Pakome
JF-Expert Member
- Dec 8, 2024
- 1,651
- 1,129
Kwa historia ya CHADEMA tangu inaanza haijawahi kuyumba kwa kiwango hiki cha sasa ni kama inataka kusambaratika
Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kususia uchaguzi tangu isajili Chama chake
Ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kutokusimamisha mgombea wa Uraisi
Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kukosa Wabunge tofauti na ilipokuwa mikononi mwa Mbowe
CHADEMA ilipokuwa mikononi mwa Mbowe ilikuwa ikisonga mbele na hata tumeona idadi ya Wabunge pamoja na Wanachama ikiongezeka
Sio kweli kwamba CCM ndiyo imewakataa Wabunge wa CHADEMA bali uongozi wa CHADEMA wa sasa ndio umewapotezea dira Wabunge wa CHADEMA
Alisikika Lissu akisema kuwa wale Wanachama wanaotaka Ubunge wasahau hilo, hakuna cha Ubunge
Kauli kama hizo nikauli za kupotezea Wanachama Mwelekeo wala sio za kujenga
Lissu angekuwa ni kiongozi mzuri basi CHADEMA ingesonga mbele badala ya kuyumba
Nikama Lissu ameishiwa skill za uongozi badala yake anatumia backup ya Gen Z ambayo inawezakujiweka pembeni muda wowote baada ya kuchoshwa na harakati au kuendelea kuchafua CHADEMA na kuonekana ni Chama cha wahuni kwasababu ya matendo ya wanaharakati wake, ikiwemo matendo ya kupindua Serikali ambayo yapo kinyume na Katiba ya Tanzania
Lissu atakujakuonekana ni kiongozi mbovu kuwahi kutokea baada ya CHADEMA kujifia
Ni vigumu sana kwa sasa kumkumbuka Mbowe, atakumbukwa baada ya CHADEMA kupoteza kabisa mwelekeo na kujifia
Mwisho wa siku CHADEMA itakuja kuonekana kuwa ina tabia za Gen Z kwasababu matendo yake ni kama yanafanana
Kauli za kuita viongozi wa Serikali kuwa ni wezi alianza Lissu kwa kutamka hadharani
Hata kama viongozi ni wezi kwani hakuna kauli za staha ambazo zinatumika tangu kuumbwa kwa ulimwengu?
Je, ni lazima yatumike matusi ndipo ujumbe ufike?
Lissu alilalamika sana kwamba Mbowe hafai badala yake yeye ndiye anafaa, inakuwaje tena anakwama wakati alisema yeye ndiye mwenye sifa zote za kiongozi anayetakiwa kuongoza CHADEMA
Sifa kubwa ya kiongozi wa Chama cha Siasa ni kuongeza wafuasi na sio kupunguza
Kiongozi yeyote wa Chama cha siasa anayepunguza Wanachama huwa anaonekana kama mharibifu
CCM inafahamu majukumu ya Mwenyekiti wake na hii ndiyo sababu ya Chama hicho kupambana kwa namna yeyote kuhakikisha idadi ya Wanachama wake inaongezeka na sio kupungua
Inapigana usiku na mchana, kwa namna yeyote ile kuongeza idadi ya Wanachama wake, huku Lissu akipigana kufa na kupona kupunguza idadi ya Wanachama wake
Wanachama ni lulu na hazina ya Chama, sababu hii ndiyo inayoifanya CCM iwapokee Wanachama wa vyama vingine waliotupwa nje na kuendelea kuongeza nguvu ya rasilimali watu
"Uchafu ulioutupa wewe kwa mwenzio ni dhahabu"
Ni sawa na kauli ya " enyi wote mlioelemewa mizigo njooni CCM mpumzishwe"
CHADEMA ya Lissu imekuwa na kazi ya kutafuta Watakatifu, inataka kuwa na Wanachama Watakatifu peke yake
Ni sawa na Mwanaume anayetafuta Mwanamke mtakatifu jambo ambalo ni gumu sana kwa dunia ya sasa mara nyingi ushauri unaofaa mtu mwenye fikra hizo ni ule wa yeye kuumba wakwake mwenyewe labda ndiye atakayeweza kuwa na sifa anazozitaka yeye