Hii tabia ya Wanasiasa kujibishana na polisi isiachwe iote mizizi. Alianza Malima, Kigwangalla, Nape, Lissu na sasa Mbowe

Hii tabia ya Wanasiasa kujibishana na polisi isiachwe iote mizizi. Alianza Malima, Kigwangalla, Nape, Lissu na sasa Mbowe

Mmewatumia polisi mpaka wamesahau wajibu wao, sasa hivi wanajigeuza wanasiasa waziwazi. Bila machafuko yatakayopelekea kubadilisha mifumo ya utawala, sheria zitazidi kusiginwa na waliopewa majukumu ya kusimamia utekelezaji wa sheria.
 
Polisi anakuwa kama mgombea anamwambia mgombea mwingine HUSHINDI BTW polisi kujibizana na raia duniani ni jambo la kawaida sana
 
Upumbavu kulazimisha police ajitambue kwenye mambo ya siasa. Hiyo siyo kazi yake.
Raia tuwatii police siyo kurumbana nao.

Huwezi Fanya marumbano na mtu aliyebeba bunduki. Utapigwa risasi na siasa zako. Jitabue unabishana na bunduki siyo mwanasiasa mwenzako.
Trained to shoot not to politicize.
we ni mwanaume au mwanamke? polisi aliyebeba bunduki akikuinamisha akupumulie kisogoni inaonekana utakubali! sio kwa ulofa huo
 
Kifupi taaluma nyanja zote imeingiliwa na siasa. Polisi pamoja na uduni wa elimu yao, wapo karibu sana na wananchi, ni nadra siku kupita hamjapigana kikumbo. Hawajui sheria na ni waoga kama mbwa koko.
 
Kwahiyo hapo unaona umeongea pointi sana? Haki na wajibu. Polisi watimize majukumu yao kulingana na taratibu wataheshimiwa tu
 
Naona wanaokosea Ni baadhi ya police,
Kama wakifuata Sheria kwenye utendaji wao haita kua shida.
Kinachoonekana Ni baadhi ya police kutofuata taratibu za Kisheria kwenye utendaji wao kuonyesha upendeleo wa waziwazi.

Hapo uwezi kusema mtuafuate Sheria bila shuruti maana hapo kunakua hamna Sheria , rather ni uonevu.
Na kwenye uonevu lazima mtu ajitetee.

Police inpaswa ifanye kazi ki weledi.
Wanao enda nje ya taratibu za kazi ndio wanafanya Raia ajibizane nao. Na ndio wanao haribu uhusiano unaopaswa kuwepo kati ya Raia na police.


Kuwaachia police wanaofanya kazi namna hii italeta shida baadae. Sio vizuri serikali kuachia itufikishe huko.

Police wanaweza kuchukiwa na Raia kwa kuonekana wanafanya kazi kwa upendeleo. Sio Jambo zuri.
 
Never on earth a normal and sound mind can obey an illegal order. The police force has to change with the changing social, cultural, and political environment. Ndugu mtoa uzi: Your minds and attitudes seem to be in the slavery and colonial days.
 
..Polisi anatakiwa apokee maelekezo toka kwa viongozi wa kiraia / wanasiasa.

..Polisi wetu waachane na tabia ya kufokea, na kudhalilisha, viongozi wa kiraia na haswa wanasiasa wa upinzani.
 
Kama hawajui mipaka ya kazi zao tutajibishana nao tu mbele kwa mbele. Iweje watumike na maccm kuvunja sheria za Nchi mchana kweupe halafu tuwanyamazie? Tutapambana na mkoloni mweusi na vibaraka vyake kokote kule iwe polisiccm au tumeccm na kokote kule.
 
Kuhoji ni muhimu sana ili kujua uhalali wa unachoambiwa. Hata polisi kiapo chao kinasema watii amri halali siyo kila amri ni kutii.
Huo ndiyo utawala wa sheria.
 
Mwandishi una akili ndogo tu ndicho kinachokusumbua, mtu hapaswi kumheshimu polisi bali sheria, kitu kidogo namna hii unashindwa kuelewa.!

Tatizo madikteta huwatumia hao polisi kama nyenzo za kufanikisha utawala wao wa kiimla na ndipo vibaraka wa utawala wa kidikteta huja na fikra kama zako.

Katika nchi inayotawaliwa kiimla polisi hujihisi kuwa juu ya sheria na wao hushurutisha raia kutii sheria zote zikiwemo zile kandamizi huku wakiwa na mamlaka ya kutoa adhabu pasipo kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

That's where this country has reached.
 
Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii Sheria bila Shuruti kwa sababu mabishano kati ya Polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama Taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
We suppose to focus according our direction according our environment that's only way we can help our peoples no body should come and say that he is there to save the problems of our peoples we are the one we are leader we suppose to change the direction ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo OCD wa HAI yuko right kabisa kumuambia Mbowe atashindwa na Mbowe yuko wrong kumjibu hatoshindwa
 
Ni vema wanasiasa wakapewa elimu ya kutii Sheria bila Shuruti kwa sababu mabishano kati ya Polisi na wanasiasa sasa yameanza kuzoeleka na hilo si jambo jema.

Huko nyuma tumewahi kuwaona akina Adam Malima, Dkt. Kigwangalla, Nape, Sugu, Lissu, Mdee na Bulaya na sasa ni kiongozi mkuu wa upinzani Mbowe.

Kama Taifa nadhani kura mahali tunakosea, Tujirekebishe!

Maendeleo hayana vyama.
Uaskari polisi ni huduma kama zilivo huduma nyengine. Ni kukosa tu ustaarabu ndo maana tunahalaisha misemo kama " unauliza makofi polisi?"
 
Back
Top Bottom