April26
JF-Expert Member
- Jul 14, 2020
- 1,405
- 2,147
Wakuu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...... Kazi iendelee.
Leo nahitaji ku-share matukio mhimu katika maisha yangu hasa yaliyo tokea tarehe 26/4 (April26) kwa vipindi tofauti tofauti.
Tukio la kwanza hii ndiyo tarehe niliyo letwa duniani (birth day) lakini nje na kuzaliwa.
Hii ndiyo tarehe ambayo mwaka fulani nikiwa mdogo niliugua ugonjwa uliowachanganya sana wazazi wangu nashukuru nilipona.
Hii ndiyo tarehe ambayo nilipata ajari tukiwa kwenye gari wakati tukifanya test baada ya matengenezo,gari ilimshinda fundi (dereva) na kwenda kugonga kichuguu kilichokuwa pembeni ya barabara nashukuru tulipona wote,shida ilikuwa mwendo kasi.
Hii ndiyo tarehe ambayo usiku wake wa April 25 mwaka 2008 kuamkia April 26 nilizinguana na mhindi tukiwa shift ya usiku kiwanda cha nguo huko Mwanza nikampiga nikaacha na kazi niliondoka akiwa anatokwa damu puani na mdomoni.
Hii ndiyo tarehe ambayo wakati napata mahusiano yangu ya kwanza kabisa yalikuja kuvunjika April 26 ni baada ya kuwa nimepumzika home nilipokuwa nimepanga mchumba wangu akanikuta na rafiki yake ambae alikuwa amepitia pale akiulizia rafiki yake yaani mchumba wangu akidhani angemkuta pale, mchumba wangu alidhani nimetembea na rafiki yake. Walikuwa wanajuana vijitabia.
Hii ndiyo tarehe ambayo nilibatizwa na kuwa mkristo ilikuwa 26/4 mwaka 2015.
Lakini pia hii ndiyo tarehe ambayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana kutengeneza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo ni baadhi makubwa nayokumbuka lakini hii tarehe imekuwa ya ajabu sana kwangu.
Naipenda hii siku kwa kuwa hata ikiangukia tarehe za kazi yaani j3 -Ijumaa huwa napata fursa ya kupumzika na kuitafakari safari yangu ya maisha.
NB; Nashukuru sana Mungu amenilinda na kunisimamia japo jambo la kushangaza ni kuwa hii tarehe 26/4 yamekuwa yakitokea matukio ambayo naona kabisa sio mazuri kuliko navoipenda siku yenyewe. Nina imani kubwa Mungu anakusudi lake now niko 30+ years. Najiona mwenye mafanikio yaliyo ndani ya uwezo wangu. Nina afya njema. Amina.
Mwenye wazo na ujuzi kuhusu matukio ya kufatana na tarehe/siku/majira naomba kujuzwa tafadhari.