Hii ni ajabu ya Dunia. Wana CCM wenyewe hawajui ni kwa nini chama chao kinaitwa Chama cha Mapinduzi!

muhimu zaidi ni yale mambo ambayo wananchi wananufaika nayo kutoka Chama Cha Mapinduzi mathalani maji, elimu, afya, amani n.k

yaani wadau waanze kubabaika na kwanini wewe unaitwa@Allen Kilewella? ili imsaidie nini kwa mfano?

wananchi wanahitaji umeme, wanahitaji miundombinu ya maana, waanze kubabaika na sijui kujua nini na nini ilikua vipi, hawana kazi za kufanya?

elimu ya msingi, secondary na elimu ya juu ulizembea kujifunza hayo, halafu ndio uje kuuliza watu wakiwa uraiani na shughuli zao, ili ikusaidie nini ukijua gentleman?🐒
 
Yaani ulivoandika ni kama vile hivyo vitu ni toshelevu hata Kwa 30% ya uhitaji wake kwa watanzania.

Wanachama hawajui kwa nini chama chao kinaitwa Mapinduzi!?
 
Yaani ulivoandika ni kama vile hivyo vitu ni toshelevu hata Kwa 30% ya uhitaji wake kwa watanzania.

Wanachama hawajui kwa nini chama chao kinaitwa Mapinduzi!?
umeenda mbali kama vile unauliza jambo la maaaana!!!!!

muulize mtu yeyote maana ya jina lake au ukoo wake kama atakwambia kitu?
atakwambia tu ni Fulani wa ukoo wa kwa mzee Mroso, muulize Mroso maana yake nini kama atakwambia japo haina maana yoyote 🐒
 
Kwa ivo unataka kusema chama chenu kiliitwa mapinduzi bila ya sababu maalum!?
 
Kwa ivo unataka kusema chama chenu kiliitwa mapinduzi bila ya sababu maalum!?
nadhan huenda ikawa kama wewe tu ulivyo itwa Allen sijui nani huko hata havieleweki 🤣

lakini nyuzi zako wadau wanapata ufahamu na uelewa Fulani, hii ikimaanisha Allen nani nani sijui huko haina maana yoyote kwao,

cha maana kwao ni hayo madini, maudhui na si vinginevyo 🐒
 
Mtoa mada hapa umepotezwa
Allen Kilewella
 
Umemalizia vizuri, imepoteza hadi reply yangu niliyokuwa niiweke. Lakini bado ni vigumu pia kuthibitisha kama wenyewe walikuwa katika hilo wazo la Hegelian dialectic hata katika nadharia tu.
Kuna watu kama kina Babu, Hanga, Nyerere, Mwiru ma ideologues wale kina Mwakawago etc na to some extent kina Mkapa, Sokoine, Msekwa na Warioba na wasomi wengine wa siku hizo walisoma haya mambo na kuyaelewa usiwachukulie poa hivyo.
 
Siwachukulii poa katika hizo nadharia za ujamaa na Ukomunisti ila sijawahi kuona yeyote akizungumzia au akigusia maana iliyo nyuma ya jina la chama chao walichokiunda 1977.
 
Siwachukulii poa katika hizo nadharia za ujamaa na Ukomunisti ila sijawahi kuona yeyote akizungumzia au akigusia maana iliyo nyuma ya jina la chama chao walichokiunda 1977.
Wamei localize na kuifanya yao hawawezi kukwambia wameitoa kwa Hegel kwa sababu wataonekana wanagezea. Hawataki kuonekana wamegezea itikadi, wanataka kuonekana wameitunga wao. Imetokana na watu wao.

Na pia Watanzania wangapi wanamjua Hegel?

Ukimwambia Mtanzania wa kawaida "Hegelian Dialectic" ataona kama unamtukana.

Lakini ukimwambia "Mapinduzi Daima" ataelewa kirahisi zaidi.

Yote mawili yana maana moja.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi ni chama cha Kijamaa chenye falsafa za "Mapinduzi Daima" ambazo mizizi yake ya kiitikadi inatoka kwa Hegel kwenye "Hegelian Dialectic".

Na makomredi wa Zanzibar kina Babu na Hanga walikuwa na mchango mkubwa wa kuieneza dhana hii ya "Mapinduzi Daima" kuanzia "Mapinduzi Matukufu ya 1964" mpaka "Mapinduzi Daima" ya TVZ, mpaka "Serikali ya Mapinduzi Zanzibar", ndiyo chama kikapata jina hapo hapo kikawa Chama cha Mapinduzi.
 
Uko very shallow aisee
 
Ndio hata TANU ASP hadi CCM. Ni Vyama vya mlengo kushoto Ukomonisti na ujamaa hawa wanaakini kwenye Mabadiliko, au mapinduzi . Change, Revolutionary Equality Usawa
 
Ukiangalia kwa umakini wanachama wa CCM hawana tofauti sana na waumini wa Kiislam. Unakuta mtu anaamini kitu lakini hajuwi chochote kuhusu dini yake.
 
Ushawahi kuona mwana CCM ana akili timamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…