Hii tabia ni mbaya sana kwa baadhi ya wanaume wa JamiiForums. Kupewa namba sio lazima

Hii tabia ni mbaya sana kwa baadhi ya wanaume wa JamiiForums. Kupewa namba sio lazima

😂😂😂Eeeeh hapo kwenye mwandiko nilisema huyu angalau ananyoosha ila akili zao zimefanana sana bwana....ngoja nimtafute da mau kwenye comment 😂😂
Umekosea mkuu
 
We mtu anakwambia muda wote gari limewaka anataka kupelekewa moto kwa nini vijukuu vya Pharaoh visiombe number😂😂😂
😄😄😄alikuwa anabip kapigiwa anapiga mayowe
 
🤣🤣🤣🤣 kwaiyo nina swagger za mbali za ki da Mau… halafu unaeza kuta huyo da mau ni kabibi flan hivi ka sisiemu
Hata sasa mana muda wote analalamika wanaume wanamroga 😹😹😹
Mara ataibuka analalamika hawampi pesa wanapiga free P
 
Kwanza kabisaa usiamini story zote humu utakuwa mjinga sana humu kuamini kila story na kuanza kumdefine mtu kulingana na story alioleta… visa vingi ni uongo uongo

Hii tabia imekuwa kero sana kwa watu wa humu jf (wanaume),, lengo la kutumia ID fake ni ili mtu alete kisa chake na majanga yanayo msibu bila kutambulika na yoyote yaani mtu anakuwa huru kutoa ya moyoni mwake

Wakati mwinginee pia hivi visa havina uhalisia ni kuchangamsha genge la JF na mtoa story kupunguza stress anapoingia humu

Sasa nashindwa kuwaelewa wale wanakimbilia PM kuomba namba tena kwa ulazima… mtu unakuta unamwambia nishauri humuhumu ila anabaki kukulazimisha utoe namba.. huwa nawashangaa mnataka cha ziada nini… tutoe namba zetu humu ili identity zenu zijulikane na wengine mlivyo wa hivyo muje mututangaze humu

Mimi niliacha hadi kutumia ID yangu ya zamani kwasababu kuna baadhi ya watu nilikosea sana nikawapa namba yangu na tumekuwa marafiki na story nazozileta humu hazifanani na uhalisia wa maisha wangu kwa mitazamo yao so ikawa ngumu mimi kuandika visa vyangu kwa ID yangu ikabidi nitengeneze ID mpya

Mwinginee anakuja PM anakwambia ameona Mimi nafaa kuwa mke wake mpk unaanza kujiuliza huyu ana wazimu hatujuani sikujui na huna uhakika kama hii ID ni ke o me ila umekazana kusema tunaendana huwa mnakuwa na wendawazimu kichwani mwenu

Kama mtu kaomba ushaurii hajasema kuwa anahitaji kutoa mawasiliano yake na hajapost kutafuta mume au mke kwenye jukwaa la Love connect muache jamani kutusumbua

Wengine hatuwezi kuzifunga hizo pm kwasababu kuna baadhi ya member wanashindwa kuchangia mada labda for their reasons wanaamua kuja pm ili kutoa ushaurii

Mawasiliano hayalazimishwi jamani kama nimeomba ushaurii unaweza kunishauri bila Kutaka namba yangu.. kama ningehitaji kujulikana basi platform ni nyingi na wana saikolojia ni wengi ningeenda huko kuomba ushaurii

Nipo jf kuomba ushaurii wowote kwasababu ni sehemu ambayo ninajisikia comfortable kueleza chochote bila kujulikana na yoyote humu

Haya ninayasema kwasababu kuna members wamekuwa wakinishambulia PM kwa maneno mabaya kisa tu nimekataa kutoa namba yangu… jambo ambalo limeniudhi.. kama mtu kisa namba anaweza kunitolea maneno machafu hata nikimpa namba yangu hashindwi kuja kuni expose humu

Tuheshimiane humu.. hizi story za humu zinaishiaga humu na story zingine nyingi humu ni Chai tu hazina uhalisia… sasa wewe kujifanya una ushaurii sana mpk kulazimisha namba na ukinyimwa unaleta matusi hebu huo ushaurii jishauri mwenyewe labda utakusaidiaa

Weekend njema
Sindano hii iwachome daadeki
 
Kwenye profile ya mhusika mfano hapa kwenye id yangu bonyeza yatatokea maneno follow ignore, start conversation so wa kumuignore unaclick ignore unakua ushamaliza kazi
Ignore list unabonyeza wapi mkuu??
 
Kuna member alianzisha uzi juzi kati akiomba namna ya kukwepa zawadi sijui na blah blah kama hizo nikamuuliza kama alishawahi kusikia neno SITAKI

Na wewe kama hujawahi kusikia neno SITAKI basi nakuelekeza....maana yake ni kukataa,litumie hilo huko PM,litakusaidia
Na kuna wimbo Diamond kaimba kabisa
 
Kwenye profile ya mhusika mfano hapa kwenye id yangu bonyeza yatatokea maneno follow ignore, start conversation so wa kumuignore unaclick ignore unakua ushamaliza kazi
Ok asante
 
😹🤣🤣 nimeamka kukojoa comment yako imenifanya nicheke mpk machozi..!!

Watu na ma sponsor wenu 🤣
aaaah wawaache wapumue sasa😂😂
 
Sasa ulikosea pakubwa
Ila kwanza watu ni jasiri sana sijui ama ni matamaa,unawezaje kumtaka ambaye hata hujawahi ona sura yake,
Anyway ungempanga jamaa mmoja unawapa namba yake,simple kama ataka kuchezea rungu aendelee kukutafuta
 
Back
Top Bottom