Hii ni tabia mbaya nionavyo mimi, kwa mashoga na madogo wa mke

Hii ni tabia mbaya nionavyo mimi, kwa mashoga na madogo wa mke

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Nashangaa kitanda nacholalia iweje mke wangu ulale na dada yako, na wakati kuna chumba kingine, ati kisa mimi sipo?

Nashangaa bafu la chumbani wadogo zako wanalitumia na wakati unajua ni la wawili tu mimi na wewe na wakati huo kuna bafu tena la ndani hapo kwenye korido?

Nashangaa we dogo unajipodolea kwenye kipodoleo-meza cha wife wakati kule chumba chako uliko fikia kuna kipodoleo-meza cha wageni?

Agha! Haya yote hufanyika ninapokuwa lindo, shift ya usiku ama safari wakati mwingine ninapoondoka alfajiri ila asubuhi namwacha wife na mdogo wake wakati beki tatu ndio shahidi.


Haya sasa chumba changu kinafahamika na madogo wa mke wangu wakati mimi madogo zangu wakija hawagusi huko niwepo ama nisiwepo.

Hivi kweli unaeshimiwa we Braza

NB: mimi sio mhusika hapa nimeandika tu kuelimisha, na nimewahi shuhudia sana enzi zile....


Maybe tunaweza elimika kwa wale wanaoona mambo haya ni ya kawaida kumbe sio. Ngoja tuone.
Aiseh vichwa dagaa hawataelewa😀
 
Wewe kama baba na kichwa cha familia unashindwa kumueka chini mkeo na kumkanya huo ujinga wake??

heshima uipate jf wakati mkeo yupo chumbani hapo
 
Kwahiyo kati ya

1. Kumkalisha chini na kumkanya kiume na..
2. Kusimulia JamiiForum.. ndo' ukachagua namba mbili?

Mitano ya mwisho
 
hii sio mimi , mimi nimeleta ujumbe tu, kwa ambayo niliwahi shuhudia.😀😀
 
Kwahiyo kati ya

1. Kumkalisha chini na kumkanya kiume na..
2. Kusimulia JamiiForum.. ndo' ukachagua namba mbili?

Mitano ya mwisho
Sio mimi mkuu ni namna nilivyowasilisha na kushuhudia mambo hayo
 
wewe kama baba na kichwa cha familia unashindwa kumueka chini mkeo na kumkanya huo ujinga wake??

heshima uipate jf wakati mkeo yupo chumbani hapo
Sio mimi mkuu ni namna nilivyowasilisha na kushuhudia mambo hayo
 
Tuanze na wewe unayekaa na house girl kumteta mkeo! Wewe mwenyewe huna adabu kabisa. Na wewe ndio chanzo
 
Mkanye akikataa muombe mdogo wake awe anatumia chumba chenu pia na ukiwepo! Na ikiwezekana mlale wote watatu km ana akili atastuka
 
Back
Top Bottom