Hii system ya kwenda kusoma chuoni, huenda itakuja ku-collapse siku moja

Uzuri kwa wenzetu ajira zipo. Mtu anamaliza high school anaenda kozi fupi mfano real estate agent miezi sita tu au unesi au mambo ya kodi, akitoka hapo ajira straight forward. Hii bora kuliko kupoteza muda chuo miaka minne halafu unabakia na madeni kibao experience zero.

Mtoa mada una point kubwa na kuna article nilikuwa nasoma jinsi mikopo ya chuo inavyowarudisha nyuma vijana kimaendeleo nchini marekani.

Wale wanaoamua kusoma chuo kwa kutegemea mikopo ni shida. Marekani mikopo ya wanafunzi ni janga kubwa sana. Yani mtu kama huna uwezo wa kulipa cash kusoma chuo au kupata scholarship ni bora kufanya kozi fupi ujilipie kisha uajiliwe moja kwa moja au ujiajiri
 
Point. Umeupiga mwingi!
 
Kwanza tuanzie hapa, " mental conditioning" ndio nini?! Elimu si kwa ajili ya kuajiriwa , ni kwa ajili ya wewe kujitambua na kuijua vizuri Dunia.Ukielimika vizuri basi Dunia itakupa kila kitu unachohitaji kutoka kwake!
Marekani wengi hawapendi kukaa chuoni kama kuku wa kisasa wafugwao! Huo mfumo technolojia inaupiga teke! Dunia ya leo watu wanasoma online via internet.
Unataka kwenda kukaa Chuo (Boarding) na umalize kukariri madesa yako uajiriwe! Hiyo Dunia uliyonayo kichwani si hii tunayokwenda nayo!
 
Kama kuna kaukweli fulani katika uzi huu
 
Kama kila mtu baada ya sekondari school ataingia kitaa kujiajiri maana yake baada miaka kadhaa hakutakuwa na hata walimu mwisho wa siku hata hizo shule hazitakuwepo, hospitali hakutakuwa na madaktari, wauguzi nk
Tutarudi kwenye ujima
Upo sahihi mkuu.
 
Pole sana !!! Unaidharai lak 9!?? Walahi mungu atakunyooosha haya kazi LA 150000/ per month utaisikia kwa wenzi

Wewe seniweba itakua umemaliza udsm, njoo hapa jF baada ya miaka 3 ndo uje utetee huu utopolo ulioandika leo Seniweba
 
Kinanishangaza wale wavumbuzi watechnolojia wa ulaya hawasoma elimu za juu kiviile, wengi ni o-level na high school.. wamarekani wengi hawafiki chuo kikuu
 
Aiseeeee
 
Elimu unayosoma leo, inazaidi ya miaka 30, yaani baba yako aliosoma kitabu hichi hicho unachosomea leo udactari. Hakuna mabadiliko


Kila kitu kimebadilika kaka, elimu ya sasa inahitaji mabadiliko makubwa mno tena sana, na yenyewe inaonyesha kama inademand kitu


Kinacho wauma vijana, mpka wanafananish hii elimu na toilet paper ni kwamba haina maslahi, kijana anataka akimaliza chuo aanze kujitegemea, leo hii unamwambia ajiari, atajiajiri vip mtaji hana na ametoka familia ya kimasikin. Ndo yale ya kurudi nyumbani

Isitoshe hii elimu siasa imeingia ndan, leo mwanasiasa anapiga hela sana kushinda hata professor, sasa unakuta mtaalamu huyo anaona bora siasa na anacha research na yy anaingia kwenye sias, kwahio ni full tafran
 
Well explained.
 

Umeelezea vizuri mno mkuu.
Sisi watoto wa mama SSH sijui tunakwama wapi
 
Kuelimika vizuri ni lazima ufike chuo kikuu? Binafsi naona elimu ya form 4 is more than enough kwa mtu ambaye alikuwa mtu wa kuzingatia masomo toka UPE na aka absorb 90% ya mafundisho na kuyaelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…