni ya ajabu mno naombeni maana yake

Kama kila ndoto ni reality bhasi naelekea kuwa Superhero kama SuperMan au The Flash kulingana n matukio ninayoyaota.
 
Sehemu ya kwanza ni kuhusu mafanikio yako;sehemu ya pili ni kuhusu Maadui zako,wawili utafanikiwa kumdhibiti mmja na mwingine atajificha nyumbani kwake.
 
mkuu me hii kwangu imekaaje huwa naota mara kwa mara nipo nakula chakula hii itakuwa na maana gani?
Kula chakula Mzee Tafsiri yake katika ulimwengu wa kiroho unabashiriwa kupata mafanikio Duniani haswaa mafanikio ya kipato chako kukua na kuongezeka

Hapo inatakiwa uwe makini usitoke nje ya mstari katka Yale mazuri unayo yafanya Huku Duniani ili hizo ndoto zisije kukata ,

Watu wengi Huwa Wana wadanganya watu kuwa kuota unakula chakula eti ni kulishwa chakula na wachawi nakataa Big no

Kula chakula ni ndoto Moja nzuri sana chakula ni baraka so when it comes ukaota unakula chakula tafsiri yake maisha yako yataangazwa na baraka + mafanikio ya kiuchumi Hela hazito kupiga chenga ,

Binafsi Mimi hiyi ndoto ya Kula chakula ni njozi ambayo Huwa naiota pia so niliota nakula chakula au napewa chakula iwe kimeshaiva au Bado kibichi Huwa haipiti siku tatu lazima nipate pesa ,

Na inapotokea nikaenda against na nature Huwa naota Nina nyimwa chakula Nikiotaga hivyo kuwa Nina nyimwa chakula Huwa Nina changanyikiwa cause I know after that nitapitiq msoto ,
 
Kama kila ndoto ni reality bhasi naelekea kuwa Superhero kama SuperMan au The Flash kulingana n matukio ninayoyaota.
Sio Kila ndoto ni real ila Kuna baadhi ya ndoto ni real haswaa Kwa wale watu ambao wako oppossessed with spirit
 
Kula chakula Mzee Tafsiri yake katika ulimwengu wa kiroho unabashiriwa kupata mafanikio Duniani haswaa mafanikio ya kipato chako kukua na kuongezeka

Hapo inatakiwa uwe makini usitoke nje ya mstari katka Yale mazuri unayo yafanya Huku Duniani ili hizo ndoto zisije kukata ,

Watu wengi Huwa Wana wadanganya watu kuwa kuota unakula chakula eti ni kulishwa chakula na wachawi nakataa Big no

Kula chakula ni ndoto Moja nzuri sana chakula ni baraka so when it comes ukaota unakula chakula tafsiri yake maisha yako yataangazwa na baraka + mafanikio ya kiuchumi Hela hazito kupiga chenga ,

Binafsi Mimi hiyi ndoto ya Kula chakula ni njozi ambayo Huwa naiota pia so niliota nakula chakula au napewa chakula iwe kimeshaiva au Bado kibichi Huwa haipiti siku tatu lazima nipate pesa ,

Na inapotokea nikaenda against na nature Huwa naota Nina nyimwa chakula Nikiotaga hivyo kuwa Nina nyimwa chakula Huwa Nina changanyikiwa cause I know after that nitapitiq msoto ,
hii ndoto ya kula chakula huwa naichukia sana huwa nahisi ni kama kuna mtu ana deal na mimi traditionally😅
 
Supu na nyama: Hii inaonyesha maisha yako yapo kwenye kipindi cha kujitafutia riziki kwa juhudi (kama ulivyozoea kunywa supu kazini), lakini sasa unapitia changamoto au vikwazo unavyovikataa (nyama huuitaki lakini inaambatana na supu yako). Inaashiria pia kuwa kuna mambo unayoyataka kwenye maisha yako ila yanakuja na mzigo au vikwazo usivyotamani.

Bakuli kujaa mkaa: Mkaa unaashiria majaribu au matatizo yanayoharibu kile unachotarajia kuwa kizuri. Supu inamaanisha rehema au baraka, lakini unapofika unakuta imejaa mkaa – maisha yako kwa sasa yanaonekana yana uzito wa madeni, majukumu au matatizo unayohisi yanakunyima amani.

Nyoka mkubwa: Nyoka mara nyingi kwenye ndoto ni ishara ya watu wabaya, majaribu au roho za usumbufu. Nyoka mkubwa anayeingia nyumbani kwako na kujaribu kuingia shimoni, anawakilisha mtu au hali fulani iliyokuwa inakusumbua kwa muda mrefu, au shida iliyokuwa imejificha nyumbani au maisha yako lakini sasa umepambana nayo na umeishinda (kumpiga kwa mawe).

Nyoka mdogo anayekimbilia shimoni: Hii ni ishara ya changamoto ndogo, watu wanaojifanya marafiki lakini wana madhara baadaye, au shida ndogo ambayo huja kimyakimya na kujificha kwa muda, lakini ikikua inaweza kuwa kubwa zaidi. Kwa sasa hujamalizana nayo – lakini umeiona mapema kabla haijakua hatari. Hii ni tahadhari kwako ya kutoruhusu mambo madogo yaendelee bila suluhisho.

Kuku na mayai: Kuku analinda kizazi au malengo yako, lakini bado kuna hatari inayowazunguka (mayai ni malengo au ndoto zako). Kuku kuonyesha ishara ya tahadhari ni ujumbe kuwa kuna majaribu karibu na matarajio yako ya baadaye.

Kuona nyoka huyo ni kama amerudi mara ya pili: Hii inaonyesha kuwa kuna suala au mtu uliwahi kushughulika naye lakini bado kuna mabaki au athari zake zinajaribu kurudi tena maishani mwako.
Ndugu umetafsiri hii ndoto vizuri sana, natamani nikutafute unitafsirie mindoto yangu miingi hata huwa siielewi
 
Sio Kila ndoto ni real ila Kuna baadhi ya ndoto ni real haswaa Kwa wale watu ambao wako oppossessed with spirit
Ikiwa zote ni ndoto wawezaje kutofautisha ndoto real na fake?
 
Ikiwa zote ni ndoto wawezaje kutofautisha ndoto real na fake?
Kwa mtu kama Mimi najua how to keep them different,
Inatakiwa ufahamu kutambua ndoto na kuzibashiri ni talent
 
sana sana ugali
Kama ugali kwenye ndoto unaonekana ni wa shida, au unaota kila siku ni ugali tu bila mabadiliko, inaweza kuwa dalili ya kukosa maendeleo au maisha yako kuwa kwenye mzunguko uleule.

Kama ni ugali wa furaha na umeshiba, ni baraka ya kuendelea kuishi kwa amani hata katika hali ya kawaida.
 
Inaanzia nikiwa eneo ninalifahamu nikaenda kunywa supu anaye pika supu namfahamu ni kweli anauzaga supu na huwa nakunywa mara kadhaa asubuhi nikiwa kazini.

Sasa nilipofika kwenye sufuria ya supu tulikuwa watu kama 3 hivi wenzangu wakachota na kuanza kunywa ila mm kila nikichota ile supu ilikuwa inakuja na nyama na mm nilikuwa nataka supu tu.

Basi kila nikirudisha nyama nakuta supu imerudi na nyama inabaki kama kijiko cha kulia

Basi nikajaribu mara kadhaa mwisho ikaja supu na nyama choma nikarudisha tena baadae akaja muuzaji akanichotea nikasogea na bakuli peembeni ili nikanywe supu baada ya kukaa nikaona bakuli imejaa mkaa basi nikawa nautoa ule mkaa mpaka mpaka supu ikaisha kwenye bakuli.

Wakati naendelea kushangaa kuangalia upende wa nga`gambo ya barabara nikaona watu ninaowajua ni madereva toyo wanaua nyoka ambaye alikuwa juu ya ukuta akiingia kwenye fremu ya biashara ambayo hiyo fremu naifahamu vizuri tu ni wanauzaga mchele.

Ikanibidi niende nikasaidie nilipofika nikakuta yule nyoka ndo anaishilia kuingia ndani kwa usawa wa lenta ya nyumba.

Basi mm nikawahi kwa ndani nikiwa na mawe mawili mkononi nilipofika mlangoni nikashangaa nyoka mwingine mdogo ananipita miguuni kwa kasi akaingia kwenye shimo lililo kwenye kona.

Kwenye kona pia kulikuwa na kuku kalalia mayai ila kuku alionyesha tu ile ishara ya kunyanyua mbawa na kulia.

Basi nikarusha jiwe la kwanza nikampiga yule nyoka mkubwa kwenye shingo akawa amepoteza mwelekeo.

Nikarusha na la pili nikampiga kichwani akaanguka chini maana alikuwa anakaribia kuingia shimoni nikaona anajikunja kunja ndiyo nkashtuka kutoka usingizini.

Wakati huo hapo ndani kwa hoyo fremu nilikuwa napaona ni kwangu maana niliona vitu vyangu kuanzia kitanda na vingine na hilo tukio lilikuwa ni kama la pili kwenye ndoto kumaanisha huyo nyoka ni kama alishawahi nitoroka mara ya kwanza.

Je? Huyu nyoka mdogo nitamuua lini? Kwa maana akikua si atanidhuru tu.

Nawasilisha kwenu wataalamu

Ila kwa sasa hii nyumba nimepanga ninahama muda wowote maana nimeshalipa kodi kwingine hivo bado nadaiwa hapa kama laki 2 hivi nikilipa tu nahamia zangu kwingine.
Ndio manake mimi kabla sijalala lazima ninywe SMART!!!.....kuondoa mambo kuota!!
 
Back
Top Bottom