Hii wiki itakuwa ndefu sana - karibu tuzogoe!

Hii wiki itakuwa ndefu sana - karibu tuzogoe!

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
15,052
Reaction score
36,866
Wale ambao kibaruani pasua kichwa, home napo kupo kama hakupo, siasa na mambo ya nchi yanatuumiza vichwa na mioyo - tukutane hapa tubadilishane mawazo.

Kama unajisikia kujibu maswali, fanya hivyo. Kama hutaki, utakua umetumia vizuri uhuru wako wa kuchagua!
  1. Ukipewa nafasi ya kumuondosha fisadi mmoja hapa duniani, unamtanguliza nani?

  2. Nani umeshindwa kumsamehe kwenye maisha yako, na kwanini?

  3. Nini hukukifanya halafu ukajutia baadaye?

  4. Kwa sisi ambao bado tunaweweseka tukilala baada ya kushuhudia damu na ubongo wa watu kwenye matukio ya Oktoba 29 na 30 , tufanye nini kurudi kuwa sawa?

  5. Muulize mwanaJF yoyote humu swali la kizushi.

Alamsiki!
 
1. MR SMILE

2. kijana wa kuitwa A, kwa alichonitendea, siwezi kumsamehe kamwee.

3. Kuna mtu aliniomba nimsaidie kufanya jambo lake, ila mie nikakataa, kumbe nilikua napishana na fursa. Najutia sana.

4. Sijui.

5. Mjep vipi bado unanipendaa??
 
Y itakuwa ndefu?
Tunachoka, kila kona habari, mara bunge, mara kesi za kubambikiwa, mara kuachiliwa huru, ukigeuka huku video zaidi za polisi, sema ndiyo hivyo tu nimeshazoea mambo ya mtandao, ila ilitakiwa nitoke online, nijidetox kwa muda.
Nafikiria kujikumbusha kupika maandazi na vitumbua ninenepe tena, nipike mimi sio Dada. Nimevitamani vyote vya nazi ikiwemo 😋😋😋
Vitumbua vya nazi 😍 na mimi nimetamani
 
Back
Top Bottom