Hii ni miujiza siamini hata! Nahisi naota

Hii ni miujiza siamini hata! Nahisi naota

Inasikitisha sana
Hapa niamini hii kitu ni kweli.


Mimi NIKIWA broke nabeti nachapwa balaa ila nikichukua nachotaka kukibetia nikampa kapuku au mtu asiyejiweza asiye jua kesho atakupa nini.


Nashangaa madeal YANAKUJA automatically bila hata kujiboost.


Toa kwa moto uone kama hutomoata Setfree mtumishi utafunguliwa milango ya baraka zote nyuma mbele Mungu ni mwema yupo tu.
 
Hiyo ilikuwa ni sadaka kubwa sana,Mimi niliwahi kulipwa pesa ya madai ambayo nilikuwa nadai miaka kama 3 hiv, kuna siku nilikuwa natembea mtaani kuna mzee nafikiri alikuwa kilema amekaa anaomba msaada,nikampa kiasi kidogo cha pesa,Mida ya jioni nimekaa home nkashangaa pesa inaingia kwenye a/c kwa harak nkajua ni ule msaada niliotoa umesaidia kulipwa madai yangu
 
Bi mkubwa mshari,huwa tunasema kabla hujapanda Kama konda akicheka na Kila mtu mzima kipande hakitatimia,.pia hongera kwa kupata kazi..
 
65cb1ab82ed9421cb984f9d63b49252f.jpg
 
Leo nilikua nasafiri kuelekea Morogoro Wakati nipo kwenye gari ya Temeke-Mbezi (Dala Dala) konda akaanza kukusanya pesa kama kawaida yao .

Ghafla tukaanza kusikia malumbano

Sauti Kali ya konda ilisikika .

"Kwa Nini hukunambia mwanzo...

"We bibi mwanga nini

"Mapema yote hii
"Hujui iyo iyo100 Kubwa ,
"Usinitafutie matatizo naomba 100 yangu nauli haijatimia hii .

Maneno yote hayo alikua anaambiwa mama mtu mzima tena kachoka hasa .

Watu wote kwenye gari kimya, Bibi wa watu kainamia chini ,Sauti ya konda Kali ilitawala ndani ya Dala dala.

Nilijiuliza sh 100 huyu konda ndo yamtoke maneno yote, Ukingalia umri wa huyu abilia ni kama mama yake.

Konda huyu alikua na macho mekundu mithili ya pili pili iliyoiva, Mdomo wake ulikua mweusi tiii .
Roho iliniuma maana niliona kama mama yangu anaambiwa vile.

Nilitoa noti ya shilingi elfu 10 Kisha nikampa konda .

"Hiyo elfu 10 kata tsh 100 unayomdai huyo mama Kisha chenji inayobaki mpatie huyo mama.
Watu wote wakageuka nyuma maana niliongea kwa hisia sana .

Konda hakuongea tena, Hakuweza kunitazama usoni haya ilimshika, sura lake lilikua kama mgonjwa wa bawasiri akijisaidia haja kubwa chooni.

Yule mama kwa sauti ya chini iliyochanganyika na mfadhahiko huku macho yake yakilengwa na machozi kwa mbali akasema "ahsante mwanangu Mungu akubariki"

Gari lilifika mbezi mwisho nikashuka safari ikaanza kuelekea Morogoro.

Wakati nipo kwenye gari simu iliita namba ngeni ikinijulisha Kuwa maombi Yako ya kazi yamejibiwa hivyo angalia Katika Email Yako.

Nilishutka sana maana Miezi 3 sasa imepita tangu nitume maombi ya kazi CRDB BANK, kiukweli nilishakataga tamaa.

Email yangu inaonesha nimekubaliwa, Jumatatu inahitajika niwasili ofsni nikiwa na vyeti vyangu original.

Ilinibidi nishuke kituo cha Ruvu nikuludi nyumbani.

Morogoro nilikua naenda kwa Rafiki yangu Michael mtoto wa Mzee Makacha kumsalimia.

Nimejifunza kitu kupitia tukio hili.

Karma IPO, Utalomfanyia mtu nawe utafanyiwa either kwa direct or indirect hivyo tujikite kufanya mema .

Alafu, Kama jambo lipo ndani ya uwezo wako msaidie huyu mtu usiwe kikwazo
Niamini Mimi, Mungu yupo na atakulipa .
Mkuu, stori yako inasuza moyo sana; iwe ni kweli au ni ya kutunga.

Sasa fanya hivi mkuu: sote tutanufaika sana, na hasa watu kama huyo mama uliyempa msaada; ambao wapo wengi kwelikweli ndani ya nchi hii.Fanya lililo bora kwa taifa hili kuondokana na huu utawala usiojali hali za watu wa namna ya huyo mama.
Hata huyo Konda uliye mwona kutokuwa na roho ya ubinaadam, ni matokeo ya haya yanayofanyika chini ya uongozi mbovu tulio nao sasa hivi.

"NORNOE"

Ni HAKI yetu kuwachagua viongozi tunaowataka. (hata kama itakuwa ni hao waliopo madarakani sasa hivi; lakini tuwe na UHURU wa kuwachagua; tusilazimishwe.
 
Nimependa sana andiko lako, nasikitika kuwaona watanzania HASI zimewajaa Wengine Tunakupondea kufundisha wema ulio wima , unavyo simamisha vitu, nawengine tumesikia furaha kwa ushuhuda wako ,, nguvu za universe chanya husimamia mambo chanya, nguvu hasi husimamia nguvu hasi .

Mimi nimefurahi roho ulio ionesha kwenye andiko lako kutusimulia

Nguvu hizo hazionekani na macho
Ila huwa Zina jidhihilisha zenyewe

Ni kama hasira hazionekani Wala kushikika
Na furaha hazionekani Wala kushikika


HONGERA SANA.
 
Kuna mijitu ina laana sana ona mama wa @ Lucas Mwashambwa anavyodhalilika lakini lenyewe liko bize kumsifia mama abduli
 
Kuna mijitu ina laana sana ona mama wa @ Lucas Mwashambwa anavyodhalilika lakini lenyewe liko bize kumsifia mama wa mwenzake abduli
 
Back
Top Bottom