Madam madini yanashikiliwa na hao viumbe.
Usidhani ukitaka kufanya biashara ya madini unaingia tu unafanya unapata,hata ukiwa na mabilioni kama hao jamaa hawataki ushike mali zao huzishiki.
Kitendo cha kumuita akufanikishie upate jiwe ni sawa na kutumia pesa yake.
Tena bora ufanye hivyo,maana ukitaka pesa kama pesa Yani hizi hapa masharti yake ni zaidi ya hayo nilokutajia.
Kuna kisomo kinaitwa Qassam/azma,hivi ni visomo vya kuwaita marohani wenye mali za madini na pesa.
Mie nilipoenda na huyo ndugu yangu tulipiga kisomo cha kumuita Hamamah.Huyu anakuja kama ndege tai mkubwa,na kadri unavyozidi kusoma azma anabadilika kuwa mwanamke mzuri sana.
Masharti ya kupewa pesa kama pesa;
-Ukubali kuoana nae yani yeye awe mke wako.
-Usioe mwanamke mwingine zaidi ya yeye huyo jini.
-Usijaribu kujihusisha kivyovyote na wanawake wengine.
Mamaangu wewe kuweza!?
Nikakubali masharti yale nilokutajia juu kule,masharti yale ni ya wao kukupa pete itakayokuwezesha kupata dhahabu kila unapoenda machimboni,maana Hamamah ni malkia wa dhahabu.
Sasa kuivaa ile pete na ukatafuta dhahabu pale ni sawa anajitafutia yeye.
Sasa kauze hiyo dhahabu ambayo kakusaidia kuipata halafu utombee pesa yake.
Alooooo😂😂😂 kazi unayo.
Sasa jiulize ningekubali masharti ya pesa kama pesa kingenikuta nini!?