Hii video ya wanafunzi wa Primary wakiwa wanasubiri mwendokasi hadi Saa 2 Usiku inafikirisha

Hii video ya wanafunzi wa Primary wakiwa wanasubiri mwendokasi hadi Saa 2 Usiku inafikirisha

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Kuna hii video nimekutana nayo ambapo hawa wanafunzi wanasemekana wamekaa hapo kwa mwendokasi kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku.

 
Tanzania ni nchi inayotaka dikteta mzuri kuliko mwana democrasia mbovu !

Wote ni wabaya ila dictatorship nzuri ni bora kuliko democrasia mbaya ilopitisha mzembe kama samia

Britanicca
Na haya ndiyo mawazo yangu, ndiyo sababu nilichagua kumuunga mkono Magufuli.
Haya ndiyo mawazo ya Kamanda mstaafu mmoja wa Polisi aliye ongoza Dar miaka ya 2000 na kitu. .
Nilimsikia akiongea kwenye mahojiano ya TV. Yule muhaya mwenzio ndugu yake Mama Prof. Anna Tibaijuka.
Wananchi wengi tu Wana mawazo haya.
 
Inasikitisha sana atachelewe kurudi na bado atatakiwa kuwahi shule na asubuhi pia mambo ni yale yale tu.

Huu mradi wa Mwendokasi na mabasi yake unakera sana, juzi nilipanda mwendokasi Kisutu to kimara, imefika shekilango ikaanza kuzingua, ubungo flyover ilipanda kwa shida sana mbele kidogo ikazima m, dereva akashuka kucheki shida nini ikawaka tukaendelea kwa mwendo wa kobe, kuunguruma kwingi lakini ikageuka mwenda pole na ikazima tena katikati ya barabara. Akaifosi ikafika korogwe nikaona cha kujiweka matatizoni ni nini na kuna usafiri mwingine, nikashuka na baadhi ya abiria wengine nao walishuka na sababu ilikuwa ni hiyo. Baada ya kushuka nikaicheki ikiondoka, nyuma imefunguliwa sehemu ya injini, inatoa moshi mweusi mwingi sana sijui kama walifanikiwa kufika kimara mwisho kwa hali ile.
 
Back
Top Bottom