Hii ni milio mbalimbali (Beep noise) inayoashiria kuwepo hitilafu kwenye computer yako

Hii ni milio mbalimbali (Beep noise) inayoashiria kuwepo hitilafu kwenye computer yako

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mara nyingi kwenye kompyuta kumekuwa na milio mbalimbali kuonyesha kwamba Kompyuta kuna hitilafu mbalimbali, na hali hii inapotokea inakuwa ni vyema kutambua tatizo lipo sehemu gani hasa.

1. Sauti kidogo tu (very short beep) sauti hii huonesha kuwepo kwa tatizo kwenye Ubaomama (motherboard) Pia inaweza kudhihirisha kuwepo kwa tatizo kwenye BIOS AWARD.

2. Kompyuta ina-beep kwa muda mrefu na baadae hufuatiwa na sauti mara tatu mfululizo kwa kipindi kifupi ishara hiyo huonyesha kwamba kuna tatizo kwenye mfumo wa “graphics card”.

3. Kompyuta inapiga kelele muda mfupi na baadae inafuatiwa na kelele (beep noise) mara tatu kwa kipindi kirefu (three sequential long beeps) hii ikiwa na maana kwamba RAM ina tatizo.

4. Ukisikia kompyuta yako ina-beep inaacha, ina-beep inaacha na baadaye ina-beep mfululizo hapo elewa kuwa kuna tatizo kwenye mfumo wa uunganiko kwenye “processor/ CPU (central processing unit).

5. Kompyuta ina-beep Mara tatu inaacha inabeep-mara tatu tena inaacha na kufuatiwa na ku-beep mara nne hapo elewa kwamba kuna tatizo kwenye “video memory”.

6. Pale unapotokea mlio mmoja wa muda mrefu na baadaye inaanza milio tisa ya muda mfupi (nine short beeps) hii ina maana kwamba kuna tataizo kwenye BIOS.

7. Kompyuta inapotoa milio mara 3 (three beeps) ikatulia ikatoa milio minne (four beeps) ikatulia na baadaye inafuatiwa na mlio mmoja mfupi hapo elewa kwamba kuna tatizo kwenye “graphics card”.

8. Kompyuta inapotoa milio minne (Four beeps), ikatulia na baadae ikatoa milio mitatu (three beeps) ikatulia na baadae mlio mmoja tu hii nayo huonesha kwamba mfumo wa RAM kuna hitilafu.

9. Kompyuta inapotoa milio mitano (5) kwa ufupi sana hii nayo huonyesha kwamba kuna tatizo kwenye ‘Processor” (CPU).

10. Pia inapotokea kompyuta ikatoa mlio kwa kipindi kirefu bila kukata (Long, constant beeps) elewa kuwa kuna tatizo kwenye Mfumo wa RAM kwa ujumla.

Unapokutwa na tatizo hilo kwenye Kompyuta yako inakuwa ni rahisi sana kutambua wapi kuna tatizo ili lipate kupatiwa ufumbuzi wa kina uliotukuka.

Credit: Cataux Computers
 
Back
Top Bottom