Hii ni mara ya pili polisi wanashambuliwa mtaa wa Narung'ombe na Ndanda, Kariakoo

Hii ni mara ya pili polisi wanashambuliwa mtaa wa Narung'ombe na Ndanda, Kariakoo

mkuu unazungumzia polisi kupigwa au kuzongwa zongwa na wasifanye kazi kwa usahihi???

wapige polisi halafu waendelee kukaa hapo kijiweni[emoji28][emoji28][emoji28]hauko serious.

aither umeonewa au umefanya kosa,kitendo cha kumpiga askari ni kutafuta kesi ya msingi kabisa,inayoweza kusababisha kufungwa,kulemazwa au kufa kabisa.
Acha kutisha raia mkiendelea na ujinga wenu mtapata kibano tu bila kuangalia khaki zenu
 
Mkuu, unazungumzia polisi au wale wagambo waliowekwa kufanya operation uchwara ya kionevu kuwaonea bodaboda vijiweni kwa kisingizio cha wrong parking na kisha kuwatoza faini ya 70,000/?

Kama ni hao sio polisi ni wagambo na kipigo ni haki yao kabisa [emoji106]
Talking about hawa. Wiki mbili zilizopita nimeshuhudia kifo cha mmoja wao pale mtaa wa Uhuru. Dereva wa Eicher aliwagonga akaenda kujisalimisha kituo cha polisi.
 
Kwamba polisi wamekuja kufanya kazi na mkawazuia kwa kuwapiga? Na wakaondoka? Hawakua na silaha? Kama ni kweli hongereni ila kuweni makini siku nyingine katika mambo ambayo polisi karuhusiwa kutumia silaha yake na ikibidi kuua kabisa ni pindi anapo shambuliwa akiwa na silaha.

Sheria inamtaka polisi aitumie silaha yake kujilinda ili ailinde na hiyo silaha na akishindwa kufanya hivyo anashtakiwa, kwahiyo kuweni makini pindi mnapomshambulia polisi mwenye silaha.
 
Talking about hawa. Wiki mbili zilizopita nimeshuhudia kifo cha mmoja wao pale mtaa wa Uhuru. Dereva wa Eicher aliwagonga akaenda kujisalimisha kituo cha polisi.
Hao ni suala la muda tu tutasikia mengine...

Kwanza hiyo operation ni kama mradi wa watu fulani hivi, ipo ki mchongo mchongo...

Wameji organize wakaokota vijana wasio hata na uhakika wa kupata mlo wa siku, wamewakabidhi virungu kisha wamekodi hizo gari na kuzurura nao hao wahuni kusumbua vijana walioamua kutafuta riziki ki halali.

Wakikukamata hawakupeleki police, kuna yard yao kule karibu na MSD (nyuma ya veta) ndo wanakushurutisha ulipe hiyo fine ya mchongo 70k wakuachie...

Bodaboda hawakai kwa amani vijiweni, kuna boda alinusurika kifo baada yakugongwa na mwendokasi pale mataa ya morogoro rd / lumumba ( Aura mall ), katika harakati za kuwakimbia hao kamata kamata...

Ni suala la muda tu tutasikia ya kusikia yetu macho.
 
Siungi mkono polisi kupigwa , wala polisi kuonea watu, lakini inafikirisha kidogo, haiwezekani eneo moja hilo hilo mpigwe na kuzomewa mara mbili na mshindwe kufanya kazi iliyowapeleka pale isipokuwa operation mfanyayo ni batili

Wakiwa kwenye msako wa kukamata bodaboda wakorofi kila wakifika mtaa wa ndanda na narungombe ni kichapo tu na aibu kutoka kwa vijana wa kisambaa waendeshao bodaboda

Na hii inathibitisha udhaifu wa polisi au dhulma waifanyayo
Kama wasemavyo vita inaweza kuanzia huku huku kwenye bodaboda na machinga, sikuamini macho yangu, polisi anachangiwa mpaka wanakula kona[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787], picha ipo ila kimaadili haifai kuwekwa hapa
Kazi kwenu
polisi ndio walio jishusi heshima kwa sababu ya kuomba kwao na kupokea rushwa ingawa sio hao walio enda kuwakamata wamesha wazoesha kuwapa 2000 na kuwaachia sasa jamaa wanashangaa kukamatwa mtoto umleavio ndivio akuavio lakini boda boda nao wanajipalia mkaa
 
Kwamba polisi wamekuja kufanya kazi na mkawazuia kwa kuwapiga? Na wakaondoka? Hawakua na silaha? Kama ni kweli hongereni ila kuweni makini siku nyingine katika mambo ambayo polisi karuhusiwa kutumia silaha yake na ikibidi kuua kabisa ni pindi anapo shambuliwa akiwa na silaha.

Sheria inamtaka polisi aitumie silaha yake kujilinda ili ailinde na hiyo silaha na akishindwa kufanya hivyo anashtakiwa, kwahiyo kuweni makini pindi mnapomshambulia polisi mwenye silaha.
tatizo walisha wazoesha kuchukua hela kwa makosa haya sasa unapoenda kuwa kamata unafikilia nini
 
Back
Top Bottom