Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Ndiyo hivyo,maana sijaona kitu kinawapa ubize zaidi ya usafiri[emoji23],

Na imagine na hii mvua wanaishije[emoji23],

Nyie dar mateso sana,
 
Kwangu hakuna nafasi kwa sasa ya kutunza mgeni hatakama nafasi ipo utatumia lugha ya kiutu.

Hivo utakaa hizi cku 3 kwa shida ili tutafute nauli urudi au kama una nauli ya kurudi itabidi urudi siku fulani.
Dah!! Yani mtu/Ndgu wa kijijini aje kwako alafu umwambie hivyo?? Hata kama ulimpa hifadhi ya mwezi mzima ila kitendo Cha kumwambia hivyo tu umeharibu. Ataondoka sawa lkn maneno utakayo yakuta huko kijijini siku ikienda hutoamini macho Yako.
 
Wabush povu linakutoka. Nimeshafanya sasa unasemaje? Na nimefanya nilivyo fanya
 
Sisi wengine wakati wadogo Mara nyingi tulikuwa tunapokea ndugu, unaambiwa huyu ni mjomba, Dada, shangazi, Kaka na wengineo. Wanasomea pale, wanapata kazi na wengine wanaolewa kutokea pale. Wanaoongoza kukataa ndugu ni wale waliopitia kwa ndugu kwani baada ya kupata kazi na kujitegemea wanaona majukumu yao ni kwa mke na watoto wake anasahau alipotokea.
 
Tafuta hela ndugu ili utamani kula na ndugu zako wakati wote... haya malalamiko yako ni ishara ya umaskini
 
Hii ni dalili za maisha magumu sana. Mungu akunusuru, maana kulala na kula sio kitu cha kumzimia mtu simu.
Masikini ndio wanaendekeza kuja kwa watu bila taarifa. Matajiri kwanza hawana huo muda wa kutembeleana hovyo majumbani. Hakuna watu wenye bajeti kali kama matajiri, kwanza lazima utoe taarifa mapema .a sio kwenda kukaa tu kwake bila plan.
 
Mfano,
Una eneo kubwa (nyumba) una chakula Cha kutosha una kipato cha kati (shida ndogo ndogo hazikupigi chenga)

Sioni ubaya wa ndugu jamaa na marafik kuja kutembea kwako dats Kuna watu wamejenga nyumba ya kufikia wageni kuondoa muingiliano na choko choko za familia yake na wageni..

Ukiona mtu analalamika jua ni masikini wa akili na hali
 
Watu wanajisahau sana
Nawakumbusha , tomorrow is mystery hakuna aijuae!

Unaowadharau sahivi ipo siku utawahitaji na hutawapata!
Maisha mzunguko
Cha mhimu mtu atoe taarifa kwanza Kwa mhusika na kuwe na sbb inayomfanya aje!
Hakuna mtu anadharau mtu anayejiheshimu na kuheshimu wengine. Kuna ndugu unatamani wawe wanakuja kukutembelea mara kwa mara. Sitaki mtu akae kwangu halafu asambaze majungu kwa watu. Mimi naishi na watoto wa dada na kaka, hapa ni kufuata masharti ya nyumbani kwangu. Nikisikia majungu kwa ndugu na jamaa na nikahakikisha umeyapeleka wewe utaenda kuishi nao.
 
Ss hiyo kesi nyingine
Mtu akija kuishi kwako lazima afuate Sheria za hapo kwako!
 
Kuna kipindi ndugu wa mke wangu walikua wengi mno home, nikiwa kijana mdogo kabisa ndio tunaanza maisha na wife.

Sijui walijua Mimi ni "Jesus" naweza walisha wote kwa kuombea tu Chakula kiji multiply.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…