Hii ni 2025 na hili ni jiji namba moja Tanzania ambalo tunajivunia ila wananchi wake bado wanatumia maji ya chemi Chemi, yaani mwaka 2025 bado tupo primitive stage na hapa ni jijini Dar es salaam, sasa mikoa jirani hali ikoje.
_________
Wakazi wa Ubungo Riverside Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wanachota maji kwenye chemchem iliyopo katika Mto Gide leo Ijumaa Desemba 12, 2025.
Kwa wiki kadhaa sasa maeneo mengi ya Mkoa wa Dar es Salaam yamekuwa yakikabiliwa na uhaba wa maji hatua inayowalazimu kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo.
Desemba 10, 2025 akuzungumza na waandishi habari, Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema oparesheni wanazofanya ikiwemo kurudisha Mto Ruvu katika hali yake ya kawaida imeanza kuleta matunda na kipaumbele cha Serikali ni kuwa kiwango cha maji kinachopatikana kigawiwe kwa usawa.