Mugabe alipigania vita ya uhuru wa Zimbawe, alipigana na akashinda lakini uhuru huo haukugusia ardhi, ardhi ilibaki kuwa mali ya wazungu waliotuvamia hapa afrika bila visa wala passport.
Baada ya uhuru, alifatwa na wenzake waliomuunga juhudi kwenye kupigana vita ya uhuru wakamwambia kulikua na haja ipi ya kupigania uhuru kama ardhi inabaki kwa watu ambao waliwapora?
Kipindi hiki chote kabla hajaanza harakati za kuirudisha ardi kwa waafrika, wazungu walikuwa wakimpenda sana Mugabe kwasababu hakuwangilia kwenye umiliki wa ardhi waliyoipora.
Wazungu waligeuka mbogo na kuwa adui wa Mugabe pale walipoona Mugabe karudi upande wa kuwatetea wenzake wapate ardhi yao, hapo ndipo Marekani na Uingereza wakaanza kumwekea Mugabe vikwazo vingi sana na kumfanya aonekane mbaya.
Kwa upande wa Afrika Kusini mpaka leo wazungu wanamuenzi Mandela kwasababu Mandela aliwaruhusu kuendelea kumilki ardhi na Migodi, Karibu ailia 80 ya ardhi inamilikiwa na makaburu Afika kusini na Mandela aliruhusu hivi ndio maana wazungu walimsifia sana na kudanganya ulimwengu kwamba Mandela ndiekiongozi bora kuwahi kutokea Afrika.