Hii wiki itakuwa ndefu sana - karibu tuzogoe!

Hii wiki itakuwa ndefu sana - karibu tuzogoe!

Wale ambao kibaruani mambo pasua kichwa, home napo kupo kama hakupo, siasa na mambo ya nchi yanatuumiza vichwa na mioyo - tukutane hapa tubadilishane mawazo.

Kama unajisikia kujibu maswali, fanya hivyo. Kama hutaki, utakua umetumia vizuri uhuru wako wa kuchagua!
  1. Ukipewa nafasi ya kumuondosha fisadi mmoja hapa duniani, unamtanguliza nani?

  2. Nani umeshindwa kumsamehe kwenye maisha yako, na kwanini?

  3. Nini hukukifanya halafu ukajutia baadaye?

  4. Kwa sisi ambao bado tunaweweseka tukilala baada ya kushuhudia damu na ubongo wa watu kwenye matukio ya Oktoba 29 na 30 , tufanye nini kurudi kuwa sawa?

  5. Muulize mwanaJF yoyote humu swali la kizushi.

Alamsiki!
1-thamani ya uhai ni kubwa sana haidhuru huyo aliye hai ni mhalifu kiasi gani, kwa hio upande wangu siwezi kufanya hivyo kwa yoyote.

2- hakuna hata mmoja binadamu ila umaskini ni adui yangu, siwezi kuusamehe.

3- nyeto! Sijui kwa nini kuna msuto wa nafsi kiasi hicho.

4- angalia mara nyingine, tena rudia, ukijiwa na machozi lia, kisha sali kwa imani yako kuomba Rehema za Mungu, msamaha na uponyaji wa mioyo iliyo jeruhika.
 
5.... nakupenda nataka uwe mshangazi wangu..... aaaah maisha mafupi bn..... watu wamekufa kama kumbikumbi.... tuinjoy hii pumz tulonayo....😊 😃... Besides za chugg/dsm ? Uko poA?
Haa haaa manaake hapo kwanza nicheke 🤣
Rudi kule chocho ukanishushie mistari kwanza.
 
Back
Top Bottom