Hii ni idadi ndogo ya bidhaa toka Kenya na Tanzania hatuwezi kutengeneza

Hii ni idadi ndogo ya bidhaa toka Kenya na Tanzania hatuwezi kutengeneza

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,298
Sitaki kupoteza muda

1. Blueband
2. Pipi kali (tropical mint)
3. PK
4. Big G (original)
5. Gomba (bigijii) bidhaa za kampuni ya K sweet)
6 . Chumvi
7. Jamaa (sabuni)
8. Omo
9. Kiwi (rangi ya viatu original)
10. Dai n.k

Ni bidhaa nyingi sana tunapata toka huko.

Kama tukilipa kisasi cha mahindi yetu tungewazidi kete lakini jambo la kushangaza zikitengenezwa hapa Tanzania zinakuwa fake au hazina ubora kama hizi.

Ni nani asiekula pipi kali ya tropical mint?

Blueband tunatengeneza wapi?

Tanzania inatengeneza bigijii lakini hakuna kama za Kenya (kama ipo ya TZ nitajieni)

Siku hizi kuna kiwi za kangaroo toka Uchina lakini Kiwi toka Kenya itabaki kuwa juu tu toka zamani.

Natamani kutaja umuhimu wa kila bidhaa hapo lakini sitamaliza. Taja bidhaa ambayo sio muhimu kwa Tanzania au Tanzania inatengeneza nzuri zaidi.
 
Zamani hizo pipi kali na big G zilikuwa zinatengenezwa hapa Tz. Nadhani chini ya marehemu Mengi alichukua franchise Uniliver. Sijui kilitokea nini uniliver Mikocheni ikafa...imebaki huko Irings kwenye Chai nadhani.
 
... hata dakika moja huwezi kushindanisha bidhaa iliyoongezewa ubora (za viwandani) na iliyotolewa shamba na sumu kuvu na mavumbi yake hivyo hivyo mna-export; never!
 
Una maanisha Kenyata ni juha kwa sababu kapiga ban mahindi toka tz?
Mimi naona hakuna haja ya kuwanyoosha hao nyang'au wote. Tumnyooshe hiyo mlevi peke yake kwa kuzuia maziwa, insurance na ile bank ipate figisu..ile supermarket nadhani tayari imekwisha..na kunogesha tunapiga pin kwa wanae mlamba miguu..fungia na products za malkia chini ya mgongo wa wakunya Uniliver..ili wamfurushe huyo mlevi mjengoni haraka sana.
 
Bidhaa ya Unilever hiyo brand kubwa ya misosi duniani
... vyovyote hoja ni kwamba inavuka mpaka kuingia Tanzania kutokea wapi? Kwanini hao Unilever (mabeberu) hawakuja ku-invest Tz? Kuvuta mitaji ya kigeni inahitaji akili nyingi sio kujitoa ufahamu halafu waje tu! Tz inaihitaji zaidi dunia kuliko dunia inavyoihitaji Tz.
 
Back
Top Bottom