Hii ngoma ndio kama inaanza bandugu, Afrika Kusini wagonjwa 9,064 kwa siku

Hii ngoma ndio kama inaanza bandugu, Afrika Kusini wagonjwa 9,064 kwa siku

Smart countries and people are no longer concerned with the (mere) cases but the focus is on the serious case. The other term of serious case is a sick people. In some countries like Sweden, the number of cases is rising but the number of serious cases fallig down. Even in Tanzania, the incidence may be the same, as they are now closing up the COVID 19 service centres.
 
Hii covid 19 ilikuwa ni mtego mdogo sana,JPM alishtuka mapema sana kwamba kadri unavyopima ndivyo unazidi kuwapa watu ugonjwa...yaani ukipimwa tu,unao..!!
Pia ni saikolojia na kwa wakenya imewaingia vizuri. Huku down south tahadhari twachikua ila maisha tunaishi kama hamna covid-19, mchawi namba moja ni imani yako.
 
MK254,

Sisi hatuhitaji kusikia ugonjwa wa kishetani ktk nchi yetu, waelezee hao hao wa A. Kusini
 
Dawa ni kupima. Pima pima.

Wanapima for the sake of justifying the expenditure of the grant given to them by the Paris Club of Government Lenders. Kwa kutumia akili ya kawaida, testing has nothing to do with the confrotation of the spread of the pandemic. There are very few countries which going on with the "testing things", most of them are just doing the interpolation of data obtained from previous daily tests.
 
Hiki kitu kinazidi kuwa hatari, Afrika Kusini namba zinapandisha balaa, karibu elfu kumi kwa siku.
Achana na mambo ya takwimu, utakuja kugundua kuwa hayakuwa na maana yoyote wakati huo muda umeshapita. Chapa kazi, kuambukizwa ni kitu cha kawaida sana, piga kazi hivyo hivyo na ugonjwa, wala hakuna tatizo.
 
Ivi umeangalia mkutano wa mwisho wa Trump hakuna social distancing wala baba yake na lockdown nyinyi watu wakibera kweli mnajifungia kisa mafua hata vyoo hamna? Mwarobaini wenu ni Swarm of locust, Kenyata aendelee tu na Kujipendekeza kwa International communities lakini tumeona pia EU wame realise list ya nchi zilizo kuwa Safe na permitted kuingia EU, Kenya pamoja na kujikomba komba still hayumo hii first batch japo system inaendelea kuwa updated.
 
Hahahaha munaongea kama vile mna uhakika. Mzee lini utakiri Tz tumeweza kutoka kwenye ushenzi wa corona japo ipo?

Kuweza corona lazima utumie mbinu za kisayansi maana yenyewe ni tatizo la kisayansi, sio kujichokea na kujiaminisha umeweza huku umewaacha watu wataabike wenyewe.
 
Tunamshukuru Rais wetu ametuondolea corona

Hajaondoa corona, kawaondolea wananchi wake hofu, ambayo ndiyo ugonjwa mkubwa kuliko corona yenyewe. Hofu ilivyoondoka watu kinga zao zikaimarika, na pia kwa kuwa walisihiwa kutumia herbal tonic kibao, ndiyo usiseme, watu wako fit balaa. Na miezi tisa baadaye tunategemea kuwa na baby boom, maana mchanganyiko wa limao, tangawizi, saumu, pilipili manga kwa mbali, yaani unafanya "makamuzi" kama vile una umri wa miaka 27 vile.
 
MK254,

Waziri Ummy Mwalimu afunga kambi ya wagonjwa wa Corona wilayani Kibaha Pwani

muungwana.co.tz

Jul 3, 2020 9:00 PM

[https://1]

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii na Wazee Ummy Mwalimu amefunga kambi ya wagonjwa wa Corona iliyokuwa Lulanzi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Akifunga kambi hiyo jana ambapo alisema, kati ya kambi 85 zilizokuwa zinahudumia wagonjwa wa Corona zimebaki 11 ambazo nazo zinaendelea kufungwa siku zijazo kutokana na ugonjwa huo kuendelea kutokomea hapa nchini.

Aliwasihi wananchi kuacha kujibweteka na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ili kuepuka kupata maambukizi mapya.

“Tumefunga kambi 74 hadi sasa na hii hapa Lulanzi ilikuwa ni Kati ya kambi kubwa ambayo ilikuwa inapokea wagonjwa wengi na leo naifunga rasmi kwani mgonjwa wa mwisho hapa aliruhusiwa Mei 26 hakuna mwingine aliyepokelewa hadi leo” alisema.

Aidha Waziri Ummy aliwataka wakazi wa Kibaha kufika katika Hospitali ya Wilaya kupata huduma na kuondoa hofu ya kuwa kituoni hapo bado kuna wagonjwa wa Corona.

Alisema, wananchi wanatakiwa kuondoa hofu kwani majengo yote yamefanyiwa usafi baada ya wagonjwa kuondoka katika Hospitali.

” Lulanzi sio tena kambi ya wagonjwa wa Corona , wananchi ondoeni wasiwasi na mfike kupata huduma za afya, tusikimbilie Tumbi ile ni Hospitali ya Rufaa tungependa ibaki kutoa huduma za hadhi ya Rufaa” alisema Ummy.

Alitumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa Halmashauri ya mji wa Kibaha kusimamia utoaji wa huduma za viwango vinavyostahili kwa wagonjwa.

Akiongea katika Hospitali hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alimshukuru Rais Pombe Magufuli kwa Hospitali hiyo ambayo imemaliza uhitaji wa Hospitali ya Wilaya aliyokuwa akiiomba kwa zaidi ya miaka saba iliyopita.

Koka aliwataka wananchi kufika kutibiwa katika Hospitali hiyo ambayo imeondoa kilio cha uwepo wa Hospitali ya Wilaya .

Alisema changamoto iliyopo katika Hospitali hiyo kwasasa ni pamoja na ubovu wa barabara na gari la wagonjwa ambalo Waziri Ummy aliahidi litapatikana hivi karibuni.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema, Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma za kawaida kwa wagonjwa Juni 6 na kwamba jamii bado ina Mashaka kufika katika Hospitali hiyo.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG

Maoni yaliyotolewa katika taarifa hii ni ya mwandishi mwenyewe, hayana uhusiano na Opera News

[https://cdn-af]
 
Niliwaambia wakenya huu mwaka huu lazima mtii. Sasa mnajifungia na korona inazidi kwenu nchi yenu inazidi kudidimia kuelekea lower income wakati sisi licha ya korona tunazidi kupaa
Corona ni ugonjwa wa kistratejia umekuja kufanya mapinduzi ya kiuchumi duniani sasa mpaka ukiisha itabaki story tu Tanzania ilikuwa masikini lakini sasa hv hatuwafikii hata robo hahahaha
 
MK254, Sasa kazi kwenu sisi tunafunga ninyi munaoneza kambi za Corona na bado hapo tv zenu watangaze na hii basi kama kweli wao wanajifanya wanajua kuaandika habari.
 
Tuwape pole hawa majirani wa kaskazini...
IMG_20200704_201857_080.JPG
 
Kuweza corona lazima utumie mbinu za kisayansi maana yenyewe ni tatizo la kisayansi, sio kujichokea na kujiaminisha umeweza huku umewaacha watu wataabike wenyewe.

Nipe majina ya watu wote wanaotaabika na Corona Tanzania unaowaongelea hapa.
 
Tusitishane Bure Tuchape COVID 19 Haipo. Ndugu Zangu Tutaishi Nao Kama Ukimwi
 
Back
Top Bottom