Uwanja utajengwa kama Engineer Hersi alivyo ahidi, Shida iliyopo ilikua eneo dogo maana utajengwa pale pale Kaunda.
Yanga walimwomba Rais Samia awasaidie eneo kwakua Serikali ilisha walipa wakazi wa eneo lile kupisha mradi wa Daraja la Jangwani na upanuzi wa mto Msimbazi na vivutio vingine.
Mradiuo wa Serikali utahusisha kumbi za starehe, maeneo ya maegesho, upanuzi wa mto Msimbazi utakao kua na mandhali ya kitalii kwaiyo ni mradi mkubwa unao fadhiliwa na Benk ya Dunia.
Kama mtakumbuka vizuri Rais Samia Ali waambia Yanga: mmeniomba jambo lenu ( Eneo la ujenzi) na Mimi Naomba mshughukikie Swala la Feisal mu mwache akacheze.
Kwaiyo Mradi uo wa upanuzi wa mto Msimbazi na Daraja la Jangwani unao fadhiliwa na Benk ya Dunia utakua wa kisasa.
Yanga walitakiwa wapeleke michoro ya uwanja utakao kaa katika eneo ilo kwakua mradi mkubwa wa kisasa hauta ruhusu ujenzi wa uwanja ambao auendani na mradi uo.
Kwa ujumla Yanga walishakua tayari muda mrefu kuanza ujenzi ila ni lazima Serikali ianze ujenzi wa mradi na usanifu wa mradi kwa ujumla uende sambanba na ujenzi wa uwanja uo wa Yanga