Hii ni idadi ndogo ya bidhaa toka Kenya na Tanzania hatuwezi kutengeneza

Hii ni idadi ndogo ya bidhaa toka Kenya na Tanzania hatuwezi kutengeneza

miaka ya nyuma kipindi tulikuwa na Tanbond wakenya wao walikuwa na blueband cha kushangaza wao mpaka sasa wanayo ila sisi hatuna, tulikuwa na mazima fresh matamu sana yalikuwa kwenye pembe tatu rangi ya kijana na kaki haya maziwa nayakumbuka hadi leo ukipikia chai unapata harufu nzuri sana sijui yapo wapi.......... tunashida sana.
 
Sitaki kupoteza muda

1. Blueband
2. Pipi kali (tropical mint)
3. PK
4. Big G (original)
5. Gomba (bigijii) bidhaa za kampuni ya K sweet)
6 . Chumvi
7. Jamaa (sabuni)
8. Omo
9. Kiwi (rangi ya viatu original)
10. Dai n.k

Ni bidhaa nyingi sana tunapata toka huko.

Kama tukilipa kisasi cha mahindi yetu tungewazidi kete lakini jambo la kushangaza zikitengenezwa hapa Tanzania zinakuwa fake au hazina ubora kama hizi.

Ni nani asiekula pipi kali ya tropical mint?

Blueband tunatengeneza wapi?

Tanzania inatengeneza bigijii lakini hakuna kama za Kenya (kama ipo ya TZ nitajieni)

Siku hizi kuna kiwi za kangaroo toka Uchina lakini Kiwi toka Kenya itabaki kuwa juu tu toka zamani.

Natamani kutaja umuhimu wa kila bidhaa hapo lakini sitamaliza. Taja bidhaa ambayo sio muhimu kwa Tanzania au Tanzania inatengeneza nzuri zaidi.
Kodi na Sheria za kodi,feza na viongozi wasio na uelewa wa Biashara ndio mchawi wa Nchi
 
Bidhaa zao si bora zina kemikali zinazoongeza usababishi wa kansa. Tunaweza kutengeneza zetu zikatumika sana tu.
 
Kiwanda cha Tanbond kilishakufa siku nyingi
Viwanda vya Kenya ni kwa hisani ya mkoloni,ukinywa Milo kutoka kenya inayouzwa Tanzania na inayouzwa EU tunayouziwa bado ovyo. Ukija kwenye mngaro wa viatu na siagi kiwi na blueband ya kenya itabaki juu milele.Tanbondi yetu itasubiri sana. TZ KONYAGI Iitabaki juu milele.
 
Back
Top Bottom