Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
No Reforms No ElectionWakati wa Yesu kulikuwa na uonevu mkubwa wa kisiasa. Lakini Yesu alijikita kwenye misheni ya Ufalme wa MUNGU KITU Bora kuliko siasa za mpito.
Wakati wa Paulo kulikuwa na harakati nyingi sana za siasa Asia na ulaya. Tena uchawa kulikuwa umekithiri lakini alijikita katika misheni ya kumueleza Yesu na uwezo wake. Na Ufalme wa MUNGU.
Gwajima KWA kipawa na uwezo aliopewa naamini angejikita kwenye INJILI na mambo ya Ufalme wa MUNGU angebatiza Hadi watekaji. Nakumbuka mtumishi mmoja Scotland alihubiri Hadi bar zikakoswa wateja. Paulo alihubiri Hadi waganga wa kienyeji wa efeso na MIUNGU yao wakafirisika KWA kukosa wateja.
Ukiona watumishi wa Mungu wako bize ila aggregate ya matokeo yao inabaki vilevile. Au unafanya watu watafakari viongozi wa Siasa badala ya Mungu jua Kuna tatizo kubwa.
Naamini KWA ushawishi na vipaji alovyopewa Gwajima anagejikita kwenye INJILI angebatiza kabisa Hadi watekaji na wanaowatuma (kama wanatumwa). Kama mtekaji sugu Sauli wa Tarso alibatizwa naamini Gwajima angesitisha hii taaruki KWA kujikuta na ijili zaidi ya maelezo na press za kisiasa.
Tungeshuhudia anguko kubwa la waumini wa uislam na upagani nchini na Kristo angechukua usukani wa Taifa.
Ni hayo tu.
Mtumishi
Matunduizi