Hii taarifa ya Tunduru kuwa lazima uchanjwe ndio upatiwe pesa za TASAFU ni kweli?

Hii taarifa ya Tunduru kuwa lazima uchanjwe ndio upatiwe pesa za TASAFU ni kweli?

LUPEM

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2020
Posts
426
Reaction score
638
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wapokeaji wa pesa za TASAFU, wameambiwa kuwa ,lazima wachanjwe ,ndio wapokee pesa za TASAFU.Na kama watakataa kuchanjwa, basi hawatapewa pesa hizo.

Kwa hali hiyo, wananchi hao wametakiwa kuchanja kwanza ndio, waende kupokea pesa. Yaani unachanjwa kwanza, ndio unaelekea kwenye chumba cha pesa. Kama hautaki, unatakiwa kuondoka. Je, hii ndio chanjo ni hiari?
 
S anatutesa kala pesa za mabeberu sasa kuchoma lazima..taratibu tu itakua lazima nchi nzima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hii dhambi Samia itamtafuna sana na hatokuwa na mwisho mzuri wa utawala wake.
Kushauri watu kuchanja ni dhambi? Rais ameshasema kuchanja ni hiari, hao wengine ni watafuta kiki tu waonekane wamechanja watu wengi kwenye maeneo yao!! Lakini vilevile hii habari ina ukweli kiasi gani? Maana siku hizi kila mtu anaweza kujianzishia tu mada yeyote, Mf. kuna watu waliandika humu Samia kaenda US na ATCL, which ulikuwa ni uongo 100%
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wapokeaji wa pesa za TASAFU, wameambiwa kuwa ,lazima wachanjwe ,ndio wapokee pesa za TASAFU.Na kama watakataa kuchanjwa, basi hawatapewa pesa hizo.

Kwa hali hiyo, wananchi hao wametakiwa kuchanja kwanza ndio, waende kupokea pesa. Yaani unachanjwa kwanza, ndio unaelekea kwenye chumba cha pesa. Kama hautaki, unatakiwa kuondoka. Je, hii ndio chanjo ni hiari?
Kama ni kweli,wanakosea.
TASAF=Tanzania Social Action Fund.
U=?
😝😝😝😝
 
Mithali sura ya 14 na aya ya 31.
Kwamba maskini hana uhiari wa kuamua juu ya mwili wake linapo kuja suala la chanjo. Wajue pasi shaka yeyote wanamsuta Muumba wao ambaye amewafanya hao wategemea fedha ya TASAF.
 
Utaratibu unaotakiwa ni kwamba ukijitolea kwenye majaribio ya chanjo unalipwa fidia. Sasa kwa hapa bongo sijaona fidia yoyote ikilipwa na matamko yanavyotolewa ni kana kwamba watu wanalazimishwa, kama tulivyosikia juzi kwa watumishi wa serikali. Hofu yangu ni kwamba hii pesa ambayo watafiti wanatakiwa kutoa kwa ajili ya kulipa fidia iko wapi? hiiiiii bhagosha......
 
Hao wanufaika wasikubali kuchanjwa mana hata bila ya hizo hela za TASAF bado Mungu wao hatawaacha Bali atawatengenezea njia nyingine ya kuishi. Chanjo ni hiari aliye tayari achanje.
 
Dalili zilianza kujionyesha mapema kabisa kwamba yale yalikuwa ni maneno ya kisiasa tuu, lakini ukweli ni kwamba swala la chanjo ni la lazima. Na ni lazima kwa sababu tunalazimishwa na wazungu kwa sababu pia tunahitaji msaada wao.
Lakini tuliambiwa we are a donnor country, na watawala waliopo waka nod kuonyesha ni kweli
 
Waka "nod"?😝😝😝😝
What is the same meaning of nodded?


to make a slight, quick downward bending forward of the head, as in assent, greeting, or command. ... to bend (the head) in a short, quick downward movement, as of assent or greeting. to express or signify by such a movement of the head: to nod approval; to nod agreement. to summon, bring, or send by a nod of the head.
 
Back
Top Bottom