Johann Krapf, Mjerumani, alianzisha Anglican Church, kanisa la Ufalme wa Uingereza?
Alikuwa Mjerumani na Mlutheri, lakini alitumwa Afrika na Shirika la misioni ya Kianglikana CMS. Wakati wake walikuwapo ambao hawakusisitiza udhehebu kuliko yale waliyoona kama "kujenga ufalme wa kristo".
Johann Ludwig Krapf (
11 Januari 1810 –
26 Novemba 1881) alikuwa
mmisionari wa kwanza wa
Uprotestanti nchini
Kenya katika
karne ya 19 akatunga
kamusi ya kwanza ya
lugha ya
Kiswahili.
...
Ethiopia 1837-1842
Mwaka
1836 alikutana na mwakilishi wa
Church Missionary Society (CMS) aliyemkaribisha kufanya kazi na CMS. Misioni ya Basel ilimpa ruhsa akapokea wito wa kwenda
Ethiopia. Krapf alianza mara moja kujiandaa akisoma
Ge’ez (lugha ya Kale ya Ethiopia) na
Kiamhari (lugha ya kisasa ya Wakristo katika nyanda za juu Ethiopia).
1837-1842 Krapf alifanya kazi ya umisionari huko Ethiopia. Mpango wa misioni ya CMS ilikuwa kuwaamsha Wakristo
Waorthodoksi kwa matumaini ya kwamba watakuwa wenyewe wamisionari bora kwa wenzao
Wapagani au
Waislamu.
Lakini Krapf hakuelewa vema
Ukristo wa kiorthodoksi wa
Waamhari. Alishindwa kuelewa maana ya
liturgia,
mila na
desturi nyingi. Hakuelewa hasa kwa nini Wakristo Waorthodoksi walisoma
Biblia katika lugha ya kale ya Ge’ez hata wasipoelewa lugha hiyo badala ya kutumia tafsiri ya Kiamahari aliyokuwa amefanya.
Hivyo Krapf alijisikia amevutwa zaidi na
Wagalla – hili ni jina la zamani za watu wanaojulikana leo kama
Waoromo au
Borana. Wagalla kwa jumla walikuwa wakifuata
dini zao za kiasili, athira za kiislamu zikianza kuonekana. Krapf alijifunza lugha yao alianza kutafsiri sehemu za
Agano Jipya katika Kigalla (
Kioromo).
Mwaka 1842 Krapf alipaswa kuondoka Ethiopia pamoja na wamisionari wengine wa Kiprotestanti, akiwa na ndoto ya kurudi na kufanya kazi kati ya Wagalla. Alikaa muda kidogo
Kairo (
Misri) akafunga ndoa,
bibiarusi alikuwa amemfuata kutoka Ujerumani.
Wakati ule kwake nyumbani Tübingen Chuo Kikuu kilikuwa kimefuata taarifa zake na 1842 kikampa cheo cha
udaktari (PhD) kwa ajili ya
utafiti wake katika lugha na
historia ya Ethiopia.
Afrika ya Mashariki 1844-1853
Ethiopia ilikuwa imefunga milango yake, hivyo Krapf aliwaza njia nyingine. Alikuwa amesikia ya kuwa Wagalla waliwahi kufika hadi
pwani za
Afrika ya Mashariki. Hivyo akasafiri hadi
Zanzibar kwa lengo la kuwafikia Wagalla kupitia eneo la
Kenya ya leo. Sultani
Seyyed Said alimpa ruhusa ya kuanzisha kituo cha misheni huko
Mombasa.
Mwaka
1844 Krapf alifika Mombasa akianza mara moja kujifunza Kiswahili pamoja na lugha ya wazalendo wa eneo la
Mijikenda. Huko
mke na
mtoto waliugua
malaria wakafa. Krapf alihamia
Rabai iliyoko katika vilima juu ya Mombasa penye
joto kidogo akaanzisha kituo cha
Rabai Mpya.
Mwaka
1846 mmisionari mwingine (
Johannes Rebmann) alikuja kufanya kazi pamoja naye. Huko Rabai Mpya Krapf alitunga kamusi na
sarufi ya kwanza ya Kiswahili.
Krapf na Rebmann walikuwa
Wazungu wa kwanza walioona milima yenye
theluji Afrika. Rebmann aliona
Kilimanjaro, Krapf aliona
Mlima wa Kenya. Taarifa zao zilipofika
Ulaya zilichekwa na wataalamu waliodai milima yenye theluji haiwezekani Afrika.
Krapf aliendelea kuwa na matatizo ya
afya akarudi Ujerumani mwaka
1853.
Urithi wake
Hadi kifo chake aliendelea kuboresha vitabu vyake kuhusu
utamaduni na lugha za mataifa mbalimbali ya Afrika. Kwa jumla aliandika kamusi au kutafsiri sehemu za Biblia katika lugha zifuatazo: Ge’ez, Kiamhari, Kioromo, Kiswahili, Ki-mijikenda,
Kikamba,
Kimasai.
Ludwig Krapf alitoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza
lugha ya Kiswahili kwani aliweza kutafsiri
Injili ya Luka na
ya Mathayo ,pia aliweza kuandika
sarufi ya Kiswahili inayohusu jamii ya
Wasambaa.
Nyumba yake huko New Rabai imekuwa
makumbusho chini ya Museums of Kenya. Jengo la
Ubalozi wa Kijerumani huko
Nairobi limepewa jina lake.
Krapf alikuwa Mlutheri, lakini Kanisa
Anglikana linamkumbuka kama mwanzilishi wa
madhehebu yake nchini
Kenya.
(soma yote:
Ludwig Krapf - Wikipedia, kamusi elezo huru )