Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Yalinikuta Jumapili alikuja mtu wa aina hiyohiyo nyumbani tofauti ni kuwa huyu aliletwa na ndugu yangu, alichonikera ni vile alipofikishwa tu akawa na kidaftari chake ameandika namba za simu za watu wake anaojua wapo Dar, akaomba simu yangu na kuanza kuwapigia mmoja hadi mwingine mbaya zaidi akawa anawaambia uongo kuwa yupo ameekaa kwangu kwa zaidi ya mwezi, kilichonikwaza zaidi siku iliyofuata nimerudi toka mihangaiko yangu jioni nakuta sebule imejaa hao rafiki zake kama kuna kikao cha kikoba wamechukua vinywaji kwa jirani bila kunishirikisha bill ipo kwangu.
Unafukuza wote, tusiendekeze ujinga
 
Kiukweli kwa maisha tuliyo nayo sasa inapendeza mgeni akija aje kwa taarifa.

Ni asiyeelewa tu namna dunia imefikia wapi kwa sasa ndo ataona ye mgeni akija tu kwake bila taarifa ni sawa.

Hawa hawa tunaowaamini wengi wamekuwa mwiba kwa baadhi ya familia hasa baada ya kuja bila kuwa na vya msingi vilivyowaleta.
Kwani hao wageni wao hawana kazi ya kufanya hadi wadhurure miji ya watu?
 
Salamu mtu anapaswa aje kwa wakati maalumu, aje na matumizi yake.
Kwani hana kazi hadi aanze salimia watu?
Hivi kumbe kuna wakati maalumu wa kumsalimia ndugu[emoji3061].Watu wengi tunajisahau sana hasa tukipata vijisenti akija ndugu unaona km anakuwekea kiwingu msumbufu mmoja ila umesahau kwamba huyo unae mdharau hujui keaho yake.Mkuu yakija kukukuta utakuta mtu anayekuja kukusaidia ndo ulie kua unamuona kero ama mpuuzi.
 
Mentality ya kimasikini hii na kuendekeza ujinga na upumbavu
Umaskini upi? Kuwa mnyenyekevu ndio umaskini?

Umaskini ni ile dhana ya kudhani mtu akikutembelea anakuna kumaliza bajeti yako.

Huo ndio typical umaskini.
 
Hivi kumbe kuna wakati maalumu wa kumsalimia ndugu[emoji3061].Watu wengi tunajisahau sana hasa tukipata vijisenti akija ndugu unaona km anakuwekea kiwingu msumbufu mmoja ila umesahau kwamba huyo unae mdharau hujui keaho yake.Mkuu yakija kukukuta utakuta mtu anayekuja kukusaidia ndo ulie kua unamuona kero ama mpuuzi.
Watu maskini wakipata aisee ni hatari
 
Nasikia wasukuma wana hizi tabia[emoji23]
Mke wa kaka yao awafulie nguo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2772]
Akiyanani,
Nifue nguo za mume,
Za watoto,
Nifue na za mashemeji??
Hii sio sawa.

Mi mke Wangu hata nguo zangu na watoto hafui Kwa mkono, nimemnunulia mashine
 
Si bora hata hiyo sebule ipo. Wengine tunakaa self... [emoji1787][emoji1787]

Mara ba demu anaweka weka kambi mara siku 3 mara siku 1 mara wiki.

Na mwingine yupo standa...

Jamani tupeane taarifa hata 1wk before
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbaya zaidi MTU akishakaa kwako siku akiondoka huko anakofikia Ni kumsema mkeo vibaya.

Mara jamaa kaolewa maana yule mke Ni mvivu. Mke mchoyo, mke anadharau n.k

Kumbukeni mke wangu Ni pambo la nyumba yangu, sio MTU wa kusonga ugali kwa ajili ya mijitu ya kijijini.

Mke wangu ashindwe kunilisha vipaja vya kuku kisa Kuna mgeni au mke wangu asiwe na Uhuru wa kujiachia nyumbani kwake kisa mgeni!

Kwendreni huko.
Neno kwendeni huko ndilo nimelikalili 😂😂🤣
 
Kipindi nipo country (kijijini) nateseka na kilimo cha ufuta Kuna mjinga mmoja nilimpa chumba changu aishi baada ya kupata matatizo yake baada ya kurud nilicho kikuta sikuamini kurikuwa na kunguni mapanya kama yote mwisho wa siku nikamtimua na mpaka leo Sina hata shobo nae kwa ufupi najuta kwanini nilimpa chumba changu sometimes ndugu sio
 
Back
Top Bottom