Hii ya Mwanasheria mkuu (AG) kushtakiwa kwa makosa yaliyotendwa na Rais kama taasisi au mtu binafsi akiwa madarakani nimeikubali

Akiamrisha, AG ana uwezo wa kikatiba wa kumzuia Rais kutekeleza jambo analotaka?

Ni ujinga wa hali ya juu kuwa na sheria kama hii. Atashtakiwaje mtu ambaye hana uwezo wa kumzuia Rais kutenda kosa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukishindwa kumzuia unajiuzulu tu.

Mbona mzee Mtei alijiuzulu japo ilikuwa ni nafasi tofauti!
 
Chalinze waandamane kudai haki zao za msingi kama maji na umeme Rais aamuru police force kumuua kiongozi wa waandamanaji, polisi watekeleze halafu mwanasheria mkuu ambaye hana cheo cha u Amiri jeshi mkuu ashitakiwe!!!!!
Very stupidity
Unaelewa majukumu ya AG lakini?
 
chini ya sheria hii, yeyote atakayekuwa anakubali kuteuliwa kama AG lazima atakuwa ama ni psychiatric case ama ni msukule!
 
Bunge lipi??

Siku hizi watz tuna bunge?

Ninavyojua,siku hizi nec ya ccm ndiyo wanaojifanya bunge,kiongozi wao ni yule mgonjwa Ndugayi
 
Utopolo rais inabidi ashitakiwe!!
 
Msingi uliopelekea kuandikwa kwa katiba kongwe duniani “magna carter” ilikuwa ni kudhibiti wafalme wasifanye mambo kwa utashi wao.

Kutumia hiyo hiyo magna carter waingereza wakachinja Charles the 1 kwa madai ya uhaini wa taifa, kwa ivyo hakuna mtu anatakiwa kuwa juu ya national interest.

Unapoweka sheria inayosema wale wenye mamlaka awawezi shitakiwa kwa maamuzi yao au matendo wakati walipokuwa madarakani sio tu kwamba unakabidhi mustakabali wa nchi kwa watu wachache bali unaenda against principles muhimu kadhaa za katiba.

Usione katiba tu imeandikwa kila sura ina principles zake sasa hiyo sheria inaenda weka:
Power legitimacy kwa viongozi wa juu kufanya wanavyoweza wakiwa kwenye hizo nafasi.

Inavunja misingi ya protection of freedom maana wenye mamlaka hawana limitations ya vitu wasivyoweza fanya kesho raisi anaweza sema piga risasi waandamanaji wote awezi shitakiwa.

Inavunja principles za stability maana uwezi jua kesho PM au Speaker atakuja na wazimu gani kutokana na kwamba awawezi shitakiwa na kuondoa dhana nzima ya predictability serikalini.

You can go on and on..... ni sheria mbovu, sasa sijui constitution lawyers wanafanya nini wakati huu upuuzi unatendeka.
 
Anyway labda mkuu nisaidie kwa ufafanuzi maana sijaona akifafanua chochote hapo ili inisaidie mimi kutambua ana amini nn,hiyo itanipa fursa ya mimi kutoa maoni yangu
Mkuu jamaa ameongea kinyume au kejeri,Soma katikati ya mistari utamuelewa
 
Kabla hawajaipitisha hili,ingetakiwa AG ale kiapo kwa niaba ya Rais,pm,vp na sp ili kutoa utata huu,maana huwez kubeba mzigo wkt walioapa kuilinda katiba ni wengine
 
Kwani juzi spika alivyoshtakiwa nn kilipungua?
Kama hoja ni viongozi wa mihimili why wazir mkuu? Kwa nn KUB hakuingizwa kama viongozi wa kitaifa?
Ukipata majibu nitag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…