Hii njia ya Kenya, Uganda, Rwanda na mataifa mengine hasa ya Africa kupambana na Corona inachekesha

Kijitikile ngwale 2 reloading 😅....Yani this people never learn.
Usichokijua ni kwamba kinjikitile alikuwa genius na alifanikiwa 100℅ katika mapambano dhidi ya majeshi yenye silaha bora kabisa.. remember,aliwafanya watu wake wapambane bila kuzingatia udhaifu wao,nasi chini ya jiwe tutashinda tu .. keep watching
 
Reactions: Oii
Kenyatta ni mpumbavu,haelewi anafanya nini,ameshachanganyikiwa. .kuna maana gani kufungia watu usiku,huku mchana wakichangamana kama kawa. .. sasa usiku na mchana,ni muda upi watu huchangamana kwa kiasi kikubwa???.. sijawahi kuona mtu mpumbavu kama kenyatta
 
Itakuwa vile virus havifanyi kazi wakati wa mchana 😂😂😂
 
Jameni tuombe wazungu wagundue dawa mapema maana miafrika kwa jeuri tutakufa mpaka tufutike duniani.
Hawa wanaobeza, ipo siku watakosa hata hizo hela wanazopewa na CCM za kushinda mitandaoni.
Lifestyle yetu sisi waafrika ni tofauti sana na wazungu...nyie kenya hamna utofauti na mataifa mengine ya afrika,hilo ulielewa
Kama sisi tukifa,nyie hamuwezi kupona,hata mkijifungia ndani. ..mark my words
 
Tatizo lenu huwa mnapenda kuhamisha hoja
Hapa inazungumzwa hoja ingine,badala ya kushughulika nayo au kupita kimya,unapandika uzi unaojitegemea,hatujadili kima chini hapa
 
Kenya mmejipanga uwongo mbaya. Wasiomuelewa Uhuru ni sawa na wale wanaomlilia Gaddafi leo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufungia watu ndani sio suluhu

Haya Marekani naona amechukua uamuzi wa Magufuli, go to work but abide closely with precautions

Kuna vinchi vingine tayari uchumi wao upo ICU, lazima viende na hii Corona View attachment 1399779

Marekani si nchi, ni dubwana.

Ukiongelea nchi taja nchi tu. Marekani ni idea.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Reactions: Oii
Hawa kwa sasa muwazuie wakae huko kwenu, mvumilie atleast hizi siku ziishe, tumefunga mipaka, halafu mumefungiwa kote hata Uganda hamuendi maana huko ndiko mlikua mnatumia kupenya kuja Kenya...

Kupenya? Kwani boda yenu na Ug ipo wazi? Kuna chocho kibao za kuingilia Kenya from Tz kuliko Ug. Sasa mwehu atakaekwenda Ug kuzamia Kenya atakuwa ana akili kama zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naomba uelezee kidogo umemaanisha nini kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Marekani ni nchi 50 zimeungana pamoja (states) kila state ina gavana wake na inajimwambafy kivyake. Kila state ina serikali yake, sheria zake, mahakama zake, bunge lake. Halafu kuna serikali, mahakama, bunge la states zote, kama shirikisho.

Rais Trump kasema atafanya quarantine New York watu wasitoke. Gavana wa New York Andrew Cuomo kamwambia huwezi kufanya hivyo, kwanza ni kinyume cha sheria.

Trump mwenyewe kanywea.

Gavana wa Rhode Island kasema magari yenye plate numbers za New York yakishikwa yanapita state ya Rhode Island watu watakamatwa, Gavana wa New York kamwambia nitakushitaki ukiwakamata watu wa New York, kufanya hivyo ni kinyume na katiba.

Utaona nchi gavana anamkoromea rais, halafu rais ananywea mwenyewe.

Ndiyo maana nasema Marekani si kama nchi nyingine, idea ya uhuru na utawala wa sheria imetamalaki.

Tanzania Mkuu wa Mkoa anaweza kumkoromea Rais kwa sababu Rais kavunja sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…