Hii ni kali, polisi wenye daladala wanaiibia serikali

Hii ni kali, polisi wenye daladala wanaiibia serikali

Hii nchi ukipata mia mbili ukapata chakula na familia yako mengine ni kuyaangalia tuu maana unaweza kudata. Hakuna kitakachorekebishwa hapo unajichosha
 
Tulio na kumbukumbu , miaka ya 70 mwanzoni, Rais Nyerere alichukizwa na rushwa na utendaji mbovu wa maafisa wa juu jeshi la polisi.

Aliwafukuza wote baada ya utafiti kufanyika na kuthibitika kuwa si waaminifu kazini.
Mama Samia tunaomba afaye hivyo.

Afisa wa polisi hawezi kwenda mwenyewe, kiholela, kuchukua kwenye kituo chao mafuta ya diesel bila kuwepo mtandao wa wizi.
Wakiwafukuza hovyo unadhani nyakati za uchaguzi watawatumia kina nani ?
 
Tulio na kumbukumbu , miaka ya 70 mwanzoni, Rais Nyerere alichukizwa na rushwa na utendaji mbovu wa maafisa wa juu jeshi la polisi.

Aliwafukuza wote baada ya utafiti kufanyika na kuthibitika kuwa si waaminifu kazini.
Aliweza kuwafukuza kwakuwa yeye mwenyewe alikuwa na uaminifu usio na shaka.

Hali ni tofauti leo. Labda hao polisi nao wameona hapo ndipo urefu wa kamba zao unapofikia! 😆😆
 
Aliweza kuwafukuza kwakuwa yeye mwenyewe alikuwa na uaminifu usio na shaka.

Hali ni tofauti leo. Labda hao polisi nao wameona hapo ndipo urefu wa kamba zao unapofikia! 😆😆
Mama asipolishughulikia hili kikamilifu litaisumbua serikali huko mbele.
 
Hujajibu swali.
Kula kwa urefu wa kamba yako maana yake kufanya uhalifu wa wazi wazi?
Kwa watumishi wa serikali katili ya CCM kula kwa urefu wa kwamba ni kufanya uhalifu wa wazi-wazi na ndiyomaana kauli hiyo ilitolewa wazi-wazi.
 
Wana maximize profit Kwa mgongo wa walipakodi maskini. Huko ndiko hata tozo zetu zinatafunwa.
 
Duh kwahiyo wanaenda kujaza mafuta ya GIPSA kwenye daladala zao au mimi ndo sijaelewa? kudadek kweli enzi ya mkw.ere ilisharudi. ni fujo kwa kwenda mbele bila hofu!
 
Tahadhali Ichukuliwe katika kutoa tuhuma hakuna mtu ambaye anahaki ya kutoa hukumu katika tuhuma ambazo hazijathibitishwa bila kuacha Shaka yoyote.

NI Muhimu kutunza haki za asili za Binadamu.

Kama tukiruhusu kunyoshea vidole watuhumiwa na ku generalized Makosa Kwa wote wakati wahusika wanajulikana ni hatari kubwa Kwa mustakabali wa haki za Binadamu.

Hakuna forum ya Askari Polisi kujibu tuhuma hasa hizi za jumla Sisi tuliolelewa na Polisi na kuishi nao Kwa karibu tuwasemee hasa katika hali ngumu wanayopitia.

Hoja kwamba hawana mafunzo na wakati wa kuwaajiri Kuna mapungufu inatakiwa ifanyiwe utafiti wa kina maana haiakisi ukweli wa hali halisi Kwani Kuna ushahidi wa kutosha kwamba watu wema wanaweza kuharibiwa na mazingira.

Pia umaskini ni chanzo kikubwa cha kubadili tabia tufuatilie kuona jinsi mtu mwenye njaa anayoweza kufanya Jambo ambalo kama angekuwa ameshiba asingefanya.

Vetting Kwa kuangalia Sura au muonekano haitoshi kubaini mtu mbaya au mzuri hapa Muhimu ni kuongeza mbinu zaidi za kuwajua Askari wabovu.

Hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe bila Kuwa na muhali kama Kuna ushahidi wa Wizi basi hatua Kali zichukuliwe badala ya kuongelea kwenye vyombo vya habali badala yake viongelewe kwenye tahasisi husika za kisheria.

Polisi wachache wahalifu wasichukuliwe kwamba wanafanya uhalifu Kwa niaba ya jeshi zima.
 
Kwa hiyo polisi mwizi, tena ofisa, atamkamataje mwizi?
Hilo sio la kujiuliza, hushangai mnamkamata mwizi asubuhi mnampeleka kituoni jioni mnakutana nae kwenye viti virefu anashushia bia baridi?
 
Back
Top Bottom