Nilidhani mnajua kuwa msimu huu ndiotunajenga timu baada ya kuwaacha baadhi ya wachezaji kufuatia viwango vyao. Tuwe wakweli, Tambwe alishafika mwisho kwa umri ule. Makambo mpira ni biashara pia, timu haikuwa na fedha kipindi anauzwa. Kamusoko pia tayari pancha za uzeeni zishaanza. Timu ilihitaji vijana wenye kasi. Tatizo tunasahau upesi mno, mnataka kushinda tu, kwa timu gano hasa mliyokuwa nayo msimu uliopita? Ajibu hakuachwa, aliwapiga chenga viongozi akapewa mkataba wa awali na mikia. Swali kwenu enyi walalamikaji, mlikuwa na pesa ya kumwongezea mkataba Ajibu kabla haujaisha? Vipi kwa Gadiel ilikuwaje kwani?
Nawasihitusiwe wajuaji wengi, tutavuruga timu kwa kusikiliza maneno ya mbumbumbu fc. Zahera tunamjua tangu msimu uliopita, no ujinga kumtilia shaka kwa mechi za awali kwenye timu changa. Huo sio mpira hata kidogo, ni ushabiki wa vijiweni.