Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Ha ha ha.... wewe nimekukubali sana huna kuremba kabisa.
 
Ni upumbavu kudhani unachowaza wewe na wengine wanawaza.. simu ni yangu mtu akinisumbua its either na mblock au nazima nipumzike. Acheni kuja kujipendekeza kwa mashemeji zenu. Mnatusumbua sana nyie wa bush.
Nani wa bush mzee? Mbona una makasiriko, sisi tunaangalia namna mambo yanavyoenda katika jamii, katika kesi nyingi Hali inakua hivo. Na kiuhalisia ukiona una mind vitu Kama ndugu zako wa bush kukupigia simu kuomba msaada, wewe mwenyewe uchumi wako mdogo. Una mansion au villa umejenga na nyumba ndogo ya nje hauwezi kuhangaika na vitu vidogo Kama mtu kula sijui kulala, wewe bado haujajipata ndomaana una makasiriko.
 
Matusi ya nini? Kwani hutaeleweka bila matusi? Mwinjaka nini?
 
Ubinadam kazi. Nimalizie kwa maneno hayo.
 
Tutafute hela wazee, sisi tukienda home mbona huwa tunabeba familia nzima tunabatiza safari kuwa tunaenda RIKIZOπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Umeona mzee bush wabeba gharama zetu za familia nzima tukiwa kule wanatupa huduma nzuri sometimes wanakopa, ndo mtu mmoja kutoka huko umzimie simu, πŸ˜‚πŸ˜‚ ni umaskini tuu
 
Umeona mzee bush wabeba gharama zetu za familia nzima tukiwa kule wanatupa huduma nzuri sometimes wanakopa, ndo mtu mmoja kutoka huko umzimie simu, [emoji23][emoji23] ni umaskini tuu

Maisha ni magumu ndio vyakula vimepanda bei
Kuna watu ni matajiri wana nafasi na hawataki wageni [emoji23][emoji23][emoji23] kila mtu akae kwao[emoji23][emoji23]
 
Na Mara nyingi sana watu waliotelekezwa wamesaidiwa msikitini, hili nimeliona Mara nyingi.
 
Maisha ni magumu ndio vyakula vimepanda bei
Kuna watu ni matajiri wana nafasi na hawataki wageni [emoji23][emoji23][emoji23] kila mtu akae kwao[emoji23][emoji23]
Wageni ni baraka, changamoto zipo lakini upendo na kuelekezana kiungwana ni jambo zuri zaidi, haijarishi we ni tajiri au maskini kuwa mkarimu na mtoaji ni moyo tu wa mtu. Ukiwa mkarimu unapata thawabu kwa mwenyezi mungu
 
Siku watakapoamua kukusafirisha hao ndio wachimba kaburi wagawa chakula kwenye msiba wako be humble brother..
Watu tunajisahaulisha haraka mno au pengine hatufikiri sawasawa, maisha ya Afrika Ni undugu,likikupata ndugu zako ndio wataokubeba
Huku Hakuna funeral companies kwamba ukifa itaenda lipia gharama uzikwe ,Ni Hao ndugu zetu tunaowanyanyapaa ndio wachimba kaburi
Ikitokea umeumwa Ni Hao Hao ndugu ndio watakua wauguzi
Indeed we need to be humble, mengine Ni umaskini kama walivyosema wachangiaji wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…