Msanii wa Bongo Fleva, Abdukiba, anatajwa kuingia kwenye mvutano na muuza chips wa mtaani baada ya kukumbushwa deni la zamani la shilingi elfu kumi, madai ambayo yameibua mjadala mpana mitandaoni.
Kwa mujibu wa muuza chips huyo, ugomvi ulianza baada ya kumkumbusha msanii huyo deni la chakula walichokuwa wakichukua hapo awali. Anadai kuwa waliwahi kuchukua chips na kuku yenye thamani ya shilingi elfu 15, ambapo Abdukiba alitoa shilingi elfu tano na kubaki na deni la shilingi elfu kumi, jambo lililodaiwa kumkera msanii huyo.
Inadaiwa kuwa mvutano huo uligeuka kuwa vurugu zilizosababisha kioo cha gari la Abdukiba kupasuliwa. Kufuatia tukio hilo, muuza chips anasema kaka yake ambaye ni mmiliki wa kibanda hicho alipelekwa polisi, na baadaye wakatakiwa kulipia fidia ya shilingi laki tatu kwa uharibifu wa kioo cha gari hilo. Hata hivyo, kutokana na kushindwa kupata kiasi hicho, waliishia kulipa shilingi laki mbili.
Muuza chips huyo anasisitiza kuwa kwa mtazamo wao, Abdukiba ndiye aliyekuwa na kosa, hivyo hawawezi kumsamehe fedha walizodai kulipa. Anadai kuwa hata siku msanii huyo akifariki, watahudhuria msiba wake wakiwa na shilingi elfu kumi ya deni la chips pamoja na shilingi laki mbili walizolipa kama fidia.
#nifollow Zone Tz
View attachment 3531594