Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii mada nzito sana[emoji23] mimi nishazimiwa sm mara kibao tu enzi hizo ila siwez mzimia now mtu sm labda sababu na uwezo wa kumpa malazi na chakula bila kupungukiwa
Yawezekana wanaokwepa mambo yao hayajakaa vzr so anashindwa kuwa wazi but kama una nafasi usimzimie mtu sm mpokee then akitulia mweleze situation ataelewa ataondoka kwa amani na hatakuwazia mabaya
 
Watu tunajisahaulisha haraka mno au pengine hatufikiri sawasawa, maisha ya Afrika Ni undugu,likikupata ndugu zako ndio wataokubeba
Huku Hakuna funeral companies kwamba ukifa itaenda lipia gharama uzikwe ,Ni Hao ndugu zetu tunaowanyanyapaa ndio wachimba kaburi
Ikitokea umeumwa Ni Hao Hao ndugu ndio watakua wauguzi
Indeed we need to be humble, mengine Ni umaskini kama walivyosema wachangiaji wengi
That's true.. unayemkataa anageuka kuwa msaada.
 
Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.
Kitu cha kwanza katika maisha yangu ni ndugu zangu, pamoja na familiar yangu.

Mwanamke wangu anatakiwa awapende ndugu zangu kama mimi ninavyowapenda ndugu zake,na kama hataki basi akwende kwao.

Siku ukiwa na matatizo makubwa ni ndugu zako ndo watatafutwa na ndo watakao uhifadhi mwili wako.
 
Jamaa mbona una hasira dhidi ya ndugu zako, wallikufanya nini mpaka unawaitia Mijitu?

Mkuu Jaribu kuwa Mnyenyekevu basi.

Hao unaowadharau ipo siku utawakumbuka na hutawaona.

Kama huwezi kumsaidia mtu basi achana naye ila usimpe majina mabaya eti Mijitu.....Itakuwa wewe Kweli Umeolewa maana hizo hasira tu sio kidogo.
Hahahaaa naona unamtafuta
 
Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za simu za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu wa Dar mnachekesha sana
Mkija mikoni mara zote mnajisabu karibuni Dar ndg zangu tutembeleane sie tuko huko wewe ukija maswala ya nauli ya kurudi niachie Mimi maneno mengi ya kiswahili na kitapeli mtupu... mwisho mnatuachia na no Zenu za simu. Mtu analima mpunga wake anauza gunia2 ananunua nguo mpya na nauli anabakiza Ili aje matokeo yake unamzimia simu kisa hajakupa taarifa Sasa ulimkaribisha wa Nini ukiwa kwake Kijijini kwann usimchukue umwambie mara nyingine ukitaka kuja toa taarifa.

Watu wa mjini kumbukeni mnapokuwa mikoani ndg Zenu wanawajali sana kunavyombo vimenunuliwa special Kwa ajiri yenu hata baba wa familia hajawahaaai tengewe kumbukeni ninyi ndo Huwa mnakula majogoo na mbuzi wakubwa huko kijijn Tena kuku kienyeji pure achana na broiler wenu. Ninyi ndio Kila kitu mnasifia Cha Kijijin mara hii mihogo mizuri mitamu Ina unga ..maembe haya mazuri Sana Nina miaka kadhaa sijala embe tamu kama hili. Mkiaga hamkatai kubebeshwa mpunga,karanga au mahindi Ili Hali wewe ulikuja n mikate na sikonzi 3 tu garama ya ya3500.

Acheni roho mbaya
Mkuu umeongea kwa uchungu sana ni kweli wanaendaga na mkate na sukari kilo moja lakini mwishowe wanapewa gunia limejaa nafaka na jogoo wa kwenda kula na wanawe.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Masikini ndio wanaendekeza kuja kwa watu bila taarifa. Matajiri kwanza hawana huo muda wa kutembeleana hovyo majumbani. Hakuna watu wenye bajeti kali kama matajiri, kwanza lazima utoe taarifa mapema .a sio kwenda kukaa tu kwake bila plan.
Ukiona mtu ni mchoyo kwenye chakula na malazi kwa mtu,tena wanaofahamiana na anafikia kiasi ambacho anazima hadi simu kabisa ujue huyo ni tajiri kwa nje lakini kiundani ni mwenye uchumi uliojaa madeni na hali ngumu.
 
Hii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.

Mi nipo zangu home jana inaingia simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.

Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.

Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.

Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.

Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.




Mimi walienda kusema nafuja sana pesa badala ya kuwasomesha watoto wao. Mtu kazaa watoto 13 anataka nimsomeshee... Mimi nina 3 tu. Bado wanaenda kusema nakuaje na watoto wachache ... Mwanaume gani. Mke amenikalia kichwani anarudi jioni kama mwanaume. Wanataka wife awafulie nguo zao. Na wanakuwa wakali akirudi awapatie chakula n.k sina hamu na ndugu kabisa.

Mmoja tumekaa naye mwaka mmoja amekuja nimsomeshe diploma. Akirudi toka chuo anaangalia TV mpaka saa 4 akipewa kazi basi za home siku yupo asaidie... Anasema anateswa sana hawezi soma. Nikasubiri likizo. Akaenda kwao kusalimia. Nikamwambia atafute chuo aendelee kusoma huko, nitamlipia ada.

Alilia sana anataka arudi Dar. Nilimwambia huku wifi yako atakutesa hutapata muda wa kusoma. Akabembeleza sana nilimkatalia coz alishanipakaza sana kijijini na kumchafua sana wife. Na mtu mwenyewe ni ndugu wa mbali kabisa..

HAWA WAGENI WENGINE NDO HUNAJISI WATOTO NA UNDUGU UNAISHIA HAPO HAPO. MNAHARIBIANA FUTURE. KILA MTU AKAE KWAKE. DUNIA YA SASA IMANI IMEKWISHA. TUSAIDIANE KATIKA SHIDA LAKINI SI KUVAMIANA TU NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA UKARIMU. NDUGU WENYEWE IMANI IMEWATOKA. ANGALIA WANAOBAKWA, NAJISIWA AU LAWITIWA. MHUSIKA UTAKUTA BABA, BAMDOGO, MJOMBA, COUSIN NA JIRANI KWA MBALI KIDOGO.
Hivi kwenye miaka hii bado mtu anaweza kutoka tu huko kijijini na kuja mjini BILA SABABU na kuamua tu kuwa nitaenda kukaa kwa NDUGU (Baba mdogo, mkubwa, Shangazi, Dada, Kaka, Bibi, Babu nk????!!
 
Hivi kwenye miaka hii bado mtu anaweza kutoka tu huko kijijini na kuja mjini BILA SABABU na kuamua tu kuwa nitaenda kukaa kwa NDUGU (Baba mdogo, mkubwa, Shangazi, Dada, Kaka, Bibi, Babu nk????!!
Tunakuja kuosha macho
Tuacheni[emoji23][emoji23][emoji23]

Kila mtu ana ndoto za kufika Dar.



Nadhani shida siyo chakula..
Shida ni taarifa.
 
Back
Top Bottom