The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kumekuwa na kautamaduni ka viongozi na mashabiki wa upinzani kuwasifia viongozi wa CCM pindi wanpokuwa wamestaafu toka kwenye majukumu yao ya kiserikali/chama.
Utamaduni huu unawachanganya wananchi hasa wale wenye uwezo mzuri wa kutunza kumbukumbu, kwani mara nyingi unakuta huyu mstaafu wanae msifu kwamba alikuwa mtu mzuri sio kama wa sasa, walimshambulia na kumtupia kila taka.
Kwa hiyo wananchi wanavyoona mnasifia wastaafu wa CCM, wanajua kwamba kumbe hata hawa mnaowatukana leo wakistaafu mtakuja na ngonjera nzuri mlizowatungia za kuwasifu.
Na hii pia nimegundua kwamba husababishwa na kufanya siasa kwa mihemko yaani unakosoa kutukana au kushabikia bila upeo mkubwa wa kupima mambo.
Tufanye siasa kwa utulivu na upeo mkubwa.