Hii timu si ya wananchi bali ni ya Matajiri!!

Hii timu si ya wananchi bali ni ya Matajiri!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Wananchi hawasajili wala hawachangishani fedha za kusajili. wanaosajili ni mtajiri. Ila wananchi bado wanasema timu ni yao

Wananchi hawatoi hela za kuendeshea Klab, mitaani wanajisifu timu ni yao.

Wananchi hawajui hata Jezi wanazovaa mitaani zimeiingizia Klab shilingi ngapi, ila matajiri wanajua wao hawajui.

Wananchi wanaambiwa tu kuwa Klab imeingia mikataba "minono" na makampuni mbali, ila hawajui hela za mikataba hiyo zinaingia kwenye Akaunti gani ya Klab. Matajiri wanajua wao wananchi hawajui

Sasa matajiri ndiyo wanaamua nani awe ama asiwe kiongozi kwenye Klab yao, wao wananchi wamebakia kutetema tu uongozi uko mikononi mwa matajiri.

Nyie wananchi mnawezaji kusema hii timu ni yenu wakati kila kitu kinafanywa na matajiri na siyo nyie??
 
Wanachi waliwekeza muda mrefu ndio maana unaona hao matajiri wanakuja wao kuwekeza!! Hiyo Logo ya yanga ni pesa tosha kuliko hata hizo za tajiri. Mtaji wa watu ni mkubwa ndio maana hata leo GSM au Mo akitoka yanga/ Simba bado timu haziwezi kosa mwekezaji.

Tatizo lako ulianza kunywa ulanzi 😅😅😅🏃
 
Back
Top Bottom