Hii ni Maalum kwa Wafanyabiashara wa sasa au wanaotarajia kufanya biashara siku za usoni

Hii ni Maalum kwa Wafanyabiashara wa sasa au wanaotarajia kufanya biashara siku za usoni

Wakuu
Kama wewe ni mfanyabiashara jiandae kwa kuingia gharama hizi katika uendeshaji(zote ni za serikali ispokua # moja)

1. Kodi ya Frame – Malipo ya pango kwa mwenye jengo la biashara.
2. Kodi ya TRA – Kodi ya mapato au VAT inayotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
3. Leseni ya Biashara – Kibali cha kuendesha biashara, hulipwa kila mwaka.
4. Service Levy – Ada ya huduma kwa halmashauri kutokana na huduma za jamii zinazotolewa.
5. Fire Extinguisher – Gharama ya kifaa cha kuzimia moto kwa usalama wa biashara.
6. Kodi inayotokana na Mkataba wa Pango – Gharama ya kodi inayotokana na mkataba wa pango utalipia mpangaji (mwenye nyumba haangaiki)
7. Kodi ya kuuza bidhaa Mtandaoni – hii itaanza rasmi baada ya mwezi mmoja kutoka sasa. Wale wa instagram, tiktok au X mjiandae kujisalimisha.
8. Ushuru wa Taka – Ada ya kusafisha na kuondoa taka za biashara.
9. Ushuru wa Bango/Matangazo – Malipo ya kibali cha mabango ya biashara au matangazo.

Hii serikali itizame sana hizi gharama. Zinakatisha tamaa sana, utazilipa bila kujali biashara imetiki au imefeli.
Upo tayari?
Unatamani nini kiondolewe hapo?
Mi naona zingebaki
1 na 2 tu, hizi taka taka zingine walipie wabunge.
 
Reforms zikifanyika ,tutapata viongozi wenye maono na wenye kuweza kujua uhalisia wa mambo mitaani,kwa maana watakuwa wakiwatumikia wananchi na si kugonga meza na kupiga vigeregere ,mpaka kupeleka wengine kutuambia tuhame nchi,
Toa kuanzia 4 ,5 ,6 na 9

nawewe unaamini kabisa kuwa reforms zitafanyika? hivi nyinyi vijana munawachukuliaje CCM?
 
hapo TRA kuna kodi 2, mana na VAT pia hua analipa mfanyabiashara kiuhalisia mazingira ya kibongo
 
hayo madeni yaliyokopwa yameleta faida gani kwenye nchi zaidi ya kuwanufaisha mafisadi? kutumia mtumie ninyi ila kulipa tulipe sisi huo ni uonevu
Hawajalii mkuu
Focus yao kubwa ni kuwaza deni wananchi wanalipaje... wabunge hawatutetei kbs
 
Kwan watakataa kufanya reforms miaka yote?
kabisa, CCM kufanya reforms maana yake ni kujichimbia kaburi kwa mikono yao, hilo jambo hawawezi lifanya kabisa without kupigwa high pressing ambayo ita result ngovu kutoka nje kuingilia, ambayo kwa hali inavyokwenda sasa sioni dalili
 
Back
Top Bottom