Hii Yanga ya Zahera imeanza kunipa wasiwasi

Hii Yanga ya Zahera imeanza kunipa wasiwasi

Kuna tofauti kati ya lawama na maoni. Ona mdau aliyetoa maoni hapo juu 3llyEmma: kwa kuchambua mechi za awali. Hayo ni maoni, lakini mtu anayembeza kocha na wachezaji hatoi maoni. Pia unalalamika kwa mechi moja tu,unajua mpira? Unasema timu ni mpya halafu unalalamika, unasema timu iliachawachezaji wakati mpaka msimu unaisha timu ina madeni tupu, huoni haya si maoni tena bali ni mtazamo hasi? Tunasahau tulipotoka
Kweli ni mapema sana kutoa lawama, ukizingatia ndio inaanza.
 
Kuna umuimu wakupata beki namba mbili mbadala wa Gadiel uyu Ally Mtoni awezi kabisa ziba pengo la Gadiel.
Ni namba 3 hiyo, yuko Marcelo ila kuna kipindi walitaka kumrudisha David Luhende. Hata Mwjnyi Haji alikuwa mzuri tabu uvivu.
 
Mmmmh ok...nilidhani kuwa tunatoa maoni ya kujenga kwa ajili ya timu kumbe wengine mnaona ni ushabiki wa mmnachoita vijiweni...kwa hiyo wote tuwe na mawazo yanayofanana kwa ajili ya timu...kwa hiyo maoni yako tofauti na mimi (sisi) siyo ya kijiweni ila sisi ndiyo ya kijiweni...wewe ndiye unayejua lililo jema na baya kwa timu ..very interesting...unaweza ukawa na hoja lakini uwasilsishaji wako wa hoja ulioambatana na dharau na kejeli kwa wengine wenye mawazo tofauti na wewe una walakini sana...anyway niishie hapa maana mwelekeo wake nadhani itakuwa ni kurushiwa matusi....sioni hata na haja kuendelea kutoa maelezo ya kilicho nyuma ya sualala Ajib, Gadiel, Tambwe na Makambo...
Hoja ni kuwa wavurugaji wa timu ni sisi wenyewe. Kilichonyuma hata mimi nakijua, ilikuwa kipindi kigumu kile. Kw nini basi tusiwape nafasi kwanza kabla ya kutoa conclusion? Huoni kuwa lawama za mapema namn hii yatasababisha watu kuanza kugawanyika wakati timu ndio kwaaza inatafuta muunganiko?
 
Hoja ni kuwa wavurugaji wa timu ni sisi wenyewe. Kilichonyuma hata mimi nakijua, ilikuwa kipindi kigumu kile. Kw nini basi tusiwape nafasi kwanza kabla ya kutoa conclusion? Huoni kuwa lawama za mapema namn hii yatasababisha watu kuanza kugawanyika wakati timu ndio kwaaza inatafuta muunganiko?
Haya muzee, tuone inakuwaje.
 
Hoja ni kuwa wavurugaji wa timu ni sisi wenyewe. Kilichonyuma hata mimi nakijua, ilikuwa kipindi kigumu kile. Kw nini basi tusiwape nafasi kwanza kabla ya kutoa conclusion? Huoni kuwa lawama za mapema namn hii yatasababisha watu kuanza kugawanyika wakati timu ndio kwaaza inatafuta muunganiko?

Nakubaliana na wewe ila kuna namna ya kutoa maoni ya kujenga na kubomoa...hapa ni lazima tutofautishe...ikiwa tunaanza kumlaumu kocha kuwa hafai sijui na viongozi hawafai na wachezaji nao ni nini sijui, hapo ni tatizo..lakini kama mnajadiliana kuwa tumekosea wapi jamani tufanye nini, sioni tatizo...halafu ukianza kuwashutumu wanaotoa maoni positive kwa kuyaita maoni yao kuwa eti ni ya vijiweni hapo ni tatizo hapo ndipo ulipo mgawanyiko..Mimi Yanga naifahamu mno...kwa namna ninavyoifahamu Yanga ipo kiganjani..nimeitumikia Yanga mno na hata wakati mwingine kujitoa mhanga ...lakini wapo wanayanga wasioifahamu klabu hii ila wako mbele kuwashutumu viongozi na kocha na kuwashutummu hata wale wanaotoa maoni ya kujenga...Binafsi bado naamini kulikuwa na tatizo kwa mechi ya jana...ligi ya hapa nyumbani baadhi tunaifahammu ni ya 'kihuni' ..wachezaji mle ndani uwanjani hukamiana sana na hutukanana sana..na Yanga ndio hukamiwa zaidi na wachezaji wetu huambiwa maneno mabaya sana uwanjani ..mara ninyi mamilionea mnakula hela za bure tunataka kuwaonesha leo na kadhalika...kwa hiyo ukiweka wachezaji wengi wa kigeni na wapya ni tatizo ..ni lazima kuwe na balance ya nyota wapya/wageni na wa msimu uliopita ...wachezaji wa hapa ndani wanafahamiana kwa hiyo ni rahisi nao kucheza 'kibabe' Mimi binafsi naamini Yanga imesajili wachezaji wazuri sana ila mazingira ya hapa kwa ligi ya ndani wanahitaji muda kuzoea...hata Ngoma mara ya kwanza alipotua Yanga tulimponda lakini alipozoea akawa tishio...Chirwa naye tulimponda awali lakini baadaye akawa tishio...Hata Makambo alianza vibaya na baadaye ndipo akawika...Kwa hiyo hata nyota wetu wa kigeni wapya watawika tu ila inahitaji muda kidogo...na tukitoa maoni kuwa kwenye ligi ya kwetu (ambayo imejaa mizengwe na ubabe uwanjani na nje ya uwanja) tuanze kwa ku-balance wachezaji wetu tusipuuzwe tu kuwa eti hayo ni mawazo ya kijiweni...Baadhi tunapata taabu kuambiwa hivyo na watoto wadogo ikizingatiwa kuwa wengine sisi siyo tu tumecheza mpira bali pia tumepata bahati ya kuongoza soka kwa ngazi za juu kabisa kitaifa...
 
Toka mechi za majaribio mpaka hizi za kimashindano timu yangu ya Yanga SC chini ya Mwinyi Zahera imeanza kunitia shaka sana, tena sana tu. Zahera naona alianza kupotea maboya toka msimu ulopita kwa jjinsi alivyoshughulikia suala la Yondani na Kakolanya na pia kumpa unahodha Ajibu.
Kwa hii timu ya sasa nayaona haya:
1. Timu haina mpangilio toka nyuma hadi mbele
2. Hatuna m(wa)shambuliaji wa kutegemewa-mtu wa kumaliza mechi
3. Timu ya kwanza imejaa wageni wa nje wasio na uwezo mkubwa
4. Kocha mbishi sana na hataki kubadilika
5. Si busara kumpa unahodha mgeni na wenyeji wazoefu wapo
6. Kocha anakosa mbinu za kufanya wakati mechi inaendelea hasa tukiwa tumefungwa
7. Kuna wachezaji hawakustahili kuachwa au kuuzwa; Kamusoko, Tambwe, Makambo hata Ajibu
8. Kocha kapunguziwa majukumu sasa afanye kazi yake
9. Timu haina wachezaji wenye 'fighting spirit', wapo wapo tu
10. Timu haina kiongozi ndani ya dimba-nahodha anapwaya
11. Zahera kwa sasa kashika kitasa kilichoandikwa Exit Door ( In Edo Kumwembe's voice)

Kwa sasa yangu ni hayo tu.
Nadhani ni suala la kumpa muda na kuwekeana malengo baada ya kufanya usajili kulingana na matakwa yake.
Tunataka ku achieve nini mwisho wa msimu? Aambiwe kwanza tuchukue ubingwa au nafasi ya pili pamoja na kombe la FA. Akishindwa kufikia malengo hayo, itakuwa vyema aondolewe.
Sasa hivi ni mapema sana
 
Hoja ni kuwa wavurugaji wa timu ni sisi wenyewe. Kilichonyuma hata mimi nakijua, ilikuwa kipindi kigumu kile. Kw nini basi tusiwape nafasi kwanza kabla ya kutoa conclusion? Huoni kuwa lawama za mapema namn hii yatasababisha watu kuanza kugawanyika wakati timu ndio kwaaza inatafuta muunganiko?
Sawa muzee.
 
Nilidhani mnajua kuwa msimu huu ndiotunajenga timu baada ya kuwaacha baadhi ya wachezaji kufuatia viwango vyao. Tuwe wakweli, Tambwe alishafika mwisho kwa umri ule. Makambo mpira ni biashara pia, timu haikuwa na fedha kipindi anauzwa. Kamusoko pia tayari pancha za uzeeni zishaanza. Timu ilihitaji vijana wenye kasi. Tatizo tunasahau upesi mno, mnataka kushinda tu, kwa timu gano hasa mliyokuwa nayo msimu uliopita? Ajibu hakuachwa, aliwapiga chenga viongozi akapewa mkataba wa awali na mikia. Swali kwenu enyi walalamikaji, mlikuwa na pesa ya kumwongezea mkataba Ajibu kabla haujaisha? Vipi kwa Gadiel ilikuwaje kwani?

Nawasihitusiwe wajuaji wengi, tutavuruga timu kwa kusikiliza maneno ya mbumbumbu fc. Zahera tunamjua tangu msimu uliopita, no ujinga kumtilia shaka kwa mechi za awali kwenye timu changa. Huo sio mpira hata kidogo, ni ushabiki wa vijiweni.
Uko sawa kabisa.!
 
Yanga 1-1 Kariobangi Sharks
Yanga 1-1 Township R
Township 0-1 Yanga
Yanga 0-1 Ruvu Shooting.
Kwa jinsi matokeo yalivyo kwenye mechi hizo 4 Ambazo 3 ndio game za mashindano unapata majibu kuwa safu ya ushambuliaji haiko sawa.
Haiko sawa kwa maana wote kule mbele ni wageni hawana muunganiko mzuri tofauti na eneo la ulinzi ambalo lina wageni + wenyeji ndio maana timu hairuhusu magoli hovyo.
CHA MSINGI NI..?
Je viungo wachezeshaji na winga wanapika nafasi za magoli lakini washambuliaji wanapoteza?
Au washambuliaji wanafata mipira nyuma sana baada ya viungo kushindwa kazi yao na kufanya mbele kukosa nguvu??
Jibu litabaki hakuna muunganiko mzuri wa kushambulia kuanzia katikati kwenda mbele... Kiungo namba 8 NA WINGA ZOTE ya juu na chini wanatakiwa kupika nafasi za maana sio blaa blaa ilimradi tu mpira umeenda mbele bila uelekeo sahii na lawama zinabaki kwa washambuliaji.. Sasa hii ni kazi ya kocha kuweka watu sahihi au kurekebisha.
Kwa mechi hiz chache walizocheza Yanga namuona BALAMA ana nafasi kubwa.
Mkuu huwa nakuelewa sana,najua wewe n Simba,but when come kwenye maswala ya uchambuzi huwa uegemei upande mmoja..hichi ulicho andika hapa n 100% haina ubishi.
 
Mkuu huwa nakuelewa sana,najua wewe n Simba,but when come kwenye maswala ya uchambuzi huwa uegemei upande mmoja..hichi ulicho andika hapa n 100% haina ubishi.
Great article....
 
Back
Top Bottom